tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,847
- 18,253
Zamani kabla mikeka haijaingia hapa nchini mashabiki wa mpira walikuwa na ushabiki halisi kwa timu zao pendwa. Nakumbuka mechi kati ya Man United na Arsenal iliyochezwa mwaka 2003. Van Van Nistelrooy alikosa penati dakika za majeruhi. Siku hiyo kulikuwa na mshawasha mkubwa sana miongoni mwa mashabiki wa miamba hii miwili ya soka la England.
View: https://www.youtube.com/watch?v=hhA3wcvrgyY
Tulitazama mpira huo kwenye banda moja la mpira mjini Morogoro karibu na hoteli ya GM. Kulikuwa na mashabiki wengi sana. Banda lilijaa hadi mwenye banda akalazimika kutuhamishia kwenye TV nyingine iliyokuwa uwani. Nako kulijaa pomoni. Mashabiki walikuwa na ari kubwa sana kila mmoja akiitambia timu yake kushinda. Bahati mbaya Man United wakakosa penati dakika za majeruhi, kitendo kiliwasononesha mashabiki wake mpaka leo.
Kwa sasa ushabiki wa mpira umedorora sana. Si kwa sababu nyingine bali ni kwa saabu ususi wa mikeka. Siku hizi ni kawaida shabiki wa Arsenal kuiua timu yake kwenye mkeka na kuipa ushindi timu pinzani. Kitendo hiki huua kabisa ule ushabiki uliomo ndani ya shabiki aliyesuka mkeka na kuamua kuia timu yake. Kwa mujibu wa utafiti nilioufanya hivi karibuni, zaidi ya 90% ya mashabiki wa mpira waasuka mikeka.
Siku moja nilikuwa mahali fulani natazama mpira nikashuhudia shabiki wa Man United anashangilia goli baada ya timu yake kufungwa. Nilishikwa na butwaa nikidhani labda yule shabiki ni mwehu. Kabla sijamaliza kushangaa, nikamuona anaomba kalamu na kuweka tiki kwenye mkeka. Ndipo nilipogutuka kumbe alikuwa anshangilia mkeka sio timu.
Ni kawaida kwa shabiki wa timu A kuonekana anaishangilia timu B ambayo ni mpinzani mkubwa wa timu yake kwa sababu tu timu B ikishinda mkeka wake unapumua. Katika hali kama hii, unadhani msisimko wa kishabiki utatoka wapi?
Mashabiki wengi wa aina hii huwa wanaepuka kwenda kutazama mpira mubashara, hasa pale wanapokuwa wamesuka mikeka na kuziua timu zao au kuzipa ushindi timu pinzani. Badala yake hubakia mafichoni wakifuatilia matokeo kwenye simu au kwa kuwapigia simu mashabiki wanaotazama mpira mubashara. Hii ndio sababu ya mashabiki wengi kushindwa kutazama mpira timu zao zinapocheza. Wanawaza mikeka tu!
Kitendo hiki cha kushabikia mikeka ghairi ya timu kimechangia pakubwa kuharibu ushabiki asilia wa mpira kama ilivyokuwa hapo zamani kabla ya mauzauza ya mikeka kuingia hapa nchini.
Nawasilisha.