Thread Yako Mbona Kama Vile Inanishambulia Kiaina AU Kama Vile Nimekukosea? Tatizo Ni ID Ya MATOLA au Tatizo Ni Ufafanuzi Wa GENTAMYCINE? Na Nilikuwa Na Uhakika Kuwa ID Yako Siyo Ya Comrade Wangu Suleiman Abdallah Matola ( Mzambia / Veron ) Ila Umeamua Kutumia Jina Lake Kwakuwa Unajua Ni Mchezaji wa Kiungo Uliyempenda Na Mwenye Mafanikio Makubwa Simba Sports Club na Hakuna Anayelipinga Hilo. Hata Mimi ID Yangu Ya GENTAMYCINE Nimeichukua Kutoka Kwa Rapa Mkubwa Wa Wenge Musica BCBG Aitwae Gentamycine Lisimo (Le Champion Animateur du Congo ) ambaye Nimetokea Kumpenda Kuliko Maelezo Na Kuna Mwingine Humu Ana ID Ya Roga Roga na Najua Hata Yeye Ameamua Kujiita Hivyo Kutokana Na Mapenzi Yake Kwa Mpiga Solo Maarufu Congo Brazaville wa Kundi La Extra Musica aitwae Roga Roga ( Ibambi Ikombi ) Na Wengineo Wengi tu. Matola Naamini Wewe Ni Mdau wa Soka hivyo Yote Hayo Uliyonitaka Nikamwambie Wajina Wako Ningeomba Ukamwelezee Mwenyewe ILA Nahisi Una Chuki Binafsi Kwa Matola na Simba Yetu Ya Aveva na Yawezekana Wewe Unatoka ktk Kundi Lile La Waliofukuzwa ambao Juzi Uwanjani Mlijitenga na Mkaa Mbali Huku Mkiwa Mmevalia Suti Zenu Nyeusi, Mashati Meusi na Tai Zenu Nyekundu za Asante Kariakoo Mlizoshonewa Na Fundi Wenu Mkuu Wambura.