Sijui huko kwenu, pale kwetu kuna watu wawili ndo wanaoharibu timu. Bosi mkubwa wa timu anaweza kuwa ni mzuri lakini wale jamaa wawili wamemshinda nguvu.
Kipigo cha leo naweza nisiwalaumu sana labda huenda kuwa kimechangiwa na kukosekana kwa wachezaji watatu ambao walikuwa wakianza sana sana ni wanne. Hassan Kessy anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Said Ndemla na Emmanuel Okwi hawa ni majeruhi
na Elias Maguri ingawa baadaye aliingia.
Mkuu mimi nashukuru Mungu siku hizi ule ushabiki wa sana umepungua, nakumbuka kuna mwaka nilikaa uwanjani kama nusu saa zaidi baada ya Simba kupoteza sijielewi na karibia mechi zote Simba ikishinda niko mji ambao wanacheza lazima niingie uwanjani lakini siku hizi nina kama miaka mitatu sijaingia uwanjani. Lakini kwa sababu ushabiki haufi kirahisi bado kahuzuni hakakosi timu ikifungwa na kafuraha hakakosi timu ikishinda.