Simbachawene: Magereza ya Tanzania yanaendeshwa kikoloni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema Magereza ya Tanzania yana viashiria vya ukoloni na kwamba kuna safari ndefu ya kuyabadilisha ili wahalifu watendewe haki za binadamu.

Kauli ya Waziri Simbachawene imekuja wakati kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu na wanasiasa wakidai kuwepo kwa vitendo vya ukatili ndani ya magereza.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam, alipokuwa mgeni rasmi katika shughuli ya kuchangisha fedha za asasi ya kiraia ya Utu Kwanza (Consciousness for Humanity), akisema binadamu wanastahili heshima hata wanapokuwa magerezani.

“Magereza na masuala ya jinai, bado yana vi-elements (viashiria) vya kikoloni. Mfumo wake, na ukikuta gereza ambalo lina kiongozi anayesimama kwenye misingi ya kikoloni ya kizamani anapata nafasi kubwa na huyu ndiye anayeonekana anafanya kazi vizuri,” amesema Simbachawene.

Huku akifafanua umuhimu wa haki za binadamu kwa watu wote, Simbachawene amesema mtu kuwepo gerezani ni utaratibu wa sheria, hivyo sheria hizo zinapaswa ziendane na hali na hadhi ya maendeleo ya binadamu.

“Nikiri na nikubali, kwamba bado tuna safari ndefu ya kufanya katika kuleta mabadiliko ya kushughulika na uhalifu na wahalifu, lakini na sambamba na kuheshimu haki na utu wa binadamu.”

Ameendelea; “Wale maofisa wa magereza na askari wanaokiuka taratibu ni wale ambao dhamira na moyoni mwao wanasutwa, kwamba hawa ni binadamu wanapaswa kutendewa haki na utakuta sheria haziwaruhusu.”

Kutokana na hali hiyo kuna haja ya kufanya mabadiliko, huku akitaka wadau kusaidia mabadiliko hayo.

“Kwa hiyo ipo haja kama Waziri ninayesimamia wzara inayosimamia magereza pamoja na sekta nyingine. Ipo haja ya kushirikiana na wadau kupitia forums (majukwaa) mbalimbali, likiwemo hili ambalo nimepata bahati na sikujua ina nini ndani yake,” amesema.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imempa maelekezo mahsusi ya mabadiliko hayo.

“Masuala ya jinai yana misingi yake na mtu hawezi akapewa adhabu mpaka awe amethibitika pasina shaka kwamba, ametenda kosa hilo. Kwa hiyo ni masuala mtambuka, ipo idara ya Mahakama, wapo wanaoendesha mashitaka, wapo wanaopeleleza kwa ujumla wake hao kuna kazi ya kufanya,” amesema Simbachawene.

Mwananchi
 
Dar es Salaam.

nadhani hata kwa wakati huu mali za Mbowe zote zinapaswa zizuiliwe pomja na acount zake.
lazima sheria ya Ugaidi ifuatwe kikamilifu.

Nilishangaa sana alipo fikishwa nakaona Mbowe anaruhusiwa kukumbatiana na jamaa zake!!
mahakamani lazima gaidi alindwe, nilishangaa pale kisutu inakuwaje Gaidi anapewa nafasi ya kukubatiana na watu mahakamani?!! hili halipaswi kujitokeza. ni muhimu vyombo vyetu vyote vikajifunza kutoka mataifa mengine namna ya kudili na watuhumiwa wa Ugaidi.
kamwe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visikubali kuhadaiwa au kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na mawakili au viongozi wa chadema, lazima sheria ifuatwe kikamilifu kama ilivyo kuwa inafuatwa kwa washitakiwa wengine.
nilishangaa kuwaona watuhumiwa wenzake wa Ugaidi wamefungwa pingu huku Mbowe akiwa hajafungwa pingu, sijafahamu kwa nn,!! kama hakuna ulazima basi wote wasifungwe pingu, sio baadhi wanafungwa wengine hawafungwi!!!
 
Unaandika kama vile umekalia dushe la nchi 12
 
wakiwa wanatoa maelekezo hasa kwa polish kuwa 'fulani ashughulikiwe ipasavyo ili iwe fumdisho kwa wengine " sidhani kama hata anakumbuka maneno - haki za binadamu.
Aya ya 3 toka mwisho inadhihirisha maoni yangu.
 
mimi mpaka leo sijaelewa kusudi la MwenyeziMungu kutuleta hapa duniani ni kuteseka au kufurahia maisha ?

maana ukihesabu kwa muda ambao mtu unaishi hapa duniani muda mwingi ni wa mateso,stress nk. kuliko muda wa ku_relax
Nahisi Mungu alikosa pahali pa kutupeleka maana sio kwa mateso haya

Ukiondoa raha za papuchi na vijistarehe viwili vitatu kwingine kote ni mateso kama sio mateseko
 
Ningekua na mamlaka ningeweka kamera magerezani na wapelelezi.ukifungwa umefungwa kweli kuliko hii kuambiwa walio wengi wamebambikwa
 
nadhani hata kwa wakati huu mali za Mbowe zote zinapaswa zizuiliwe pomja na acount zake.
lazima sheria ya Ugaidi ifuatwe kikamilifu.

Nilishangaa sana alipo fikishwa nakaona Mbowe anaruhusiwa kukumbatiana na jamaa zake!!
mahakamani lazima gaidi alindwe, nilishangaa pale kisutu inakuwaje Gaidi anapewa nafasi ya kukubatiana na watu mahakamani?!! hili halipaswi kujitokeza. ni muhimu vyombo vyetu vyote vikajifunza kutoka mataifa mengine namna ya kudili na watuhumiwa wa Ugaidi.
kamwe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visikubali kuhadaiwa au kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na mawakili au viongozi wa chadema, lazima sheria ifuatwe kikamilifu kama ilivyo kuwa inafuatwa kwa washitakiwa wengine.
nilishangaa kuwaona watuhumiwa wenzake wa Ugaidi wamefungwa pingu huku Mbowe akiwa hajafungwa pingu, sijafahamu kwa nn,!! kama hakuna ulazima basi wote wasifungwe pingu, sio baadhi wanafungwa wengine hawafungwi!!!
Umechanjwa Mkuu?
 
Back
Top Bottom