VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Jana kulikuwa na sinema ya bure humu JF. Mkuu Simiyu Yetu aliweka bandiko lake kwenye Jukwaa la Siasa akidai kuwa yuko Arusha na ametafiti jambo. Ametafiti na kujua kuwa Lowassa hakubaliki Arusha, alipodai yupo. Baada ya hapo akaibuka Mkuu MUSSA ALLAN,kada wa zamani wa CCM.
Lengo la Mkuu MUSSA ALLAN lilikuwa ni kuonana na Mkuu Simiyu Yetu ambaye alidai kuwa yuko Arusha. Pakawa hapatoshi. Mwanzo, mkuu Simiyu Yetu alidai kuwa yuko 'MAKATO BAR'. Akatafutwa na kuelekezwa pa kukutana bila ya mafanikio. Baadaye Simiyu Yetu akaibuka na kudai yuko ndani ya Bar hiyo.
Mwisho, ikadhihirika kuwa Mkuu Simiyu Yetu hakuwa Arusha kama alivyodai. Lakini, inajidhihirisha kuwa wakuu hawa wanajuana. Ikajulikana pia kuwa Mkuu MUSSA ALLAN ana usafiri mzuri-landcruiser. Hakika, Mkuu Simiyu Yetu, anayejifunza propaganda za Nape Nnauye, hatamsahau Mkuu MUSSA ALLAN.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam