Similarities between CCM vs Zanu-PF and Magufuli vs Mugabe

Leo mtamfananisha na Mugabe,Kesho mtasema ni rafiki wa Kagame mtamfananisha naye tena,keshokutwa mtasema ni kama Museveni,wiki ijayo mtakuja na kusema yupo kama Raila Odinga kwa kuwa ni rafiki yake...

Mnabaki kufanya comparison tuu,hamtafuti the source ya kusolve the problem,tuacheni yao tufocus yetu. juzi mlijitoa ufahamu mkaangukia upande wa Kenyatta mkaampambaaa weeee leo kafanya nini??mulemule tuu kama wengine,msiridhishwe na wengine wamefanya nini wanasababu zao za kufanya hivyoo na nyie fanyeni kwa nafasi yenu kulingana na sababu zenu/situations zenu.
Mbona povu linakutoka? Nyie si ndio mnamfananisha na wote hao au,?
 
Mugabe Hana Ukomo wa madaraka
Mbowe Hana Ukomo wa madaraka

Nguvu ya Grace ndani ya ZANU PF Ni sawa na Nguvu ya Madam Wema Sepetu ndani ya Chadema baada ya kumpiku Madam Joyce Mukya!
Duh, afadhali huku kuna gender!! Kwahiyo kwenu mama Jesxa ni takataka kabisa!!
 
Hii ndio comment ya kidemokrasia sio kuzuia Watu Eti nataka kuharibu Uzi, kwani tupo hapa kupamba Mawazo ya alieleta mada?
Uachage Ushamba kila usichokikubali kukiita Propaganda au Mtu akiwaza tofauti Eti anataka kuharibu Uzi !
Kama kwenu mtu akimpinga mkulu mnamuita bebari au fisadi. Akiongea ukweli mnamuita mchochezi, msiogope tulieni tu. Muda sio mrefu mishahara teeh!!!
 
TUCTA inatumika na CCM kutumia pesa za wafanyakazi

Ujamaa umefeli, Mashirika ya umma kujenga viwanda ni wizi mtupu

NSSF NA PPF kujenga viwanda ni kuchezea pesa

Katika Bunge linaloendelea, Naibu Spika amethibisha kuwa Sheria iliyotungwa na Bunge inakataza FAO la Kujitoa

--TAMKO ZITO Fao la Kujitoa----Soma zaidi ....Tamko zito fao la kujitoa

TUCTA wanayo hii habari?

Wafanyakazi mnayo hii habari?

Watanzania tuendelee kulala

Wacha Pesa zijenge viwanda, baada ya miaka 10 vife

Hivi Watanzania wenzangu...Sababu zipi ziliua viwanda?

Je...Bidhaa za Tanzania zina ubora wa kutosha?

Mfano..Kuna Siagi (butter) Tanzania?
 
Kilichomuondoa Mugabe Madarakani ama Kinachowaondoa Marais wengi Madarakani Ambao ni Wakatili au kwa Lugha nyepesi Madikteta ni Kitu kinaitwa Deep State.... Madikteta wote ulimwenguni wanakuwa na kikundi hiki amabcho ni kikundi kitiifu kwenye Tawala za Kidikteta. Kikundi hicho Huishi kwakutii Mtu ila ni kikundi hatari sana maana ndicho huja kudondosha Tawala hizo.

Tawala nyingi katili ambazo zimedondoshwa zitazame utakuta zimedondoshwa na Kikundi kitiifu amabacho wakati wote kilitumika kulinda masilahi ya Mtawala kwa level ya juu sana.Kilicho Mtokea Mugabe siyo kitu kigeni kwenye ulimwengu wa Deep State...
 
Robert Gabriel Mugabe (1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe.

Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.

Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kulipiza kisasi kwa kuwaua na kuwatesa watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mji wao mkubwa ni Bulawayo, mwanzo ilijulikana walikuwa wanauawa na watu wasiojulikana lakini baadaye yakawa mauaji ya halaiki ya wazi.

Tume ya kanisa katoliki kuhusu haki na amani ilitoa ripoti iliyodai kwamba zaidi ya watu 20,000 waliokuwa wanamuunga mkono Joshua Nkomo na wapinzani walipoteza maisha yao.

1983 Nkomo alikimbilia uhamishoni London baada ya wafuasi wake kumtuhumu kukiunganisha chama chake cha ZAPU na ZANU cha Mugabe na kuunda ZANU-PF, kama TANU na ASP zilivyoungana kuunda CCM.

Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu akitumia vyombo vya dola hasa jeshi la polisi ikiwezekana kufuta matokeo akiona anaelekea kushindwa.

Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1998 yalisababisha kuanzishwa kwa chama kipya cha Movement for Democratic Change (MDC) chini ya kiongozi wake Morgan Tsvangirai na mwaka 2000 kilishiriki uchaguzi wa rais. Baada ya uchaguzi Tsvangirai alikamatwa kwa kosa la uhaini akituhumiwa kutaka kumuua Mugabe baadae 2004 aliachiwa kwa kukosekana ushahidi kama viongozi mbalimbali wa upinzani hapa wanavyokamatwa kwa uchochezi baadaye kuachiwa kwa kukosa ushahidi.

Baada ya uchaguzi huo wa 2000 uvunjaji wa haki za binadamu uliongezeka maradufu, mateso na manyanyaso dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali yamekuwa yakiripotiwa. Ni katika kipindi hicho Mugabe alianzisha mabadiliko ya sera ya Ardhi ambapo wazungu na wapinzani walinyang'anywa ardhi bila fidia kama inavyotokea leo Tanzania. Ilifikia hatua hadi ya nchi za Magharibi zikaiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi.

Mabadiliko hayo ya kiuchumi yaliyofanywa na Mugabe yaliishangaza dunia na kusababisha uchumi wa nchi hiyo kushuka hadi leo, hakusikia wala kujali ushauri wa kiuchumi alikuwa akipewa.

Watu walidhulumiwa mali zao, haki za binadamu zilikiukwa kwa kisingizio cha maendeleo, makampuni mengi hasa ya wazungu yalifunga biashara zao hali ambayo leo inaonekana hata Tanzania kwa makampuni kufunga biashara zao.

Katika kipindi hicho vifo vingi viliripotiwa na wapinzani kukamatwa mara kwa mara, mfano.

May 2003 ijumaa jioni Tsvangirai alikamatwa mara baada ya kufanya press conference, akituhumiwa kufanya uchochezi kwa serikali.

Tarehe 11 March 2007 Tsvangirai alikamatwa tena akielekea kanisani, iliripotiwa kuwa alipigwa sana na kuteswa na kikosi maalumu cha polisi. Aliumizwa kichwani machoni na hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kumuona zaidi ya mke wake. Mpiga picha wa Zimbabwe Edward Chikombo aliyefanikiwa kupata picha zake na kuzionyesha hadharani muda mfupi aliripotiwa kuvamiwa akiwa nyumbani kwake na kuuawa.
View attachment 632143

Kwenye uchaguzi wa 2008 Iliripotiwa na vyombo mbalimbali kuwa Morgan Tsvangirai kutoka chama cha MDC-T alishinda kwa 47.8% huku Mugabe akipata 43.2% uchaguzi uliofutwa na kusababisha vurugu kubwa ambapo wafuasi zaidi ya 200 waliuawa.

Katika utawala wake matukio mbalimbali ya kukamatwa wapinzani na wakosoaji wa Mugabe yameripotiwa, watu walioonekana kusaidia upinzani walifunguliwa kesi na wengine ama kupotea au kufungwa jela.

March 2009 Tsvangirai alinisurika kifo baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na gari jingine ambapo mke wake, Susan Tsvangirai, aliuawa kwa ajali iliyojulikana kama ya kupangwa.

Hadi tunakwenda hewani (leo) chama chake cha Zanu-PF kimemuomba Mugabe kuondoka mwenyewe (kujiuzulu) au chama kimuondoe kwa nguvu.
Askofu Shao wa Katoliki kule Zanzibar hakukosea. ninaamini Shao alitumia falsafa kumfikishia ujumbe Askofu mwenzie Pengo lakini naona ikawa hola!!
 
Hili andiko ni kama limeandikwa kuzungumzia Tanzania, matukio mengi yanafanana, pia natabili endapo mambo yanaendelea hivi basi umaskini wetu utaongezeka na tutakua na hali ngumu zaidi ya Zimbabwe.
Inawezekana nisiwepo duniani wakati huo lakini naamini watakaoweza kuishi mpaka muda huo watakuja kusoma hili andiko hapa JF.
 
Madikteta wote wana Motif zinazofanana

Mussolini alimuua Geacamo matieote
Hitler alimuia Ezerberg

Na kuna uchwara mmoja huko puetorico amempiga risasi mpinzani wake
 
Hili andiko ni kama limeandikwa kuzungumzia Tanzania, matukio mengi yanafanana, pia natabili endapo mambo yanaendelea hivi basi umaskini wetu utaongezeka na tutakua na hali ngumu zaidi ya Zimbabwe.
Inawezekana nisiwepo duniani wakati huo lakini naamini watakaoweza kuishi mpaka muda huo watakuja kusoma hili andiko hapa JF.
Ndiyo maana yake kuna mlinganyo mkubwa sana kati ya utawala huu na wa Mugabe.
 
Mugabe Hana Ukomo wa madaraka
Mbowe Hana Ukomo wa madaraka

Nguvu ya Grace ndani ya ZANU PF Ni sawa na Nguvu ya Madam Wema Sepetu ndani ya Chadema baada ya kumpiku Madam Joyce Mukya!
nguvu ya punani haijawahi muacha mtu salama, in his voice "can you come to KIA"
 
Mtaumwa kichwa bure kulinganisha kisicholinganishika. ZANU PF ni mtoto wa CCM, wa TANU. Ndiyo iliwaunganisha, kuwaongoza, wakajikomboa. Mugabe katawala miaka 27, Magu ndiyo kwanza anaingia mwezi wa 27.
 
Kwa wenye uelewa na uwezo wa kuona mbali, Tanzania hatupo salama iwe kwa uchumi, demokrasia au kitaasisi. Kuhodhi mamlaka ni dalili kubwa ya kwanza ya udikteta. Wanaofurahia leo, kuna siku wao na watoto wao watalia vibaya. Tuombe Mungu atunusuru, na walioshikwa na upofu wapate kuona.

Hata ujifanye kuwa karibu kiasi gani na jambazi, hupo salama. Kuna hatua jambazi huamua hata kumwua jambazi mwenzake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom