Simshangai Leticia Nyerere

Simshangai Leticia Nyerere

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
202
Reaction score
1,588
Aliyeleta pesa, alileta mfarakano,
Mioyo ya watu imeteka, inaleta utengano,
Mwenye kumiliki nyingi pesa, aweza fanya lolote agano,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.

Yesu aliuzwa kwa wayahudi, sababu ilikua pesa,
Hata John aweza jiita "Iddi", kama ukimuahidi pesa,
Leticia mwana wa Mageni Musoni, shilingi inamtesa,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.

Laki tatu na nusu kwa siku, nani asiyezitaka?
Wakulima wa tumbaku, wazipata mwisho wa mwaka,
Waalimu wenye uzoefu, mwezi mzima wazisaka,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.

Leticia Madaraka Nyerere, pesa imempofusha,
Hawezi tena kuona mbele, kisa posho za Katiba,
Hata akila matembele, macho yake keshaziba,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.

Mwizi huanza kama kibaka, akizoea haogopi tena kelele,
Leticia alimsaliti Madaraka, kitindamimba cha Mwal.Nyerere,
Mahakamani akadai talaka, lakini akaendelea kujiita "Nyerere"
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.

Mahakama ingempa mipaka, asitumie tena jina Nyerere,
Hakuna Nyerere kibaka, wala mwenye kiherehere,
Apendaye pesa za "mbaka", na kuweka tamaa mbele,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
 
Huyu mwanamke ndo maana ananangania jina wa watu

Wee si unaona hata wenyewe wenye jina wanavyo mvurumishia (kama alivyobwatukiwa na Makongoro last year?) maneno ya hovyo kila mara lakini yeye kang'ang'ana tu na jina la ukoo wa watu kisa jina kubwa. Mwenyewe hudai ati tu kwa sababu alipata kuolewa huko hawezi badilisha jina tena....

Huyu dada angekuwa ni mtu mwenye kupenda Chama chake, mwenye kujiheshimu, jitambua na kujijali asingefanya habari ya mambo ya watu wa barabarani namna hii. Huu ni umtovu wa nidhamu na hauvumiliki katika zoezi la kuleta ukombozi wa kweli. Amekuuwa kipofu wa akili na anachoona yeye ni pesa tu. Haoni maslahi mapana kwenye picha kubwa yanayopingwa na kupiganiwa na wana UKAWA.

Wahenga walisema Quote..."mnapokuwa safirini kwenye mashua (boti) na ikatokea mwenzenu mmoja analeta (hujuma) mchezo wa kuitoboa mashua ni heri mumuwahi kwa kumrusha baharini pasipo huruma aangamie huko kuliko kuja kuangamia nyote kijumla jumla.
 
Amerudi BMK kuenzi jina la aliyekuwa Baba Mkwe wake.

Lakini mbona dalili za usaliti zilishaanza kuonekana mda mrefu? Kumbuka alivyopendekeza JF ifungwe eti inawatukana viongozi wa nchi including baba wa Taifa.

Kumbuka Halima Mdee alivyomshukia baada ya kukinanga CDM ambacho ndiyo chama chake kilichompatia huo ubunge wa viti maalum.

Leticia atakumbukwa ktk historia ya nchi hii kwa usaliti wake
 
Kumbe mtu mwenyewe alishaachika na anaendelea kutumia jina la Nyerere Isivyo Hahali? Hili ni funzo kwa cdm kutokuwa makini ktk uteuzi wa hawa wabunge wa viti maalumu na nadhani halitajirudia tena.hawa wasaliti wa maoni ya watz hawafai kuwepo cdm na naunga mkono huyu chakubimbi afukuzwe mara moja kwani anatutia aibu sana sisi wasukuma wa Ngudu
 
Hao waliotoka nao warudishe zile walizochukua hapo awali.. maana kazi waliyofanya ni kazi ya bure kabisa....
 
Huyo mama anayetumia jina lililotukuka la Nyerere kwa nguvu, ataingia katika vitabu vya binadamu waliofanya usaliti mkubwa kwa ajili ya pesa, akiwa sambamba na Yuda Iskariot.

Lakini akumbuke kuwa mwenzake Yuda Iskariot, alipogundua usaliti wake, alijitia kitanzi, sina uhakika kuwa huyo mama naye, itakapofika Septemba, ambapo ndiyo muda magamba wameuweka wa ndiyo watakuwa wamekamilisha kuiandika Rasimu yao waliyoiandaa pale Lumumba, kama mission hiyo itakuwa imefeli, je huyo mama naye, atafuata nyayo za Yuda Iskariot, na ataenda dukani kununua kamba na kuitundika darini, ili ajinyonge?!!
 
Wee si unaona hata wenyewe wenye jina wanavyo mvurumishia (kama alivyobwatukiwa na Makongoro last year?) maneno ya hovyo kila mara lakini yeye kang'ang'ana tu na jina la ukoo wa watu kisa jina kubwa. Mwenyewe hudai ati tu kwa sababu alipata kuolewa huko hawezi badilisha jina tena....

Huyu dada angekuwa ni mtu mwenye kupenda Chama chake, mwenye kujiheshimu, jitambua na kujijali asingefanya habari ya mambo ya watu wa barabarani namna hii. Huu ni umtovu wa nidhamu na hauvumiliki katika zoezi la kuleta ukombozi wa kweli. Amekuuwa kipofu wa akili na anachoona yeye ni pesa tu. Haoni maslahi mapana kwenye picha kubwa yanayopingwa na kupiganiwa na wana UKAWA.

Wahenga walisema Quote..."mnapokuwa safirini kwenye mashua (boti) na ikatokea mwenzenu mmoja analeta (hujuma) mchezo wa kuitoboa mashua ni heri mumuwahi kwa kumrusha baharini pasipo huruma aangamie huko kuliko kuja kuangamia nyote kijumla jumla.

nafikiri hata matatizo yake na makongoro yatakuwa yamejikita kwenye tama ya hela
 
Mtasema yote na chama lenu la kikabila leti amekuja dodoma kutetea watanzania wange nyie na ubaguzi wenu nyamazeni.
 
Kumbe mtu mwenyewe alishaachika na anaendelea kutumia jina la Nyerere Isivyo Hahali? Hili ni funzo kwa cdm kutokuwa makini ktk uteuzi wa hawa wabunge wa viti maalumu na nadhani halitajirudia tena.hawa wasaliti wa maoni ya watz hawafai kuwepo cdm na naunga mkono huyu chakubimbi afukuzwe mara moja kwani anatutia aibu sana sisi wasukuma wa Ngudu
Mbona hata wewe umeachika tena mara mbili kwa aibu sana tu,mwambie mbowe na watu wake kama kweli wao wazalendo warudishe pesa walizojua ndipo wakazurule mitaani waliko.
 
Amerudi BMK kuenzi jina la aliyekuwa Baba Mkwe wake.

Lakini mbona dalili za usaliti zilishaanza kuonekana mda mrefu? Kumbuka alivyopendekeza JF ifungwe eti inawatukana viongozi wa nchi including baba wa Taifa.

Kumbuka Halima Mdee alivyomshukia baada ya kukinanga CDM ambacho ndiyo chama chake kilichompatia huo ubunge wa viti maalum.

Leticia atakumbukwa ktk historia ya nchi hii kwa usaliti wake
Chadema kila mtu msaliti hilo liko wazi.
 
Leo Leticia anaonekana msaliti. maneno ya kashfa. Mlipomteua kuwa mbunge viti maalum hamkujua kuwa alitalikiwa na Madaraka Nyerere?
Amewahi kugombea ubunge wa Sadc kwa baraka za chadema, leo anaitwa majina mengi.
Demokrasia gani hiyo?
 
Wee si unaona hata wenyewe wenye jina wanavyo mvurumishia (kama alivyobwatukiwa na Makongoro last year?) maneno ya hovyo kila mara lakini yeye kang'ang'ana tu na jina la ukoo wa watu kisa jina kubwa. Mwenyewe hudai ati tu kwa sababu alipata kuolewa huko hawezi badilisha jina tena....

Huyu dada angekuwa ni mtu mwenye kupenda Chama chake, mwenye kujiheshimu, jitambua na kujijali asingefanya habari ya mambo ya watu wa barabarani namna hii. Huu ni umtovu wa nidhamu na hauvumiliki katika zoezi la kuleta ukombozi wa kweli. Amekuuwa kipofu wa akili na anachoona yeye ni pesa tu. Haoni maslahi mapana kwenye picha kubwa yanayopingwa na kupiganiwa na wana UKAWA.

Wahenga walisema Quote..."mnapokuwa safirini kwenye mashua (boti) na ikatokea mwenzenu mmoja analeta (hujuma) mchezo wa kuitoboa mashua ni heri mumuwahi kwa kumrusha baharini pasipo huruma aangamie huko kuliko kuja kuangamia nyote kijumla jumla.
Duuh,haya ni mapendekezo,
 
leo leticia anaonekana msaliti. Maneno ya kashfa. Mlipomteua kuwa mbunge viti maalum hamkujua kuwa alitalikiwa na madaraka nyerere?
Amewahi kugombea ubunge wa sadc kwa baraka za chadema, leo anaitwa majina mengi.
Demokrasia gani hiyo?
s i a s a zinachanganya sana
 
ndo sheeder ya kutumia jina la mume kama babako.
 
Leo Leticia anaonekana msaliti. maneno ya kashfa. Mlipomteua kuwa mbunge viti maalum hamkujua kuwa alitalikiwa na Madaraka Nyerere?
Amewahi kugombea ubunge wa Sadc kwa baraka za chadema, leo anaitwa majina mengi.
Demokrasia gani hiyo?

Imara ya jembe kaingoje shamba. Si unajua tena kuwa huwezi kujua nguvu ya mlevi mpaka uimwage pombe yake? Wako watu tena wa maana kimtizamo wa nje ndani ya ccm ambao walipewa dhamana kubwa kubwa nchini lakini hatimaye ikajulikana kuwa si watu kitu kama walivyotizamiwa. Mazingira kama haya ya mapambano au harakati za ukombozi ndipo uwezapo kujua nani mtu na ni nani si mtu kitu! Leticia, ameshajimbanua kuwa yeye ni nani na ni mtu wa aina gani. Kwa ujumla amejiabisha!
 
Back
Top Bottom