RockSpider
JF-Expert Member
- Feb 16, 2014
- 6,859
- 2,762
Maneno mazuri hayo mkuu, tatizo watz tunatafsiri kufirisika ni kutokuwa na fedha mfukoni na kuwa na vitu vichakavu, kumbe unaweza ukawa huna hela pia una vitu vichakavu lakini ukawa hujafikia level ya kufilisika. kama UDA mali zake ilikuwa mpaka Ubungo terminal na sehemu zingine za city centre maana yake walikuwa hawajachoka kilichotakiwa ni kuweka dhamana mali zake bank na kuchukua mkopo na kuja na mabasi mengine ya kisasa na kama ni kubinafsisha basi wafuate taratibu za kueleweka
Mkuu hapa tutajadili sana LAKINI ukweli unabaki kuwa a moment walipogawana Nyumba za Serikali na wananchi wakakaa kimya ndiyo siku walipo NOGEWA rasmi kuanza kugawana mali za umma kama njugu! Dhambi hii itaendelea mpaka CCM itoke Madarakani!!! Haiingii akilini Serikali imeweza kutoa Trillions as a stimulus package kwa makampuni yao! Wanashindwa ku-bail out UDA yenye umuhimu wa kipekee kwa wakazi wa Jiji la Biashara Tanzania yenye pilikapilika nyingi za kiuchumi... Haiingii alikilini kwanini walishindwa kui-restructure UDA ili iweze kukopa na kujiendesha kwa kutumia Assets zake! Naamini UDA kwa assets zilizopo inauwezo wa kununua Boat za kisasa, Treni za kisasa na mabasi mengi ya kisasa yenye kutumia both LPG na Diesel Systems kama nchi za wenzetu... Dhambi za dhulma kwa Watanzania zitaendelea kuwatafuna hadi Makaburini mwao hawa Jamaa...siku si nyingi wata gundua kuwa watu wa kawaida hawatajali wanapendeza vipi kwenye V8 na Vogue zao za bei mbaya... wameanza watoto wa mtaani el maarufu PANYA RD wameanza... kama wanaakili watagundua kuwa Social GAP waliyoitengeneza siyo deal na itawagharimu kwa sanaaaaaaa