Simba SC 1-0 Mbeya Kwanza | Benjamin Mkapa |NBC PL

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Timu ndiyo zinaingia uwanjani, muda wowote mchezo huu wa Ligi Kuu Bara utaanza hapa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

KIPINDI CHA KWANZA

Mchezo umeanza.
Dk 1: Mwamuzi anapuliza kipenga cha kuanza kwa mchezo.
Dk 1: Simba wanaanza kwa kasi, wanafika langoni mwa Mbeya Kwanza, John Bocco anashindwa kumalizia mpira aliotanguliziwa.
Dk 3: Simba wameanza kwa kasi na wanamiliki mpira muda mwingi.
Dk 5: Mbeya Kwanza hawajafika langoni mwa Simba mpaka muda huu.
Dk 9: Sakho anapiga shuti kali akiwa nje ya eneo la 18, kipa anapangu inakuwa kona.
Dk 10: Simba wanaonekana kuwa na kasi ya kutafuta bao la mapema.
Dk 12: Mbeya Kwanza wanapata kona, wanapiga akini inaokolewa.
Dk 14: Mbeya Kwanza wanafanya shambulizi la kupiga shuti kali lakini Aishi Manula anadaka.
Dk 15: Sakho anapiga shuti lingine kali lakini linatoka nje la lango.
Dk 17: Mbeya City nao wanaonyesha kuwa wapo makini, mchezo unatawaliwa na kasi.
Dk 23: William Edigar wa Mbeya Kwanza anapata nafasi lakini shuti lake linakosa nguvu, linadakwa na Manula.
Dk 25: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dk 30: Simba wanaendelea kulisakama lango la wapinzani.
Dk 33: Simba wanafanya shambulizi kali, Meddie Kagere anaukosa mpira kwa kichwa inakuwa kona.
Dk 38: Sakho anafanya kazi nzuri ya kuingiza mpira kwenye box ya wapinzani lakini hakuna wa kuimalizia.
Dk 40: Matokeo bado ni 0-0.
Dk 41: Kanoute anapiga shuti linapaa juu.
Dk 44: Simba wanafanya mashambulizi mawili makali lakini bado ukuta unakuwa mgumu.
Dk 45: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

MAPUMZIKO

KIPINDI CHA PILI
Dk 46: Kipindi cha pili kimeanza.
Dk 50: Mashambulizi ni ya kupokezana.
Dk 52: Kagere anashindwa kuutumia vizuri mpira uliomponyoka kipa wa Mbeya Kwanza.
Dk 55: Mbeya Kwanza wanafanya shambulizi la nguvu, mpira unapaa juu.
Dk 58: Mbeya Kwanza nao wanasogea mbele na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Dk 60: Simba wanafanya mabadiliko, Bocco na Mkude wanatoka, wanaingia Chama na Mugalu.
Dk 65: Mugalu anaoata nafasi nzuri lakini shuti lake linapaa juu ya lango.
Dk 69: Dilunga yupo nje anajiandaa kuingia kutokea benchi.
Dk 70: Dilunga anaingia, anatoka Bwalya.
Dk 72: Kipa wa Mbeya Kwanza anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda.
Dk 77: Kipa wa Mbeya Kwanza yupo chini, anatibiwa.
Dk 79: Mchezo unaendelea.
Dk 80: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Chama anaipatia Simba bao baada ya purukushani za kuwania mpira langoni mwa lango la Mbeya Kwanza.
Dk 86: Mchezo umekuwa mkali, Mbeya Kwanza wanafunguka na kusogea mbele kushambulia.
Dk 88: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kagere na Sakho, wanaingia Erasto Nyoni na Gadiel Michael.
Dk 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 5 za nyongeza.
Dk 90+2: Timu zote zinafunguka, presha inakuwa kubwa.
Dk 90+4: Mbeya Kwanza wanapata faulo baada ya Inonga kucheza faulo. Inapigwa inaokolewa.
Dk 90+5: Mwamuzi anamaliza mchezo.

FULL TIME

sIMBAA.jpg
 
Back
Top Bottom