Simon Group na Ridhiwani Kikwete wana uhusiano gani?

Ridhiwani kikwete wakati Simon group wanafanyiwa feasibility study ya uwezo wao wa kuendesha UDA ndio aliekuwa sole signatory wa cheki za kumlipa mtu aliyefanya hiyo study, kwa asiyejua atamtetea tu lkn ukweli ndio huo kwa uelewa wangu mdogo mwenye kampuni yake ndiye mwenye mamlaka na finances za kampuni yake, acheni kutetea upuuzi ifike muda tujitambue kwa maendeleo ya nchi yetu

Sijui kwa nini watu wazima wanatatanika! Huyu anayeitwa mwana mpendwa ndo mmiliki wa UDA. Hadithi niliyowahi kusikia ni kwamba hata pesa ya kununua UDA ilichotwa kwa amri ya mkuu. Pesa ikachotwa serikalini na UDA ikanunuliwa.
Tatizo ni kuwana Rais ambaye ana madaraka ya kifalme. Kila mtu anataka urafki na Rais, akishindwa mwanae, akishindwa mkewe, akishindwa hawal yake, n.k.
 
Kaka hizo "TECHNICALITIES" ni zipi?Au ndio hizi wahusika wakuu wenyenchi aka walanchi?Vinginevyo sitaelewa kamwe.Sasa imekuwaje tena Naibu mmoja wa Fedha amesema kesi iko mahakamani?Naona kama vile kuna ngoma fulani inachezwa lakini twaisikia kwa mbali.

Fuatilia yaliyojiri bungeni jana,kesi ilishafutwa,na sasa wameipeleka takukuru,na kwa DPP.
 
Kumekuwa na kizungumkuti kikubwa sana kuhusu kampuni ya Saimon Group na hisa za shiriki la UDA , na kizungumkuti hiki kinatokana na ukweli kuwa hisa hizo ziliuzwa kihuni huni , kuna harufu kubwa ya rushwa nk .

Maswali ya kujiuliza ni kama ifuatavyo;

i. Saimon Group ni nani ,

ii. Nguvu za kuligawa hata Bunge anazitoa wapi ,

iii. Nani yuko nyuma yake ,

iv. Ni akina nani ni wana hisa wa Saimon Group,

v. Ni kwanini magari yake yote 300 yalipewa tax exemption ,

Natoa some clue lead kwa ajili ya JF MEMBERS kufanya ufuatiliaji wa kina .....

i. Ni kuwa Saimon Kisena , aligombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi mwaka 2010 na alishindwa na Shibuda kwenye kura za maoni ila jina la Shibuda lilikatwa na kamati kuu, ndipo Shibuda kaenda Chadema .

ii. Wakati wa Kampeni , Ridhiwani Kikwete alifanya kazi kubwa sana ya kampeni kwenye majimbo matatu nchini ambayo yalikuwa ni Maswa Magharibi ( Saimon Kisena ) , Shinyanga Mjini ( Masele ) na Meatu ( Salum Mbuzi ) .

iii. Saimon Kisena , anamiliki Ginnery ya Pamba iliyoko Malampaka , na Ginery hii ilinufaika na fedha za stimulus package ambazo ni fedha za umma , na mpaka leo bado hakuna taarifa rasmi za ni akina nani walinufaika na fedha hizi kiasi cha shilingi trilioni moja na usheee....

iv. Kuna taarifa za uhakika kuwa Ridhiwani Kikwete ,ni share holder wa Saimon kwenye Ginnery hiyo , na hata kwenye umilikaji wa UDA ni sehemu ya Kampuni husika .

Naomba tujadili kwa lengo la kutafuta majibu ya maswali hapo juu.

Nitaendelea baadae ...

Safari_ni_Safari


Mwaka 2010 Simon Kisena akigombea nafasi ya kuwa mgombea ubunge ndani ya CCM alidiriki kumpiga mtama OCD wa huko Maswa na OCD yule ndiye akaadhibiwa kwa kuhamishwa kituo cha kazi



Updates :
UDA ni kitu gani kwa wasiokuwa nataarifa za kina Someni makala hii.....

SAKATA LA UUZAJI WA UDA: Hakuna atakayesalimika




Na Jacob Daffi - Imechapwa 12 October 2011




KAMATI ya baraza la madiwani iliyoundwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Ma------ kuchunguza ubinafsishaji wa shirila la usafiri jijini (UDA), kuvunjwa kwa bodi ya shirika hilo na kuuzwa kwa mali zake, imeagiza kufikishwa kwenye mkono wa sheria aliyekuwa meneja wa shirika hilo, Victor Millanzi.


Katika ripoti ambayo ----------- imeipata, kamati imeagiza meneja huyo achunguzwe na vyombo vya dola kutokana na ushiriki wake katika kulihujumu shirika hilo.


Aidha, ripoti imesema hatua ya Ma------ kukabidhi UDA mikononi mwa muwekezaji – kampuni ya Simon Group Ltd., - ni “kinyume cha utaratibu.”


Dk. Ma------ aliunda kamati hiyo Juni mwaka huu. Ripoti inatuhumu Millanzi kuuza kinyume cha taratibu rasilimali za UDA zinazohamishika na zile zisizohamishika kama sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na hasara.


Hata hivyo, Millanzi katika taarifa yake mbele ya wajumbe wa Kamati amekana madai yote dhidi yake na kusema, “Nilichokiteleza nilikifanya kwa mujibu wa sheria na taratibu za kuendesha UDA.”


Meya hakupata ridhaa (Resolution) ya mkutano wa madiwani. Yumkini mwanahisa wa pili mkubwa, Hazina naye hakuridhia maamuzi ya kikao hicho wala wakurugenzi wa bodi ya UDA.”


Kamati ya Ma------ imeeleza, “uuzaji wa rasilimali za UDA haukufuta sheria za manunuzi ya umma (PPRA) ya mwaka 2004; wala hakukufanyika tathimini ya mali zake kabla ya kuuzwa.”


Hadi kufikia 30 Juni 2010, shirika hilo la umma lilikuwa likiendeshwa kwa hasara ya Sh. 1.4 bilioni.


Kamati hiyo imebaini mali zisizohamishika za shirika hilo zilizouzwa kwa kile inachoita kiholela kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2010, ni pamoja na nyumba iliyoko kiwanja Na. 10 eneo la Jangwani Beach. Nyumba hiyo imeuzwa mwaka 1997 kwa Harold John kwa thamani ya Sh. 40 milioni.


Nyumba nyingine ni ile iliyopo Na. 60 iliyoko katika eneo la Oysterbay, ambayo imeuzwa kwa Sh. 120 milioni (1997) na ile iliyoko kitalu Na. 354, eneo la Masaki, Kinondoni, ambayo imeuzwa mwaka 2001 kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa thamani ya Sh. 600 milioni.


Katika uza uza hiyo, kimo kiwanja kilichoko kitalu Na. 261 eneo la Ubungo kilichouzwa mwaka 1998 kwa Shirila la Maendeleo la Dar es Salaam (DCC) kwa Sh. 800 milioni, viwanja Na. 1-21 vilivyoko block V, katika Manispaa ya Ilala, vilivyouzwa mwaka 2003 kwa DCC kwa Sh. 350 milioni, kiwanja Na. 38 kilichoko Oysterbay kilichouzwa mwaka 2005 kwa kampuni ya Century Properties Ltd kwa Sh. 516.2 milioni na nyumba Na. 54 iliyoko Ilala iliyouzwa 2009 kwa Trans Ocean Supplies Ltd kwa Sh 180 milioni.


Aidha, Kamati hiyo imebaini kuwapo kwa mikataba kadhaa yenye utata ya pango ya majengo na maeneo ya wazi yanayomilikiwa na UDA. Katika maeneo mengi, hata bei hicho kinachoitwa “bei ya pango,” haikuzingatia ukubwa wa eneo. Vitega uchumi vingi vimeuzwa kwa bei ya kutupa.


Kwa mfano, menejimenti ya UDA, chini ya Millanzi na Bodi ya Wakurugenzi iliyokuwa chini ya Idd Simba, ilipangisha watu mbalimbali kuanzia kwenye jengo la utawala yalipo makao makuu ya UDA, Kurasini, Dar es Salaam hadi maeneo ya wazi yaliyoko katika karakana zake.


Wapangaji hao wanaiolipa kodi ya kutupwa, ni pamoja na Nagla General Shipping Services Ltd., aliyepangishwa kwenye jengo la utawala eneo lenye ukubwa mita za mraba 19 kwa Sh. 7,500 kwa mwezi.


Wengine ni F.A.Agencies (T) Ltd., anayelipa Sh 7,200 kwa mwezi, Rafad Complex Ltd (kituo cha basi kati), anayelipa Sh. 8,400 kwa mwezi na Lake Corridor Petroleum Ltd anayeendesha kantini ya UDA kwa malipo ya Sh. 7,429 kwa mwezi. Kampuni ya Lake Corridor Petroleum Ltd imekodishwa eneo lingine la ufundi lenye ukubwa wa mita za mraba 140 ambapo inalipa Sh. 3,000 kwa mwezi.


Nyingine ni kampuni ya Mupingwa Petroleum Ltd iliyokodishiwa ofisi za UDA zilizoko bandarini kwa Sh. 4,800 kwa mwezi, Koru Freght Ltd iliyokodisha ghala la UDA kwa malipo ya Sh 2,457 kwa mwezi, huku kampuni hiyo ikiwa imepangishwa eneo la wazi katika viwanja vya makao makuu ya UDA lenye ukubwa wa mita za mraba 370 kwa Sh. 2,485 kwa mwezi.


Wapangaji wengine na kiasi wanacholipa kwa mwezi kikiwa katika mabano, ni pamoja na Seleman Keraba (Sh. 850 kwa mwezi), Mak Consult Engineering (Sh. 4,312), Macbean Sea Trading (Sh 7,200), Koru Freight Ltd (Sh. 6,000), Koru Freight pia imepanga eneo la mita za mraba 164.52 kwa Sh. 3000, Shibat Enterprises Ltd (Sh. 7,000) na Exaud Epiana aliyepewa karakana kwa kodi ya Sh. 6,000 kwa mwezi.


Kwa mujibu wa ripoti ya kamati hiyo, viwango vya soko kwa sasa vya kukodi katika maeneo ya mijini, na hasa jijini Dar es Salaam, ni kati ya dola 7 hadi 12, sawa na karibu Sh. 10,500 hadi Sh. 18,000 kwa kila mita moja ya mraba kutegemeana na eneo lilipo jengo husika linalopangishwa.


Ripoti hiyo imebainisha wazi kwamba baadhi ya wapangaji hao wa maeneo ya UDA wameyapangisha kwa makampuni mengine ambayo wao wanawatoza bei kubwa zaidi na hivyo makampuni hayo kujinufaisha zaidi kupitia mgogo wa shirika hilo.


Kampuni ya Lake Corridor Petroleum Ltd imetajwa kama mfano wa makampuni ambayo yameingia mikataba ya kukodishwa ofisi au maeneo ya wazi, lakini wakaamua kupangisha kwa watu wengine bila kupata idhini wala kibali cha UDA.


Wakati kampuni ya Koru Freight imepanga eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 1,916, kamati imebaini kwamba kampuni hiyo imekuwa ikilipia eneo la mita za mraba 370 tu.


“UDA iliingia ubia na Africarriers tarehe 13/10/2009kuendeleza kiwanja Na 437/129 kilichopo Mtaa wa Sokoine (kilipo kituo cha mabasi cha Stesheni). Makubaliano hayo yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutokuwapo nyaraka zozote zinazoonyesha jinsi mwekezaji huyu alivyopatikana, hivyo kutia shaka iwapo sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005 zilizingatiwa,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.


Upungufu mwingine uliotajwa na ripoti hiyo katika mkataba wa ubia huo wa UDA na Africarriers, ni kampuni hiyo kutaka kwamba baada ya mradi wa ujenzi wa ghorofa ndani ya kiwanja hicho cha kituo cha Stesheni kukamilika, mwekezaji huyo atatakiwa kumiliki hisa asilimia 75 na UDA ibakiwe na hisa 25 tu.


Aliyekuwa Meneja huyo wa UDA, Millanzi, ambaye alitimuliwa na Ma------ Juni mwaka huu, kabla ya kuivunja pia Bodi ya UDA iliyokuwa chini ya Idd Simba, anadaiwa kujichotea Sh. 40,622,651.80 kama malipo ya kiinua mgongo chake hata kabla ya kumaliza mkataba wake wa kuliongoza shirika hilo.


Kwa mujibu wa ripoti ya kamati hiyo ya Ma------, mkataba wa utumishi wa meneja huyo ulipaswa kufikia ukomo 30 Juni 2011, lakini hata kabla ya kufikia mwisho wa mkataba huo yeye alikwishajilipa tayari kiinua mgogo chake.


Malipo hayo yanaelezwa kulipwa kwa awamu tatu. Tarehe 19 Mei 2011 kupitia vocha Na 21, alijilipa Sh. 25,000,000, tarehe 25 Mei 2011, akajilipa Sh. 5,800,000 na 30 Mei 2011, ambapo amejilipa Sh. 9,822,651.80 kupitia hundi Na. 930322.


Katika utetezi wake wa maandishi mbele ya kamati kuhusu tuhuma za kujilipa mafao kabla ya mkataba kumalizika, Milanzi alisema, “Siyo kweli. Mimi niliajiriwa UDA mwaka 2006, tarehe 1 Juni. Hivyo mkataba wangu uliisha 30 Mei 2011.”


Anasema, “Nilitoa notisi ya mwezi mmoja na taratibu zetu (UDA) malipo yanafanywa kwenye mwezi wa mwisho uliotoa notisi.”


Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinaonyesha Milanzi alisaini mkataba wa ajira tarehe 29 Juni 2006, wenye Kumb. Na UDA/A.1/6. Ulipaswa kumalizika 30 Juni 2011.


Mgogoro kuhusu menejimenti nzima ya UDA uliibuka mapema Juni mwaka huu baada ya Meya Ma------ kuamuru kumfuta kazi Millanzi, pamoja na kuivunja Bodi ya UDA iliyokuwa chini ya Idd Simba kukabiliwa na tuhuma za ufujaji wa fedha zilizokuwa zimewekezwa na mwekezaji mpya ndani ya shirika hilo.

Nilishangaa pale Rais alihudhuria kikako ya DRT, sasa naanza pata mwanga.
 
Your text takes me to a conclusion that all those on power are laughable! Are you mentally fit? Is that a way of disposing public properties. You mean, you also have that chance of stupidly scooping public property behind a non-useful pretext of saying they had 20 buses, they are doing for the nation, etc. A Nation! What connection guarantees someone, an individual, to confiscate shirika like UDA at a throwaway cost, using funds nowhere to be traced of its originality!

And you smile, mouth open. I am not an ectoplasm like you!
Chafu kabisa weeee!


Hapa hatutukanani mkuu! Lete hija ujibiwe, The way I think to me ni kuwawajibisha waliouza kiholela hili shirika ikiwa pamoja na walioshindwa kuliendesha kwa faida hadi kufikia kuliuza kwa Simon Group. Then lay sanctions to the current owner of the company to scare others who crave for loopholes.

I bet you dont understand the real deal and the process upon selling it, just like TRL, ATCL and the like of which none of the leaders was held responsible. Do not go for the shiny leaves, go for the roots.

I hope hutanitukana tena and remember non of us want to see all these happening but what is the way out? Treating the investor as a traitor or shaping your leaders who abuse their power so frequently? In my mind the Simon Group should have been exposed by your leaders with their abusive prior offers to the deal, but they opted to keep under the carpet to conceal some penny.
Take the leaders down to their feet...
 
Hapa hatutukanani mkuu! Lete hija ujibiwe, The way I think to me ni kuwawajibisha waliouza kiholela hili shirika ikiwa pamoja na walioshindwa kuliendesha kwa faida hadi kufikia kuliuza kwa Simon Group. Then lay sanctions to the current owner of the company to scare others who crave for loopholes.

I bet you dont understand the real deal and the process upon selling it, just like TRL, ATCL and the like of which none of the leaders was held responsible. Do not go for the shiny leaves, go for the roots.

I hope hutanitukana tena and remember non of us want to see all these happening but what is the way out? Treating the investor as a traitor or shaping your leaders who abuse their power so frequently? In my mind the Simon Group should have been exposed by your leaders with their abusive prior offers to the deal, but they opted to keep under the carpet to conceal some penny.
Take the leaders down to their feet...

Your previous msg took me out of sense. Ulionyesha wazi kwamba Mnunuzi huyu amesaidia kuinua shirika. Appreciation za aina hiyo zilimfaa kama angeazimwa na serikali kama CEO wa shirika. Yeye alinunua kiwizi halafu unamsifu wakati tunajadili uhalifu wake na wote alioshirikiana nao!

Now let me come back to ground state. Ni kwamba Ktk nchi hii sasa hivi upuuzi umezidi kipimo. Ukisoma JF utagundua kwamba kuna makundi yanayoshabikia watu kwa sababu za kipuuzi. Wengine ni kwa sababu ni kabila lao, wengine ni kwa sababu anatoka bara au visiwani kama wao, wengine kwa sababu ni CDM au CCM kama wao, n.k. Mambo ya aina hii ni uchafu kabisa! Kwani kabila lako akiiba akajinufaisha, wewe binafsi inakufariji nini?

Huko CCM kuna mijitu haijui hata chama kina shilingi ngapi, lakini subiri CCM ikisemwa kwa mabaya yao, Weee! Matusi yanaporomoshwa! CDM nao hivyo hivyo. Sasa umekuja ushabiki wa kila mtu. Akisemwa Rizi1 taabu akisemwa Simon's group taabu. Tunawezaje kuwa nchi ya kushabikiana hata kwa mtembea uchi?

Huyo Simon kuna tatizo tena kubwa. Bahati mbaya ni kuwa na nchi inayoongozwa kwa cartels. Uongozi wa nchi sasa ni kama magenge ya wauza madawa. Wanafahamu upuuzi unaoendelea lakini kila mtu ananyamaza na hakuna anayemgusa mwenzake bali wanasaidiana. Hayo mambo ya TRL na ATC yasiwe ni utetezi. Wapuuzi tuwaweke kundi moja. Basi!
 
Nina mashaka.hivi katika opportunity zite za kibiashara zilizopo TZ mtu ukahangaike na kelele za daladala?
Kama wana mitaji kuna area za kuinvest kwa faida kubwa.
Biashara hizi kichaa sidhani mtu mwenye pesa zake atakubali kuingia.
Kama yumo basi ana matatixo as hata greenwaste tunaambiwa yake.
Kweli mkuu usemacho ila nchi hii ni zaidi ya tuijuavyo, inawezekana kwa juu juu tukaona kelele za daladala lakini nyuma ya pazia kuna vitu vingine kama kuchukua bonge la mkopo kwa mgongo wa UDA alafu unakwenda kufanya shughuli zingine. Kama watu wanapewa kiwanda kwa milioni 70 tena kwa mkopo alafu baada ya mwezi mmoja kinaanza uzalishaji na serikali hiyo hiyo iliyouza inaanza kuchajiwa huduma kwa mwezi 200 million kwanini hili nalo lisiwe hivyo. Siku hizi viongozi ngazi za juu wanapiga, madiwani wanapiga na wenyeviti wa mitaa nao wanapiga yaani kupata tenda katika serikali kuanzia serikali za mitaa mpaka serikali kuu ni issue. Haiingii akilini kukusanya ushuru soko, sijui maegesho n.k lazima kuna harufu ya kiongozi siku katika hii miradi wakati hizo biashara wameanza wakati wapo madarakani na kwa maana nyingine vigezo vya kupewa tenda ni vidogo
 
Kweli mkuu usemacho ila nchi hii ni zaidi ya tuijuavyo, inawezekana kwa juu juu tukaona kelele za daladala lakini nyuma ya pazia kuna vitu vingine kama kuchukua bonge la mkopo kwa mgongo wa UDA alafu unakwenda kufanya shughuli zingine. Kama watu wanapewa kiwanda kwa milioni 70 tena kwa mkopo alafu baada ya mwezi mmoja kinaanza uzalishaji na serikali hiyo hiyo iliyouza inaanza kuchajiwa huduma kwa mwezi 200 million kwanini hili nalo lisiwe hivyo. Siku hizi viongozi ngazi za juu wanapiga, madiwani wanapiga na wenyeviti wa mitaa nao wanapiga yaani kupata tenda katika serikali kuanzia serikali za mitaa mpaka serikali kuu ni issue. Haiingii akilini kukusanya ushuru soko, sijui maegesho n.k lazima kuna harufu ya kiongozi siku katika hii miradi wakati hizo biashara wameanza wakati wapo madarakani na kwa maana nyingine vigezo vya kupewa tenda ni vidogo

Safi kabisa!
Watu wanadhani UDA ni mabasi. UDA ni zaidi ya mabasi! Kuna majengo tena kwenye prime areas za masaki. Tunakumbuka Ubungo Terminal pia ilikuwa ni mali ya UDA. Kurasini ndo pia kulikuwa na terminal kubwa! Hizo ni assets za kukufanya benki ikuite kwa hamu.
 
Kamati yamkaba kigogo wa Uda


Na Daniel Mjema na Fidelis Butahe, Mwananchi


KWA UFUPI


Katika mkutano huo, ndipo Kisena anadaiwa kutoa matamshi ya kuwatuhumu baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam kuwa wamehongwa na mfanyabiashara huyo ili kulishikia kidedea suala hilo.
Dodoma. Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), Robert Kisena amewekwa kiti moto kwa saa kadhaa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.


Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge, zilisema Kisena pekee ndiye aliyehojiwa kuhusiana na matamshi anayodaiwa kuyatoa yaliyoingilia mhimili huo wa dola.


Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel jana alilithibitishia gazeti hili kuhojiwa kwa Kisena, lakini akasema hafahamu alihojiwa nini na mahojiano yatachukua siku ngapi.


Joel alisema kuwa, Kisena alikutana na kamati hiyo jana na kuongeza: “Wamemuita kwa ajili ya kumhoji, ila sijui watamhoji kwa siku ngapi. Anayehojiwa ni Kisena na siyo vigogo wa Uda.”


Mei 19 mwaka huu, Kisena alinukuliwa akisema kuwa wabunge wa Dar es Salaam wamehongwa na mfanyabiashara mmoja na kwamba kampuni yake inamiliki asilimia 70 ya hisa za kampuni hiyo.


Kauli ya Kisena ilikuwa kama kujibu taarifa ya Serikali iliyotolewa bungeni na Naibu Waziri wa Fedha, Adamu Malima aliyedai Serikali inamiliki asilimia 49 ya hisa na Jiji la Dar es Salaam asilimia 51.


Katika mkutano huo, ndipo Kisena anadaiwa kutoa matamshi ya kuwatuhumu baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam kuwa wamehongwa na mfanyabiashara huyo ili kulishikia kidedea suala hilo.


Hoja ya kutaka Kisena ahojiwe na Bunge, ilitolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akitaka tuhuma za Kisena dhidi ya wabunge zijadiliwe kwa kuwa ameingilia uhuru na kinga za Bunge.


Mnyika alisema kitendo kilichofanywa na Kisena kwa kuzungumzia nje ya Bunge masuala ambayo yametolewa maelezo na Serikali ni kuingilia uhuru na kinga za mhimili huo.


Mbunge huyo alisema kuwa mgawanyo halali wa hisa za Uda upo kama ulivyosajiliwa kwa msajili wa mashirika ya umma, kwamba Uda linamilikiwa na Serikali na Halmashauri ya Jiji.


Katika kujenga hoja yake, Mnyika alisema majibu hayo yalionyesha kuwa Uda ni Shirika la Umma, jambo ambalo lilipingwa na Kisena kupitia mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya hivi karibuni.
 
Joel alisema kuwa, Kisena alikutana na kamati hiyo jana na kuongeza: "Wamemuita kwa ajili ya kumhoji, ila sijui watamhoji kwa siku ngapi. Anayehojiwa ni Kisena na siyo vigogo wa Uda."

nukuu hii ina siri nzito, kuwa aahojiwa Kisena na sio vigogo wa UDA , hao vigogo wako wapi .?
 
Joel alisema kuwa, Kisena alikutana na kamati hiyo jana na kuongeza: “Wamemuita kwa ajili ya kumhoji, ila sijui watamhoji kwa siku ngapi. Anayehojiwa ni Kisena na siyo vigogo wa Uda.”

nukuu hii ina siri nzito, kuwa aahojiwa Kisena na sio vigogo wa UDA , hao vigogo wako wapi .?
wanajichanganya tu,mara kisena amewashutumu wabunge wa dar kwa kuhongwa na mfanyabiashara huyo,mfanyabiashara yupi?.
 
UDA ,serikali inasema inamilikiwa, ila magari yote namba zake ni private sio za SU kama ilivyokuwa likiwa shirika la umma , nani aaminiwe?
 
Kwanza nataka niseme kuhusu huyo anajiita simoni group,ni kaka mmoja msukuma Tapeli sana,alishamtapeli hadi mshahara wa baba yangu jamani,ni Tapeli mwanzo mwisho,
 
huyu jamaa ni tapeli wa kuaminika,juz Kati hapa alikuwa na.kesi ya kuitapeli kiwanfa cha mafuta kule Kahama.
aliwatapeli atawauzia mbegu sijui mashudu za pamba alafu mwisho wa siku mzigo was not delivered.
prince anawatumia watu Kama hawa kumi loot hili taifa,yaani nchi hii umekuwa chukua chako mapema,no body cares,ukipata gap unapiga ,eeehh mungu baba turehemu na hawa magisadi wenye roho mbaya,watoto wetu sijui watakuja wakute tusha binafsishwa!!!
 
Uzuri wa mwanadamu ni kifo. Ukiishakufa ndiyo mwisho wa ufisadi wako. Upuuzi uliohamasishwa na tamaa matunda yake ni funza watakaokutafunaaaa
 
Back
Top Bottom