Full Time | Jamus SC 0 - 0 Simba SC | CECAFA Kagame Cup | Kigali Pele Stadium

Full Time | Jamus SC 0 - 0 Simba SC | CECAFA Kagame Cup | Kigali Pele Stadium

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,162
Reaction score
17,626
Klabu ya Jamus baada ya kuwaduwaza Singida BS mechi iliyopita, leo anakutana na Mnyama Simba SC aliyetoka sare mechi iliyopita dhidi ya Mogadishu.

Je, nani kuondoka na alama tatu?...

1785230732351.png
 
LOEMBA .. mbona ni kama no fitness..no ubunifu
 
Simba yule striker Doumbia wametapeliwa. Striker kama wale hata Tandika wapo
Angalia sticking mfumo....ni kama kocha hajatengeneza mbinu za pamoja za ushambuliaji...
LOEMBA, GUEYYE, KAGOMA wanacheza more individual than team work...lakini bado sioni lawama kwa Dombia kwa team ambayo hutengenezi clear fiinal assist
 
Poleni wana Simba maana huo uongozi wenu ndio kila msimu unajigamba kuwa unafanya usajili kwa ajili ya kuleta kombe la Afrika. Usajili wenyewe sasa wamefungashiwa Doumbiwa kwenye "parcel" na nyongeza ya Mothus Cooper. Kiukweli kabisa viongozi wa Simba hawajawatendea haki wana Simba. Timu imekosa ubingwa mwaka jana sababu kubwa ikiwa ni kukosa mshambuliaji wa kati na golikipa imara japo kulikuwa na makosa ya waamuzi . Lakini kwangu mimi iwapo Simba ingekuwa na washambuliaji/mshambuliaji makini wa kati wenye uwezo na kipa imara bado Simba ingebeba ubingwa licha ya hayo makosa ya waamuzi.

Kwa hiyo basi kiufundi nilitegemea basi kwenye usajili huu wachezaji wa kwanza kusajiliwa ni washambuliaji mahiri wa kati wawili wa kimataIfa na mmoja wa ndani na kipa mahiri mmoja wa kimataifa. Pia nilitegemea kati ya Maema na Kante mmoja asepe maana kuwaacha wote kwa pamoja ni gharama na hasa Kante kwani ni lazima alipwe pesa nyingi kutokana na mkataba wake. Hapa nilitegemea Simba iongeze kiungo mmoja wa kimataifa ambaye angekuwa anacheza namba sita na nane "comfortably". Kwa upande wa mabeki wa kati nitegemea Simba ibaki kama ilivyo na Toure na Rushnie wakisaidiana na wazawa watatu ambao wanazima vizuri kabisa pale nyuma hao wakina Mbegu, Masinde na Nangu. Hamza huyo sio wa kutegemewa sasa hivi kwa sababu ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu hivyo itamchukua muda mrefu kurudisha kiwango chake hivyo chaguo sahihi ni kumpeleka kwa mkopo kwenye timu za madaraji ya kati apate game time ya kutosha arudishe kiwango chake

Sasa kilichotokea kimeniacha mdomo wazi:-

1. Simba hii leo ni ya kumleta Mothus Cooper kuja kufanya majaribio. Kweli viongozi wapo serious. Huyo mchezaji ukimwangalia tu kwa umbo lake hawezi kabisa kucheza ligi yetu. Hivi kweli huyo mchezaji akutane papatupapatu na mwamba Mtenje si siku hiyo hiyo ataomba tiketi ya ndege arudi kwao. Na mbaya zaidi unampa thank you Muzamiru halafu unataka kumsajili Mothus kweli vioja havitaisha Simba. Hawa viongozi hawajui kuwa Simba iliwahi kuwa na ushirikiano na Enyima wakapewa vijana wadogo wa miaka 16 Emme Izuchuku na Orji Obina kwa majaribio na wakacheza ligi vizuri tu. Sasa leo 2026 kiongozi unamleta Mothus miaka ya paspoti 29 je yake ya kweli sio miak 35 yule? Nilitegemea sasa hivi viongozi watafute ushirikiano na timu kama Mamelodi ambayo ina wachezaji vijana wenye vipaji wasio na idadi ambapo Simba ingefaidika.

2. Jambo la pili ni kuhusiana na golikipa. Niliposikia tu viongozi wameamua kuendela na Kasali nikajua tayari mwaka mwingine wa tabu kwa mashabiki na wapenzi Simba. Huyo kipa ana mapungufu mengi sana lakini kama viongozi hawajayaona na wanaamini kabisa watabeba kombe la Afrika Kasali akiwa golini basi kuna tatizo kubwa sana kwenye uongozi wa Simba.

3.Usajili wa Doumbia. Hapa ndio viongozi wa Simba wamedhihirisha kabisa hawapo makini. Sidhani kama kuna kiongozi wa Simba aliyewahi kumfuatilia huyu mchezaji kabla hajasajiliwa. Huyu usajili wake ni kama wa Mukwala tu. Wakala anakuletea video, picha na jina la mchezaji na takwimu zake za miaka miwili basi unashawishika unatoa hela unamsajili mchezaji. Takwimu na video clips zinadanganyana sana. Hii Simba ina hazina ya wachezaji wa zamani ambao wengine ni makocha na hata viongozi wa zamani wapo wanaoweza kusaidia hata bure kufanya "scouting" ya wachezaji ili mradi tu wawezewshwe. Tatizo la viongozi ni kukariri tu wanashindwa kuwa wabunifu. Hivi kwa mfano ukawapa tiketi za ndege na posho kidogo kwa mfano mdogo tu wa haraka na sio nampigia debe mtu hapa ukawachukua Pawasa, Jamhuri, Rage, Kaburu ukawatuma hebu nendeni hizi wiki mbili wakamfuatilie mcheaji fulani Kongo na wengi uwatume nchi nyingine wakati ligi zinaendelea. Nina hakika utapata wachezaji wazuri kwa bei rahisi sana maana hapo hakuna dalali japo nyie mnawaita mawakala. Hao mawakala hawana tofauti na dalali kwani kuna tofauti gani ya mtu aliyepangishwa/kuuziwa nyumba bondeni kwenye mafuriko wakati wa kiangazi na Simba waliouziwa Doumbiwa wakati wa usajili wote pesa yao inakuwa imepotea bure kabisa huku walichokinunua kwa gharama hawajakipata

4. Kingine nilichokiona kwa Simba ni kama kunakutjitambua hivi. Hivi inawezekenaje uende ukashiriki mashindano halafu unachokitafuta hakijulikani. Walisema "pre season" yao ni Kagame cup. Nilitegemea basi wawe "serious" kupamabana na kuchezesha wachezaji wa kutegemewa wa zamani na wapya ili kupata chemistry ya timu. Badala yake ni mizaha tu Semfuko anacheza pamoja na straika lao refu kuliko goli wakati Semfuko sio regular pale Simba. Hiyo chemistry itatoka wapi?. Lingekuwa jambo la maana kwao iwapo wasingeshiriki mashindano ambayo wanajiaabisha tu na kuwapa wakati mgumu wadhamini wao hasa yule mdhamini wa jezi na badala yake wangefanya pre seaon ya kujificha na kutafuta mechi na timu kubwa mbili tatu hivi ingewasaidia zaidi kuliko hiki wanachokifanya kwenye Kagame cup.

5. Mwisho viongozi waliopo Simba sasa hivi wakubali tu kuwa mpira sasa hivi umebadilika sana. Hivyo wawaandae vijana wa kuja kuchukua nafasi zao na wao wabaki kama washauri tu. Kuongoza mpira sasa hivi inabid ubunifu na kukimbia kimbia huku na kule kitu ambacho kwa mtu mwenye umri mkubwa ni tatizo.

Ni mtizamo tu
 
Mshambuliaji wa Kati yupo, why Loemba acheze 9? huyu kocha amechoka maisha ya Tz, anafanya kusudi ili afukuzwe
Wewe umeona mbali. Huyo kocha kwa mwonekano wake yupo makini sasa kama viongozi wanaleta uswahili wao ataondoka zake. Nina wasiwasi alihitaji mshambuliaji wa maana halafu anashangaa kaletewa garasa. Sidhani kama huyo kocha angekosa namba tisa wa maana kwenye ligi ya kwao pale South Africa hasa ukizingatia amefundisha miaka mingi sana na wachezaji wengi anawajua.
 
Mshambuliaji wa Kati yupo, why Loemba acheze 9? huyu kocha amechoka maisha ya Tz, anafanya kusudi ili afukuzwe
Simba wanayatumia haya mashindano kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya wa ligi. Kocha anajaribu kuwachezesha wachezaji wote ili atambue uwezo wao kwa kina kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
 
Simba wanayatumia haya mashindano kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya wa ligi. Kocha anajaribi kuwachezesha wachezaji wote ili atambue uwezo wao kwa kina kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Hii ndio fact ambayo mashabiki hawataki kuelewa. Halafu baadae husema timu haikujiandaa japo Kwa michezo kadhaa
 
Back
Top Bottom