Simiyu: Ashikiliwa baada ya mafundi kukuta mabaki ya mwili kwenye eneo la nyumba aliyoiuza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
photo_2023-09-07_09-31-31.jpg
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linamshikilia mtu mmoja anayetambulika kwa jina la Juma Peter kufuatia eneo yalipokuwa makazi yake kukutwa mabaki ya mifupa yaliyodhaniwa kuwa ya binadamu.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea Mkoani Simiyu, ambapo Jeshi la Polisi katika taarifa yake ya awali linadai kuwa linafanya uchunguzi wa mabaki hayo yaliyokutwa na mafundi ujenzi waliokuwa wanachimba msingi wa nyumba katika Mtaa wa Nyamimbi Kata ya Somanda Wilaya ya Bariadi.

Ambapo taarifa ya Jeshi hilo imeeleza tukio hilo lilitokea Septemba 4, 2023 majira ya asubuhi katika kiwanja kinachomilikiwa na mtu aitwaye Imelda Kilima ambaye alinunua eneo hilo kwa Juma Peter.

Taarifa inadai mabaki ya mifupa hiyo yamechukuliwa na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi.

====================

Taarifa zisizo rasmi kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ni kuwa mtuhumiwa huyo alikiri kuwa alimuua mke wake na kufukia kwenye shimo alilochimba ndani ya makazi yake bila jamii kufahamu, ambapo baada ya tukio hilo inadaiwa ndipo aliamua kuuza eneo hilo.

Hata hivyo imeelezwa mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa na kukiri kutenda tukio hilo alipewa jukumu la kuchimbua alipouzika mwili huo na kutoa mabaki yaliyokuwa yamesalia.

===============


 
Back
Top Bottom