SIMBA na usajili msimu ujao

Izy_Name

JF-Expert Member
Apr 9, 2020
647
1,295
KOCHA Mkuu wa Simba Robert Oliveira ‘Robertinho’ amepania kuongeza idadi ya mastar katika kilabu ya Simba huku akitazamia zaidi katika mechi za kimataifa, kwa sasa kwa kila mchezo anaocheza uwe wa kimataifa au wa ndani anakuwa na kazi nyingine ya kutafakari nini kimepelea na nini cha kuongeza, usajili wa msimu ujao akiwasoma mastaa bora anaokutana nao katika mechi kisha kubaki na faili lao ili usajili ukianza awe amemaliza kila kitu.



Robertinho amewambia wandishi wa habari kuwa tayari ana majina makubwa ya wachezaji wa nje na ndani katika faili lake na hao sio kwamba amemaliza pia anawafuatilia taratibu katika mechi zingine juu ya mwendelezo wa ubora wao.

Simba imefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa nafasi ya pili ya Kundi C ikiwa na pointi tisa nyuma ya vinara Raja Casablanca watakaomaliza nao mechi ya mwisho wenye pointi 13, lakini kocha huyo raia wa Brazili amesema anataka kufanya kazi hiyo mapema kisha atakaa na mabosi wa timu kufanya uamuzi wa mwisho lengo likiwa wawe na kikosi bora kitakachokusanya mataji muhimu ya ndani na kimataifa.

Simba iliyotinga robo fainali kwa sasa ina mastaa walioibeba hatua hiyo akiwamo Clalous Chama mwenye mabao manne akiwa kinara wa ufungaji wa ligi hiyo ya mabingwa, Moses Phiri mabao matano kwenye mechi za awali, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza, Hennock Inonga, Sadio Kanoute na Pape Ousmane Sakho aliyetwaa tuzo ya Bao Bora la Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

“Kwenye kila mchezo kazi yangu haishii tu kuhakikisha tunashinda, lakini tunatafuta watu bora ambao tunawaona na baada ya hapo nawafuatilia baadaye je viwango vyao bora vimeendelea au aliocheza kwa ubora tulipokutana naye tu,” alisema Robertnho.

“Tunafuatilia wachezaji wote wa ndani na wa nje kuangalia wapi tunataka kuongeza mtu kulingana na ubora tunaouona kwa wachezaji tulionao sasa na baadaye nitakaa na viongozi mapema kufanya maamuzi.”

Vilevile Robertinho aliongeza kwa kikosi chake cha msimu ujao amepanga kiwe na uwiano mzuri kwa kila nafasi kuwa na wachezaji wawili wenye ubora wa juu na unaokaribiana ili kutengeneza ushindani mzuri wa kusaka nafasi.

“Ukiangalia sasa kuna nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili, nadhani namna nzuri ni kuwa na uwiano mzuri wa wa kikosi, tunaweza kuwa na kikosi cha wachezaji ambao kila nafasi kuna watu wawili lakini kitu muhimu hapa ubora wao uwe mkubwa hata ukilingana sio mbaya na baadaye tuwaache washindanie nafasi.

“Nitahakikisha tunakuwa na kikosi bora sana kwa kuwa mashindano tunayoshiriki na ubora wa timu pinzani yanatulazimisha kuwa na ubora huo lakini hapa lazima tukubaliane Simba ina jina kubwa na lazima mchezaji tutakayekuwa naye awe na hadhi ya jina la Simba nafikiri hili ni kubwa.

“Simba inashiriki mashindano makubwa dhidi ya klabu zingine kubwa za ndani na nje ya nchi lazima mchezaji atambue kwamba anapokuja Simba awe na utayari wa kuipigania klabu hii kubwa na sio kuja kusota benchi na kushindwa kupigania nafasi.”
 
Robert amejitengezea mwenyewe shimo lake atakalodumbukia kwa kuropoka huko umbumbumbuni Wana hasira wamefura maana makombe hatopata kwasasa ni Mali ya Yanga na mbumbumbu watamtimua katikati ya msimu!

Mdomo siku zote huponza kichwa!
 
Acha uongo,ashindwe kutazama kwenye klabu bingwa aje atazame kwenye afcon ambako kuna idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza kwenye ligi za nje ya afrika,uwezo wa kuwalipa simba hatuna
 
Wampe muda, lakini pia wampe uhuru wa kuisuka timu upya kama ilivyotokea kwa Prof. Nabi wa Yanga.
 
Ligi kwani imeisha?

Pesa za usajili atatoa nani?

Huyo kocha hana muda mrefu atatimuliwa
 
Binafsi naona Simba Kuna mashimo ma5 tu

Toa Sawadogo leta mwanaume
Toa kapama leta ndemla/feisal/Nashoni
Toa Gadiel leta Kibabage
Toa Outara leta mtu wa kazi
Toa Okra leta Dube
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom