Simba SC yamfukuza kazi kocha wake Logarusic

SIMBA SC imevunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kwamba Logarusic amevunjiwa Mkataba kwa kukiuka masharti ya mwajiri wake na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’ aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakuwa kaimu kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]
Kibarua kimeota magugu; Zdravko Logarusic amefukuzwa Simba SC baada ya miezi 10
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu na kikubwa ni kuwatolea maneno yasiyofaa wachezaji.
Inaelezwa Loga alifikia hatua ya kuwadharau na kuwatolea maneno yasiyofaa hadi viongozi wa klabu hiyo.
Loga anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Patrick Liewig aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

princezub@hotmail.com Mahmoud Zubeiry at 07:14 8/10/2014 07:11:00 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

Bin Zubeiry
 
Kufuatia klabu ya simba kufanya usajili wa pesa nyingi na timu kuonyesha kiwango duni kwenye mechi ya jana na kupata kipigo cha goli 3 kwa bila , uongozi wa klabu umechukua uamuzi mgumu wa kusitisha mkataba wa loga

Yule jamaa mimi nilikuwa sijawahi kumkubali kama kocha mzuri toka siku ya mechi ya mtani jembe, haiwezekani mchezaji akosee mara moja tu unamtoa bila kumpa nafasi nyingine halafu tabia ya kutukana wachezaji kama watoto sio kitu kizuri, inawezekana akawa ni mzuri technically lakini kama kiongozi unatakiwa pia kujua saikolojia ya wachezaji. Jana tu nilikuwa nabishana na mwanasimba mwenzangu nikawa namwambia Simba hatuna kocha na kama ataendelea huyu kuwepo tutafungwa mpaka tukome. Ni heri ameondolewa labda tutapata mwenye akili aina ya Patrick Phiri au James Siang'a.
 
Wakati nawaambia familia kuwa hata ndoa huvunjika wakanicheka. Lakini nawaambia ushabiki wangu kwa Simba umefika mwisho. Mi sio tenaaaa SIMBA!
 
Alikuwa hajalijua vizuri soka la bongo................................maskini we!!!!!!!!!! angemuuliza maximo kwanza kilichomfanya aogope kupeleka Yanga kwenye kombe la Kagame kabla hajachukua uamuzi mgumu wa kukubali mechi ya kirafiki
 
Yule kocha mkuu wa simba ambaye simba walimuajiri ili aifunge yanga tu.hatimaye leo amefukuzwa
 
Tatizo soka la Bongo wanampima kocha kwa mechi moja. Wanashindwa kujifunza kwa Arsene Wenger, Ferguson etc. Kwa mtindo huu Soka la Bongo kukua kufikia viwango vya kimataifa tusahau.
 
simba nayo timu? siku hizi ni yanga, azam na mbeya city tu. wengine tulishawasahau kama wana exist!

nimekumbuka ya mtani jembe! yalikuwa hivi hivi mechi hata haieleweki kocha chali
 
Tangu simba imfanyie fitina wambura siipendi tena, natamani wafungwe mechi zote. Wameacha kuzingatia misingi ya mpira wanatamani madaraka ili tu wawafukuze wale wenye fikira tofauti na wao watafune mali za klabu. Shame on you msimbaziz

We bado unamzungumzia Wambura. Alifanya nn alipokuwa FAT? Si hata makabidhiano hakufanya ? Kama ulikuwa unamtegemea Wambura ili muiibie Simba mmeshindwa kafanye kazi zako si kutegemea klabu iwatoe kwenye lindi la umasikini
 
Wiki iliyopita Tukiwa Sinza Matola alituambia Jambo ila Tukawa Tunafanya Mzaha na Kwa Muda Mrefu Sana Nahodha Owino alikuwa Akiniambia Kuwa Simba haina Kocha Nikawa namkatalia na Alinipa Sababu Kadhaa ILA Kubwa ni Kwamba ANAPENDA SANA KUGOMBEA MABINTI na WACHEZAJI Wake Na UKIMZIDI TU KWA HUYO DEMU basi UTACHUKIWA na KUYAOGA MATUSI Yake Na Ukifanya Masihara UNAWEZA HATA KUPIGWA NGUMI na Pia Hajui Kufundisha na Hana Mbinu na Anabahatisha Kiufundishaji Na Ni Jana Tu Nikiwa Uwanjani Taifa NAKUMBUKA MANENO YA MZEE Wetu Juma Mnonji Kuwa TOKEA AANZE KUWA MWANA SIMBA TOKEA ENZI ZA Sunderland na Sasa Simba Sports Club hajawahi Kuona Kocha MBOVU na MSANII Kama Logarusic. Kikubwa Zaidi Kilichomsibu Loga Haswa Jana Ni Kitendo Chake Cha KUWATUKANA WACHEZAJI Matusi Ya NGUONI ktk Dressing Room Huku Akitaka Kuwapiga Baadhi Kama Baba Ubaya, Uhuru na Banda Na Isingekuwa Busara Ya Matola Angewapiga Kweli. Na Ikumbukwe Pia Kuwa Logarusic Alikwishaonywa Kuhusiana Na Tabia Zake Hizo Na Kibaya Zaidi Anapenda Mno Starehe Na Vibinti Vidogo Vidogo huku Akishindwa Kuwa Responsible Kama Coach au Manager wa Klabu Kubwa. Kuna Uwezekano Milovan au Kikieleweka Patrick Phiri au Kocha Kutoka Kusini Mwa Afrika Akaja ila kwa Sasa Mzambia MATOLA Ndiyo Caretaker. Binafsi Napongeza Kutimuliwa Kwake kwani Dhahama Kubwa Ingetukumba huko Mbeleni.
 
Simba, nyie wehu wote kabisa! Mnafukuza kocha kwa ajili ya mechi ya kirafiki? Katavi, kamata dili hiyo ila ujue mechi yako moja tu kibarua hichoooooooo!
 
coaches are hired to be fired
 
Simba, nyie wehu wote kabisa! Mnafukuza kocha kwa ajili ya mechi ya kirafiki? Katavi, kamata dili hiyo ila ujue mechi yako moja tu kibarua hichoooooooo!
naamini nunafurahi kimoyomoyo kwamba TANO hazitakuwepo......................??????????
 
BARUA YA KUMMWAGA LOGA.jpg BARUA YA KUMMWAGA LOGA.jpg
 
heri angegombea videmu halafu tuone ufundi uwanjani
Wiki iliyopita Tukiwa Sinza Matola alituambia Jambo ila Tukawa Tunafanya Mzaha na Kwa Muda Mrefu Sana Nahodha Owino alikuwa Akiniambia Kuwa Simba haina Kocha Nikawa namkatalia na Alinipa Sababu Kadhaa ILA Kubwa ni Kwamba ANAPENDA SANA KUGOMBEA MABINTI na WACHEZAJI Wake Na UKIMZIDI TU KWA HUYO DEMU basi UTACHUKIWA na KUYAOGA MATUSI Yake Na Ukifanya Masihara UNAWEZA HATA KUPIGWA NGUMI na Pia Hajui Kufundisha na Hana Mbinu na Anabahatisha Kiufundishaji Na Ni Jana Tu Nikiwa Uwanjani Taifa NAKUMBUKA MANENO YA MZEE Wetu Juma Mnonji Kuwa TOKEA AANZE KUWA MWANA SIMBA TOKEA ENZI ZA Sunderland na Sasa Simba Sports Club hajawahi Kuona Kocha MBOVU na MSANII Kama Logarusic. Kikubwa Zaidi Kilichomsibu Loga Haswa Jana Ni Kitendo Chake Cha KUWATUKANA WACHEZAJI Matusi Ya NGUONI ktk Dressing Room Huku Akitaka Kuwapiga Baadhi Kama Baba Ubaya, Uhuru na Banda Na Isingekuwa Busara Ya Matola Angewapiga Kweli. Na Ikumbukwe Pia Kuwa Logarusic Alikwishaonywa Kuhusiana Na Tabia Zake Hizo Na Kibaya Zaidi Anapenda Mno Starehe Na Vibinti Vidogo Vidogo huku Akishindwa Kuwa Responsible Kama Coach au Manager wa Klabu Kubwa. Kuna Uwezekano Milovan au Kikieleweka Patrick Phiri au Kocha Kutoka Kusini Mwa Afrika Akaja ila kwa Sasa Mzambia MATOLA Ndiyo Caretaker. Binafsi Napongeza Kutimuliwa Kwake kwani Dhahama Kubwa Ingetukumba huko Mbeleni.
 
Wiki iliyopita Tukiwa Sinza Matola alituambia Jambo ila Tukawa Tunafanya Mzaha na Kwa Muda Mrefu Sana Nahodha Owino alikuwa Akiniambia Kuwa Simba haina Kocha Nikawa namkatalia na Alinipa Sababu Kadhaa ILA Kubwa ni Kwamba ANAPENDA SANA KUGOMBEA MABINTI na WACHEZAJI Wake Na UKIMZIDI TU KWA HUYO DEMU basi UTACHUKIWA na KUYAOGA MATUSI Yake Na Ukifanya Masihara UNAWEZA HATA KUPIGWA NGUMI na Pia Hajui Kufundisha na Hana Mbinu na Anabahatisha Kiufundishaji Na Ni Jana Tu Nikiwa Uwanjani Taifa NAKUMBUKA MANENO YA MZEE Wetu Juma Mnonji Kuwa TOKEA AANZE KUWA MWANA SIMBA TOKEA ENZI ZA Sunderland na Sasa Simba Sports Club hajawahi Kuona Kocha MBOVU na MSANII Kama Logarusic. Kikubwa Zaidi Kilichomsibu Loga Haswa Jana Ni Kitendo Chake Cha KUWATUKANA WACHEZAJI Matusi Ya NGUONI ktk Dressing Room Huku Akitaka Kuwapiga Baadhi Kama Baba Ubaya, Uhuru na Banda Na Isingekuwa Busara Ya Matola Angewapiga Kweli. Na Ikumbukwe Pia Kuwa Logarusic Alikwishaonywa Kuhusiana Na Tabia Zake Hizo Na Kibaya Zaidi Anapenda Mno Starehe Na Vibinti Vidogo Vidogo huku Akishindwa Kuwa Responsible Kama Coach au Manager wa Klabu Kubwa. Kuna Uwezekano Milovan au Kikieleweka Patrick Phiri au Kocha Kutoka Kusini Mwa Afrika Akaja ila kwa Sasa Mzambia MATOLA Ndiyo Caretaker. Binafsi Napongeza Kutimuliwa Kwake kwani Dhahama Kubwa Ingetukumba huko Mbeleni.
Hapa ieleweke wazi anayengelewa ni Selemani Matola na siyo Matola wa JF.

Matola wa JF hana muda na mambo ya fitina majungu na zengwe na ndio maana waliojaa kwenye soka la Bongo ni unskills people.

Na wewe nenda kamueleze Suleiman atafute shughuri za kufanya mambo ya Simba amuulize Julio na Kibaden.

Mpaka leo ni wachezaji watatu ndio naona walijitambuwa nao ni Leodgar Tenga, Mwamed Mwameja na Laurence Mwalusako basi. ukocha ni kazi ya watu ambao hawakucheza mpira.
 
Back
Top Bottom