Simba vs Mbeya City: kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Simba vs Mbeya City: kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Simba akichapa mtu huwa siyo habari njema kwetu hata kidogo, huwa tunajikuta tunazongwa, tunazomewa na hawa mashabiki wa mikia ndiyo maana hatupendi kabisa kuona mnyama akichapa mtu.

Rekodi ya Simba itatubeba tu kwani wataruhusu bao hilo kuchomolewa na kuongezwa la pili.

Hata baada ya Simba kuongoza msimamo wangu ulibaki vile vile! Hadi mwisho Simba 1-2 Mbeya City kama ilivyotabiriwa.
 
Mkuu Makoye Matale wee ni kiboko yao, hongera kwa utabiri wako.
Leo umeona kimya hapa, wangeshinda wao hapa wangekesha mpaka saa 8 za usiku.

Mkuu Bantu lady kwa leo tuko salama salmini, tutalala usingizi huku watani wakiuguza kipigo cha pili na kufuta kabisa rekodi yao kwamba ni timu iliyofungwa mechi moja tu. Ngoja nikaangalie msimamo, niwaone wameporomokaje kutoka nafasi ya 10.
 
Last edited by a moderator:
Mechi ya leo toka mwanzo mimi sikuona kama tungeweza kushinda, kulikuwa na tatizo, mipira mingi ilikuwa haifiki mbele. Tumekubali matokeo na tunaenda kujipanga kwa ajili ya mechi zinazokuja lakini kiukweli hali ni mbaya zaidi, ndani ya mechi nne tumepoteza pointi nane, hii ni hatari sana na benchi la ufundi lisipofanyia kazi hali huenda ikawa mbaya zaidi. Tuna mechi na mgambo halafu na JKT kabla ya kuanza mechi za raundi ya pili. Hata kama tutashinda zote tutakuwa na jumla ya pointi 19 tu wakati mwaka jana tuliona kama tunasuasua lakini tulimaliza round ya kwanza tukiwa na pointi 24.

Uongozi wa simba uache tabia ya kubagua wachezaji na kumpagia kocha kikosi, wachezaji tunao wazuri na endapo wachezaji wangekuwa wote wanatendewa kwa usawa pengine hali isingekuwa hivi ilivyo.

Tunachekana kiutani lakini ndio viongozi wetu Mkuu. Kocha akikubali kupangiwa timu ndio mwisho wake. Baadaye jumba bovu ataangushiwa yeye na hataweza kusema nilikuwa napangiwa timu. Too late!
 
Tatizo la bonanza la mapinduzi liliwapa kiburi.
 
Wanaofuatilia game ya tp mazembe vs azam watujuze tafadhali.
 
Amavubi, Masuke, Ngarna, sembo, Komeo Lachuma, everlenk grafani11 Crashwise barafuyamoto Freeland and CO.
Heshima yenu wakuu, naona mnavyojitahidi kushuka.
Wakati wenzenu tunapanda, tuliwaambia hii ni VPL na si bonanza.
Ila ukweli nimefurahi mwenzenu.

Kiukweli, tunahitaji kujirekebisha sana, maeneo mengi hayako sawa, ila ligi bado ni mapema, ingawa upande wa ubingwa, niwe mkweli, ni ndoto, ila mbili au tatu yunaweza kamata, timu yetu changa sana, makosa ni mengi na tuta-improve, bila shaka!
 
Last edited by a moderator:
Mbeya ciiiiiiiiiiittyyyyyyyy ni sheeedaaaah!Simba kanyonyolewa Manyoya mchana kweupeeeee.

Tena nyumbani, walifikiri hawa ni kama Ndanda FC, hii ni habari nyingine. Nawataka Pluijm na Mkwasa wawe makini na hii timu, vinginevyo tukikutana nayo mikia watakenua kama sisi hivi leo.
 
Tena nyumbani, walifikiri hawa ni kama Ndanda FC, hii ni habari nyingine. Nawataka Pluijm na Mkwasa wawe makini na hii timu, vinginevyo tukikutana nayo mikia watakenua kama sisi hivi leo.
Makoye mkwasa akichezanao wanatupiga vitasa wallahii
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! aaaaaahaaaah hanganasungwa ni mwana wa maye yooooo wasafwa watafurahi sn mwaka uu. kazen buti yanga na yy lazima alale. tutawalisha viazi za kuchemsha aka mowola mtajamba sn mwaka uu pumbafu sn simba na yanga. twenzele mtatukoma
 
Bantu lady leo utaongea sana. hamna shida yote maisha wametuzid wameshinda wala hatutasingizia uchawi au refari. si tunakubal mpira ndo uungwana. lakini bado sana ligi na usitukane mamba kabla hujavuka mto. sisi raha yetu ni kumfunga yanga tu. nyie yanga fanyeni muwezalo ila mkija kwa simba mnakaa. mi nipo tayar simba ifungwe na team zote lakini si na yanga.
 
Back
Top Bottom