Habari za leo wana jamvi,
Tarehe 7.7.2023 Gazeti la Mwananchi lilichapisha nukuu ya hotuba ya Mhe. Waziri Simbachawene ambaye ni Waziri wa Mashauri ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora hapa Nchini.
Katika habari hiyo, Mhe Waziri amewatuhumu Maafisa Utumishi kwamba wanagawa vyeo kwa michongo ya rushwa kuanzia milioni 5 hadi 10 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika hotuba hiyo Mhe. Simbachawene alikemea na kuonya Maafisa Utumishi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Binafsi nimeshangazwa na taarifa hii, na kwa pekee nilijiuliza kwamba Mhe. Simbachawene amesahau nini?
1. Mamlaka za uteuzi katika Halmashauri nchini si Afisa Utumishi. Mkurugenzi wa Halmashauri ndiye Katibu wa mamlaka ya ajira.
2. Baraza la Madiwani ndilo linalopendekeza na kuthibitisha uteuzi wa mkuu wa idara.
3. Vibali vya kukaimu vinatoka kwenye ofisi ya Simbachawene.
4. Vetting hufanya na taasisi yetu ya usalama.
Sasa kwa muktadha huu ni wapi Afisa utumishi atachukua mchongo wa milioni 5 au 10? Lakini tuseme ukweli, kati ya Halmashauri na Pale kwa Mhe Simbachawene, wapi ndiko kwenye Michongo?
1. Vipo vyeo vya uteuzi vyenye miongozo yake, mfano nafasi ya DAS anayeteuliwa kwa mujibu wa PMG ni Afisa utumishi au afisa tawala aliye mwandamizi. Je mhe. Simbachawene hawa ma DAS ambao umewatoa UVCCM, walio kuwa wafanyabiashara nje ya utumishi, hawa walio makada walimu hao ni Maafisa utumishi/tawala waandamizi? Huo siyo mchongo?
2. Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo mtu mwenye Sifa za kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Halmashauri anapaswa kuwa Afisa Mwandamizi tena mkuu wa Idara kwa miaka isiyopungua 8 katika utumishi wa Serikali za Mitaa. Je, hawa ma DED uliowachukua mtaani na kuwapatia halmashauri zetu ndiyo mchongo unaouzungumzia? Ama kweli umeongea kwa mafumbo.
3. Katibu Tawala wa Mkoa anapaswa kuwa Afisa mwandamizi Serikalini, anaweza kuwa DED, DAS, ambaye ametumika kwa miaka zaidi ya 14 katika uandamizi serikalini. Hawa baadhi uliochukua hapa na pale ndiyo tuaminini kwamba ni Michongo uliyosema?
4. Utumishi wa umma una miongozo lukuki, upo mpango wa kurithishana madaraka ambao ofisi yako imeutupa chini, ipo PMG ya Sekretarieti za Mikoa ambayo pia umeikanyaga, mathalan zipo Kanuni za uendeshaji wa Serikali za Mitaa zinazoonesha nafasi za uteuzi na taratibu zake ambazo pia umezikanyaga. Hapa ndipo kwenye michongo.
5. Si ofisi yako inayoshusha watu moja kwa moja na kuwaacha watumishi waliokuwa wanakaimu nafasi za uongozi katika Mikoa na Halmashauri. Ofisi yako inatoa vibali vya kukaimu madaraka halafu wakati wa uteuzi mtu huyo uliyempa kibari unamwacha unaleta mtu wa kuokota hapa na pale, tuamini ndiyo michongo yenyewe?
6. Utumishi wa umma hauna ladha, watu wanajiendeea bila kuwa na matumaini ya kuwa viongozi, ndiyo maana CAG hataacha kubaini madudu..eat and run, the future is not guaranteed.
Kwa ujumla hebu turejee nyaraka za akina Rugumyamheto tuujenge upya utumishi wa umma. Kwa sasa ni kumbakumba ilimradi watu waende.
Mhe. Simbachawene, achana na Maafisa utumishi na utawala wa Halmashauri.
Michongo ipo ofisini kwako baada ya wewe mwenyewe kukubali kukanyaga Nyaraka, Kanuni, Taratibu na Miongozo ambayo ofisi yako ndiyo inayosimamia.
Wasalaam.