Simba vs Yanga: Oct 03, 2012

huku mtaani kwetu yanga wana shangilia kweli naingia JF namkuta kaka yangu @Balatanda anajitapa kweli naanza kuwaona yanga wapuuzi kweli yani 1 - 1 mnashangilia..

Huku mtaani kwetu Simba wenyewe wanakiri walikuwa wanaomba mpira uishe mana'ke kwa jinsi hali ilivyokuwa pamoja na Yanga kuwa pungufu lkn muda wowote watu walikuwa wanarudi kati
 
 
 
5 + 1 - 1 = 5 Yanga bado hizo bao hamjaweza lipa naona kabisa mnaleta msemo wa Kiswahili MBAAZI UKIKOSA MAUA UNASINGIZIA JUA
 
Hongereni watani zangu Simba.....So far mmecheza vizuri na mnastahili ushindi.......

Nina wasiwasi Nyoso anaweza kuwagahrimu pale nyuma...

Amri Kiemba kafunga goli zuri sana.....

Pamoja sana wana Yanga wenzangu


Juma Nyoso si mchezaji yule. Yule kama atumii ndumba ili apangwe sijuwii, jamaa hana mpira wala nini.
 
5 + 1 - 1 = 5 Yanga bado hizo bao hamjaweza lipa naona kabisa mnaleta msemo wa Kiswahili MBAAZI UKIKOSA MAUA UNASINGIZIA JUA

Kama msingekuwa 13 jana (11 wachezaji wa ndani Refa na yule Linesmen m'1) dhidi yetu tuliomaliza 10 lile deni lilikuwa linarudi na kupitiliza
 

Penalt ya Ulaya kabisa hii,kumbe hata ndani ya Africa kuna watu wanaweza kupiga penalt za UlayaX2
 

Attachments

  • Kaseja 2.jpg
    44 KB · Views: 240
lazimsa nisema nilikuwa sipendi kabisa soka la bongo ila naona kuna improve kidogo.....kuna madogo watafika mbali kama siasa za rage zikipungua.....

kuna huyu sijui anaitwa edward christopher....bahanuzi.....kapombe....na mido mkali kiemba...hawa madogo wazuri sana aisee....wakifanya mazoezi na kula vizuri watafika mbali
 
Ilikuwa ni pouwa sana kuangalia match ile ndani ya superspot huwez amini kama ni bongo................Kuna mabadiliko makubwa sana ndani ya soka la bongo.........Big up Simba
 

Kweli kabisa Balantanda leo Kazimoto alipotea sana,Sunzu hawezi kucheza bila Okwi.Kwa Simba Kaseja,Kapombe,Ngalema ndio walicheza vizuri.Kiiza,Nizar nao walichemsha but Twite ni mchezaji mzuri saana sasa naamini ndio maana Rage alilia
 
Last edited by a moderator:
Huku mtaani kwetu Simba wenyewe wanakiri walikuwa wanaomba mpira uishe mana'ke kwa jinsi hali ilivyokuwa pamoja na Yanga kuwa pungufu lkn muda wowote watu walikuwa wanarudi kati
...hayo ni maneno yako tu:
mpira ulikuwa balanced kabisa japo kuna wakati kila Timu ilikua inatawala kwa kiasi fulani: mfano dk. 30 za kipindi cha kwanza Simba ilitawala na dk. 10 za mwisho kipindi cha pili Yanga nao walitawala na hii ilichangiwa na sub zilizofanywa na kocha wa Yanga, kwahiyo ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa kuona malengo ya kulipa kisasi cha goli 5-0 hayatimii na ile nia ya kuendeleza ubabe na umwamba inapotea.

Mi nawapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwani walituonyesha burudani ya kutosha kwakweli.
 
Ni kweli dogo kavunjika mguu? kama ni kweli pole sana Yondani, kiukweli Haruna alicheza rafu mbaya.


Mie sijui mpira/soka lakn kumvunja mwenzio mguu hata kama mnagombea sifa za magoli huo sio mpira...Ni kumharibia future kwa makusudi mwenzio ambaye siku moja mnaweza kuwa timu moja vilevile...
 

Kwakweli hata mimi nakubali game ilikuwa nzuri lkn Mtani......
Embu niambie,ukiacha dk 30 za kwanza ulizo'mention hapo Simba ilitawala dakika gani nyingine kati ya 60 nyingine za mchezo ule?, Kiss Fm wametoa tathmini ya mchezo ule jioni hii na wamesema Yanga walimaliza kipindi cha 2 wakiongoza kwa possesion ya mpira 69% dhidi ya 31% za Simba, sasa Mtani hii si ball possesion ya Barcelona dhidi ya team fulani ya daraja la kwanza ya Uingereza?
Kwa mtazamo wangu binafsi jana kukosa MUNGU+Referee+Assistant refferee(Linesmen) kuwa upande wenu hadithi ingekuwa ya tofauti kabisa.
 
Mie sijui mpira/soka lakn kumvunja mwenzio mguu hata kama mnagombea sifa za magoli huo sio mpira...Ni kumharibia future kwa makusudi mwenzio ambaye siku moja mnaweza kuwa timu moja vilevile...
Nimefuatilia vyombo vya habari, Yondani hakuvunjika ila mfupa mkubwa ulishituka na atakaa nje wiki mbili.
 
Ball possesion haiwezi kuwa hiyo mkuu waambie hao Kiss FM wataje ya ukweli, hao marefa utawasingizia tu kwamba waliibeba Simba, sehemu moja tu ambayo refa alitubeba nayo ni kutompa red Haruna hata jukwaani tulipokuwa tumekaa tuliona hilo na tukasema hapo refa katubeba, lakini ile njano aliyopewa Edward, Cannavaro alisukuma na ingekuwa penati, Cannavaro kamchezea rafu nyingi sana Sunzu mara zote wakati wanawania mpira alikuwa anamsukuma na mwisho refa alikosa uvumilivu akampa red, Mwasika naye alimuchezea rafu Kazimoto lakini mbali na kutopewa kadi hata faulo tu haikupigwa, siwezi kumlaumu refa labda alikuwa mbali na matukio au makosa ya kibinadamu tu lakini huwezi kusema kwamba aliibeba Simba. Wale wasaidizi kama ulikuwa makini kuangalia utaona Bahanuzi alikuwa anabaki peke yake akisubiri kupitishiwa kwa nini asiwe offside na ulitaka mwamuzi msaidizi amwache.

kuhusu kutawala kama dakika 10 za mwisho ilichangiwa na kutoka kwa Mkude na kuingia na kuingia Haruna Moshi, kiungo kilipoteana na baada ya rafu mbaya ambayo Haruna aliifanya nayo mchezoni, kama binadamu isingekuwa rahisi afanye ile faulo halafu aendelee kucheza vizuri hata ukiangalia picha vizuri amekita ule mkuu lakini usoni anaonekana kuumia kama vile yeye ndo alikanyagwa kwa hiyo hata yeye hakuifurahia hiyo faulo ilimtoa mchezoni kiukweli.
 
wachezaji wa Yanga kwa mechi ya jana walistahili kucheza kwa nguvu zao zote ili kuona kama wataweza kulipa kisasi cha goli 5-0 na Simba nia yao ilikuwa kufanya juu chini wanakwepa huo mpango; na kwa kudhiirisha hilo mara baada ya kupata goli 1 wachezaji wa Simba wali relax na kila mmoja alianza kuonyesha manjonjo yake, nafikiri vitu vya Mkude, Eddo na Sunzu ulivishuudia. Lengo kuu la wachezaji wa Simba ilikua ni kuaribu mipango mizima ya Yanga ili isiondoke na pointi3.

Hivyo kwa Ball-possesion kwa Yanga kuwa juu zaidi ya Simba si jambo la kushangaza ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwasababu ya presha na tention ya mchezo ilivyokuwa, lakini swala la kusema kwa KISS FM wanasema Ballpossesion ilikuwa Yanga-69% na Simba-31% huo ni uongo; takwimu za Supersport hadi mpira unamalizika zilikua zinasomeka 52% kwa 48% zaidi ya hapo sasa itakua ni maneno ya ushabiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…