Miaka miwili ya kupotea kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi Azory Gwanda

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Leo (21/11/2019) imetimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa magazeti ya #Mwananchi na #TheCitizen Azory Gwanda kupotea huko Kibiti, Wilaya ya Rufiji baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana. #Miaka2BilaAzory

1574341630381.png

======
Leo inatimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa habari, Azory Gwanda atoweke katika mazingira ya kutatanisha.

Dar es Salaam. Leo inatimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa habari, Azory Gwanda atoweke katika mazingira ya kutatanisha.

Katika kuadhimisha kumbukumbu yake, Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd imepanga kupanda mti na kuzindua picha maalumu kama ishara ya heshima na utambuzi wa mchango wa mwandishi huyo katika tasnia ya habari nchini.

Gwanda anasadikika kuchukuliwa na watu wasiojulikana wakati matukio ya mauaji yalipokuwa yakitokea mara kwa mara katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Alikuwa akiandika habari hizo wakati taarifa za kutoweka kwake zilipoibuka mara ya kwanza. Habari hizo zilikuwa zikichapishwa katika matoleo kadhaa ya magazeti ya The Citizen na Mwananchi. Tangu kutoweka kwake, hakuna kinachojulikana kuhusiana na hatima ya kupatikana kwake.

Serikali imekuwa ikisema inachunguza anapoweza kuwepo pamoja na matukio ya watu wengine yanayofanana na ya Gwanda, hadi sasa hakujawa na matokeo yoyote yanayoweza kusaidia kupatikana kwake.

Katika siku za karibuni kumekuwa na matamko mbalimbali kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari na mashirika yao ikiwamo Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) kuitaka Serikali kulipa kipaumbele tatizo la kutoweka kwa Gwanda huku kampeni kama vile #MrudisheniAzory zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Mwaka jana, Gwanda alishinda Tuzo ya Daudi Mwangosi kama hatua ya kutambua mchango wake katika tasnia ya habari nchini. Tuzo hiyo huandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania kama kumbukumbu ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ambaye aliuawa na polisi wakati wa maandamano yaliyotokea Iringa, Septemba 2012.

Mei mwaka huu, jina la Gwanda lilikuwamo katika orodha ya “Kesi 10 Muhimu” za waandishi wa habari duniani kote zilizokusanywa na shirika la One Free Press Coalition, ambalo ni mjumuiko wa wahariri mashuhuri 30 wa vyombo vya habari vya Reuters, Quartz, The Financial Times, India Today, TIME, Washington Post na vyombo vingine. Wahariri hao hutumia ushawishi wao kuwatetea waandishi waliofikwa na majanga mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Katika mahojiano yake na BBC, katika kipindi cha ‘Focus on Africa’, Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi alisema Gwanda alikuwa amepotea na kuuawa katika wilaya ya Rufiji, akiongeza kwamba serikali imeweza kudhibiti ugaidi katika eneo hilo.

Hata hivyo, baadaye Profesa Kabudi alikanusha taarifa kwamba amethibitisha kifo cha Gwanda badala yake alisema kwamba watu hawakuelewa vizuri kile alichokisema.

Alisema kwamba alichokuwa anamaanisha ni kwamba kilichojitokeza mkoani huko ni kitu kibaya kuwahi kutokea na kilipelekea watu wengi kupotea na hata wengine kuuawa.

Chanzo: Mwananchi
 
Attachments

  • 1574341502598.png
    1574341502598.png
    333.6 KB · Views: 13
Haijulikani alipo Azory na wala haijulikani kama alikufa au lah. Ila kampuni ya Mwananchi ikiadhimisha tukio la miaka miwili tangia mwandishi huyo wa habari za kiuchunguzi kupotea ilikuwa ni kama kufanya kumbukizi ya msiba.

Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa na majonzi wameamua kuzindua picha maalum ya Azory pamoja na kipanda mti wa kumuenzi. Inasikitisha sana.

Tukio linalosikitisha zaidi ni kitendo cha aibu kubwa kinachofanywa na utawala huu wa awamu ya tano kuficha ukweli juu ya kilochomtokea mwandishi huyu.

Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa kwa utawala wowote ule duniani ambao umechaguliwa na wananchi kupitia kura.

Ni aibu sana kuona watu kama Azory na Ben wakipotelea mbali huku mamlaka ikichukulia matukio haya kama mambo ya kawaida kabisa.

Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu na kutekwa kwa watu mbalimbali nchini huku wakirudishwa wakiwa na ulemavu ama majeraha huku serikali ikiyachukulia mambo haya kimzaha mzaha ni jambo la kufedhehesha na linaloondoa heshima ya utawala wowote ule duniani.

Utawala unaochukulia mambo kama haya kwa jinsi hii ni utawala unaoitwa uliokosa ustaarabu kupita kiasi na katu haufai kupewa heshima yoyote ile mbele ya jamii ya wacha Mungu na wenye walau kiwango cha kawaida cha utu ndani yake.
 
Disappeared and died.
Aisee
Leo (21/11/2019) imetimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa magazeti ya #Mwananchi na #TheCitizen Azory Gwanda kupotea huko Kibiti, Wilaya ya Rufiji baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana. #Miaka2BilaAzory

View attachment 1268263

======
Leo inatimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa habari, Azory Gwanda atoweke katika mazingira ya kutatanisha.

Dar es Salaam. Leo inatimia miaka miwili kamili tangu mwandishi wa habari, Azory Gwanda atoweke katika mazingira ya kutatanisha.

Katika kuadhimisha kumbukumbu yake, Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd imepanga kupanda mti na kuzindua picha maalumu kama ishara ya heshima na utambuzi wa mchango wa mwandishi huyo katika tasnia ya habari nchini.

Gwanda anasadikika kuchukuliwa na watu wasiojulikana wakati matukio ya mauaji yalipokuwa yakitokea mara kwa mara katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Alikuwa akiandika habari hizo wakati taarifa za kutoweka kwake zilipoibuka mara ya kwanza. Habari hizo zilikuwa zikichapishwa katika matoleo kadhaa ya magazeti ya The Citizen na Mwananchi. Tangu kutoweka kwake, hakuna kinachojulikana kuhusiana na hatima ya kupatikana kwake.

Serikali imekuwa ikisema inachunguza anapoweza kuwepo pamoja na matukio ya watu wengine yanayofanana na ya Gwanda, hadi sasa hakujawa na matokeo yoyote yanayoweza kusaidia kupatikana kwake.

Katika siku za karibuni kumekuwa na matamko mbalimbali kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari na mashirika yao ikiwamo Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) kuitaka Serikali kulipa kipaumbele tatizo la kutoweka kwa Gwanda huku kampeni kama vile #MrudisheniAzory zikiendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Mwaka jana, Gwanda alishinda Tuzo ya Daudi Mwangosi kama hatua ya kutambua mchango wake katika tasnia ya habari nchini. Tuzo hiyo huandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania kama kumbukumbu ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ambaye aliuawa na polisi wakati wa maandamano yaliyotokea Iringa, Septemba 2012.

Mei mwaka huu, jina la Gwanda lilikuwamo katika orodha ya “Kesi 10 Muhimu” za waandishi wa habari duniani kote zilizokusanywa na shirika la One Free Press Coalition, ambalo ni mjumuiko wa wahariri mashuhuri 30 wa vyombo vya habari vya Reuters, Quartz, The Financial Times, India Today, TIME, Washington Post na vyombo vingine. Wahariri hao hutumia ushawishi wao kuwatetea waandishi waliofikwa na majanga mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Katika mahojiano yake na BBC, katika kipindi cha ‘Focus on Africa’, Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi alisema Gwanda alikuwa amepotea na kuuawa katika wilaya ya Rufiji, akiongeza kwamba serikali imeweza kudhibiti ugaidi katika eneo hilo.

Hata hivyo, baadaye Profesa Kabudi alikanusha taarifa kwamba amethibitisha kifo cha Gwanda badala yake alisema kwamba watu hawakuelewa vizuri kile alichokisema.

Alisema kwamba alichokuwa anamaanisha ni kwamba kilichojitokeza mkoani huko ni kitu kibaya kuwahi kutokea na kilipelekea watu wengi kupotea na hata wengine kuuawa.

Chanzo: Mwananchi
 
Mungu amsaidie huko aliko kama yuko hai au amefariki..sijui waliofanya hivyo wanajisikiaje
 
Back
Top Bottom