Simbachawene: Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino umekamilika kwa 100%

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,366
8,098
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Unma na Utawala Bora, George Simbachawene ametoa hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwaajili ya Ofisi ya Rais kwa mwaka 2023/2024 Bungeni Dodoma leo ambapo amesema ujenzi wa Ikulu ya Chamwino umekamilika kwa asilimia 100.

Simbachawene amesema pia taratibu za awali za kuanza ujenzi wa ukumbi wa mikutano na baadhi ya majengo ya ofisi katika Ikulu ya Chamwino zinaendelea.

Aidha amesema katika hatua nyingine ukarabati wa majengo katika Ikulu Ndogo ya Tunguu-Zanzibar na ”Rest House” iliyoko eneo la Mbweni, Zanzibar unaendelea na ujenzi wa majengo ya Mapokezi, Polisi, Geti Kuu na jengo la mitambo ya umeme umekamilika.

Ujenzi wa ukuta na baadhi ya majengo katika Ikulu Ndogo ya Arusha pia unaendelea.
 
Aaah sio kweli bana!!! Huu ni uongo bana!!!
Yani kuweka weka vile vimawe vyeupe kwenye bustani ndio asilimia miamoja....aaah huo ni uongo bana!!! Asitufanye sie hatuna macho bana!!!
 
Back
Top Bottom