Simba S.C. kwenda Angola siku moja kabla ya mechi ni takwa la kiufundi au bajeti imekata?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,721
109,155
Na kama ni takwa la kiufundi mwambieni huyo aliyeamua hivi kuwa hii ni hatari na itatugharimu kimatokeo.

Ningewaelewa Simba S.C. (hasa kiufundi) kama wangeenda Angola siku tatu kabla ila hii ya kwenda siku moja kabla ya mechi (yaani Jumamosi na kucheza Jumapili) ni hatari kimchezo (kimaandalizi), na hapa wala GENTAMYCINE nisimung'unye maneno kuwa tumefanya kosa kubwa sana.

Hivi kweli ndani ya siku moja huko Angola wachezaji wa Simba S.C. watazoea hali ya hewa, mazingira kiujumla na kuzoea uwanja ili kuweza kujiandaa vyema kisaikolojia kwa mchezo husika wa siku ya Jumapili? Hii ni kujiua kiufundi kwa Simba S.C. na tutake tusitake ni lazima itatugharimu katika utendaji wetu uwanjani siku ya mtanange (mechi).

Nilikuwa mbishi kuamini kuwa sasa Simba S.C. kuna ukata (bajeti hafifu) na pia mwekezaji Mo Dewji ni kama vile amesusa na kajiweka kando, ila kwa hili la kwenda nchini Angola Jumamosi na mechi Jumapili naamini rasmi kuwa mzigo ndani ya Simba S.C. umekata na wala tusitake kudanganyana juu ya hili.

Ukiwa umecheza mpira, ni mtu wa mpira au ni mdau (mchambuzi na mwaimu) wa mpira utanielewa vyema GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa, ila ukiwa ni "Ngala ngala' kamwe hutonielewa na utabaki kunishangaa tu.

Kazi ipo tu Jumapili kwa Waangola!
 
Na kama ni takwa la Kiufundi mwambieni huyo aliyeamua hivi kuwa hii ni Hatari na itatugharimu Kimatokeo.

Ningewaelewa Simba SC ( hasa Kiufundi ) kama wangeenda Angola Siku Tatu kabla ila hii ya kwenda Siku Moja kabla ya Mechi ( yaani Jumamosi na Kucheza Jumapili ) ni Hatari Kimchezo ( Kimaandalizi ) na hapa wala GENTAMYCINE nisimung'unye maneno kuwa tumefanya Kosa Kubwa sana.

Hivi kweli ndani ya Siku Moja huko Angola Wachezaji wa Simba SC watazoea Hali ya Hewa, Mazingira Kiujumla na Pitch Familiarization ili kuweza Kujiandaa vyema Kisaikolojia kwa Mchezo husika wa Siku ya Jumapili?

Hii ni 'Technical Suicidal' kwa Simba SC na tutake tusitake ni lazima itatugharimu katika 'performance' yetu Uwanjani Siku ya Mtanange ( Mechi )

Nilikuwa Mbishi kuamini kuwa sasa Simba SC kuna Ukata ( Bajeti hafifu ) na pia Mwekezaji Mo Dewji no kama vile amesusa na kajiweka kando, ila kwa hili la kwenda nchini Angola Jumamosi na Mechi Jumapili naamini rasmi kuwa Mzigo ndani ya Simba SC umekata na wala tusitake Kudanganyana juu ya hili.

Ukiwa umecheza Mpira au ni Mtu wa Mpira au ni Mdau ( Mchambuzi na Mwaimu ) wa Mpira utanielewa vyema GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa ila ukiwa ni "Ngala Ngala' kamwe hutonielewa na utabaki Kunishangaa tu.

Kazi ipo tu Jumapili kwa Waangola!!!
Ile timu inamilikiwa na jeshi na wanafigisu nyingi mno uko kwao na usipoenda kwa tahadhari Mambo yanaweza kuwa tofauti.

Rejea kikosi Cha Namungo mwaka Jana walivyokumbana na figisu za korona na kupelekea kutengwa na kushindia mikate.
 
Na kama ni takwa la Kiufundi mwambieni huyo aliyeamua hivi kuwa hii ni Hatari na itatugharimu Kimatokeo.

Ningewaelewa Simba SC ( hasa Kiufundi ) kama wangeenda Angola Siku Tatu kabla ila hii ya kwenda Siku Moja kabla ya Mechi ( yaani Jumamosi na Kucheza Jumapili ) ni Hatari Kimchezo ( Kimaandalizi ) na hapa wala GENTAMYCINE nisimung'unye maneno kuwa tumefanya Kosa Kubwa sana.

Hivi kweli ndani ya Siku Moja huko Angola Wachezaji wa Simba SC watazoea Hali ya Hewa, Mazingira Kiujumla na Pitch Familiarization ili kuweza Kujiandaa vyema Kisaikolojia kwa Mchezo husika wa Siku ya Jumapili?

Hii ni 'Technical Suicidal' kwa Simba SC na tutake tusitake ni lazima itatugharimu katika 'performance' yetu Uwanjani Siku ya Mtanange ( Mechi )

Nilikuwa Mbishi kuamini kuwa sasa Simba SC kuna Ukata ( Bajeti hafifu ) na pia Mwekezaji Mo Dewji no kama vile amesusa na kajiweka kando, ila kwa hili la kwenda nchini Angola Jumamosi na Mechi Jumapili naamini rasmi kuwa Mzigo ndani ya Simba SC umekata na wala tusitake Kudanganyana juu ya hili.

Ukiwa umecheza Mpira au ni Mtu wa Mpira au ni Mdau ( Mchambuzi na Mwaimu ) wa Mpira utanielewa vyema GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa ila ukiwa ni "Ngala Ngala' kamwe hutonielewa na utabaki Kunishangaa tu.

Kazi ipo tu Jumapili kwa Waangola!!!
Mwamedi keshaichoka Simba, anaona tayari inaweza kumuingizia hela hata asipowekeza hata shilingi kumi, kahamia kwa kina Mandonga
 
Na kama ni takwa la Kiufundi mwambieni huyo aliyeamua hivi kuwa hii ni Hatari na itatugharimu Kimatokeo.

Ningewaelewa Simba SC ( hasa Kiufundi ) kama wangeenda Angola Siku Tatu kabla ila hii ya kwenda Siku Moja kabla ya Mechi ( yaani Jumamosi na Kucheza Jumapili ) ni Hatari Kimchezo ( Kimaandalizi ) na hapa wala GENTAMYCINE nisimung'unye maneno kuwa tumefanya Kosa Kubwa sana.

Hivi kweli ndani ya Siku Moja huko Angola Wachezaji wa Simba SC watazoea Hali ya Hewa, Mazingira Kiujumla na Pitch Familiarization ili kuweza Kujiandaa vyema Kisaikolojia kwa Mchezo husika wa Siku ya Jumapili?

Hii ni 'Technical Suicidal' kwa Simba SC na tutake tusitake ni lazima itatugharimu katika 'performance' yetu Uwanjani Siku ya Mtanange ( Mechi )

Nilikuwa Mbishi kuamini kuwa sasa Simba SC kuna Ukata ( Bajeti hafifu ) na pia Mwekezaji Mo Dewji no kama vile amesusa na kajiweka kando, ila kwa hili la kwenda nchini Angola Jumamosi na Mechi Jumapili naamini rasmi kuwa Mzigo ndani ya Simba SC umekata na wala tusitake Kudanganyana juu ya hili.

Ukiwa umecheza Mpira au ni Mtu wa Mpira au ni Mdau ( Mchambuzi na Mwaimu ) wa Mpira utanielewa vyema GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa ila ukiwa ni "Ngala Ngala' kamwe hutonielewa na utabaki Kunishangaa tu.

Kazi ipo tu Jumapili kwa Waangola!!!
Wanazo b.26 za m.bet bwana🤣🤣 niliwahi kusema hapa jukwaani kuwa thamani ya pesa ya udhamini uliotangazwa na hivi vilabu itaonekana kwa vitendo na muongo atajulikana tu sasa maji na mafuta vimeshaanza kujitenga, b.26 kwa miaka 5 iliyoandikwa kwenye jezi dhidi ya b.11 kwa miaka 3 uhalisia utazidi kuonekana kadri muda unavyosonga mbele.
 
Futa huu upuuzi
 
Sisi ambao hatujacheza mpira na kupiga danadana walau 5 tu ni mtihani (na hata kwenye mechi za 'chandimu' utotoni tulikuwa hatupangwi,hadi pale ngumi zinapoanza ndo umuhimu wetu unapoonekana) tunacomment wapi?

Anyway, nimejaribu tu ku-imagine;vipi kama wangeenda siku 3 kabla ya mechi halafu wakanyimwa uwanja wa mazoezi kwa siku hizo zote (na figisu nyinginezo) huoni kwamba ndo ingekuwa hatari zaidi? Pengine intelijensia ya Simba SC imenusa kitu.
 
Timu haina hela! Ndiyo maana Mlete Mungu kaamua kukimbia njaa! Mwekezaji hela anazihamishia kwenye boxing. Hata sijui mashabiki tufanyeje! Kama vipi tuanze tu kupitisha bakuli. Maana hakuna namna.

Huwezi kwenda kucheza ugenini siku 1 kabla ya mchezo. Na ikitokea timu ikafungwa, tusisikie visingizio.
 
Advance part ya timu yenu ndio inayo enda kuandaa mazingira ya timu itakapo fikia na uwanja wa mazoezi, uwanja utakao chezewa mechi haufanyiwi mazoezi isipokua siku Moja kabla ya mechi mnaenda ku ukagua na kupasha kidogo.
 
Wacha zako.
 
Hivi kweli ndani ya siku moja huko Angola wachezaji wa Simba S.C. watazoea hali ya hewa, mazingira kiujumla na kuzoea uwanja ili kuweza kujiandaa vyema
Zalan waliweka pre season hapa hapa Dar, wakacheza mechi yao ya nyumbani hapa hapa Dar, wakaisubiri mechi yao ya ugenini wakiwa hapa hapa Dar, matokeo yake walifungwa jumla goli 9-0.

Hivi ilikuwaje kwa wiki tatu nzima wameshindwa kuzoea mazingira, uwanja na hali ya hewa, hadi wakafungwa idadi kubwa hivyo ya mabao?
 
Advance part ya timu yenu ndio inayo enda kuandaa mazingira ya timu itakapo fikia na uwanja wa mazoezi, uwanja utakao chezewa mechi haufanyiwi mazoezi isipokua siku Moja kabla ya mechi mnaenda ku ukagua na kupasha kidogo.
km walivyokuja lubumbashi kipindi wanacheza na tp mazembe binafsi naona sawa .
 
Huna hela na unaenda kwa ndege ya kukodi?
Uwahi kuzoea uwanja gani na uwanjani utaruhusiwa siku moja before game?

Hali ya hewa ipi unaenda kuzoea, ikiwa dar ni 30° na Angola ni 26 to 28 ? Kuna tofauti inayohitaji adoptation hapo?

Msimu huu ni cool kwao,
Check ur facts popoma.
Kwanini misimu iliyopita walikuwa wanaenda kukaa zaidi ya siku tatu mfano msimu uliopita tuliona timu ina safari siku tano kabla ya mchezo. Ni kipi kilipelekea kufanya hivyo

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom