Aliyeleta pesa, alileta mfarakano,
Mioyo ya watu imeteka, inaleta utengano,
Mwenye kumiliki nyingi pesa, aweza fanya lolote agano,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
Yesu aliuzwa kwa wayahudi, sababu ilikua pesa,
Hata John aweza jiita "Iddi", kama ukimuahidi pesa,
Leticia mwana wa Mageni Musoni, shilingi inamtesa,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
Laki tatu na nusu kwa siku, nani asiyezitaka?
Wakulima wa tumbaku, wazipata mwisho wa mwaka,
Waalimu wenye uzoefu, mwezi mzima wazisaka,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
Leticia Madaraka Nyerere, pesa imempofusha,
Hawezi tena kuona mbele, kisa posho za Katiba,
Hata akila matembele, macho yake keshaziba,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
Mwizi huanza kama kibaka, akizoea haogopi tena kelele,
Leticia alimsaliti Madaraka, kitindamimba cha Mwal.Nyerere,
Mahakamani akadai talaka, lakini akaendelea kujiita "Nyerere"
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.
Mahakama ingempa mipaka, asitumie tena jina Nyerere,
Hakuna Nyerere kibaka, wala mwenye kiherehere,
Apendaye pesa za "mbaka", na kuweka tamaa mbele,
USALITI HUU WA UKOMBOZI, SIMSHANGAI LETICIA NYERERE.