Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 609
- 1,563
Nimeifatilia Simba kwenye mechi zote za mapinduzi cup na nimeona bado wanayo matatizo makubwa sana ya kiufundi, nilitegemea mabadiliko baada ya benchikha kuichukua timu lakini silioni ilo kwa sasa!
Simba bado Wana shida ya kucheza mpira wa taratibu na kujenga mashambulizi kwa mwendo wa konokono jambo ambalo ukicheza na timu yenye kocha mjanja na wachezaji wenye fitness ya juu auwezi kutoboa!
Kocha wa singida alilijua ilo baada ya kuwasoma vizuri namna wanavyocheza ndio maana wamepata tabu kubwa sana kiuchezaji kabla ya refa kufanya yake na kagere kutoa mkono wa shukrani kwa waajiri wake wa zamani!
Singida Kama wangeongeza umakini kidogo tu na daraja la ubora kidogo walikuwa wanaumaliza mchezo ndani ya dk 45 za kwanza!
Nafikiri kukosa Kasi kwa wachezaji wa Simba sio mfumo wa benchikha isipokuwa ni aina ya wachezaji alionao ndio tatizo, anaweza kuwa Anataka mpira wa nguvu na Kasi Kama mataifa ya uarabuni yanavyocheza lakini anashindwa kufanikiwa kutokana na umri wa wachezaji alionao na fitness yao pia! Unapojenga mashambulizi yako taratibu unakuwa unampa faida mpinzani wako faida ya kuziba mashimo kwa haraka na kukuzia kirahisi sana kumfikia kwenye lango lake!
Nampongeza kocha wa singida alifanya home work yake vizuri kuisoma Simba na alifanikiwa pakubwa but umakini wa wachezaji wake na maamuzi ya refarii ndiyo yaliyomgharimu!
Kumbuka Simba kacheza michezo hii ya mapinduzi akiwa na kikosi chake chote Cha kwanza ivyo kinachoonekana uwanjani ndicho icho icho walichonacho kimbinu na kiufundi akuna Cha ziada! Benchikha anatakiwa afanye mabadiliko makubwa sana ya usajili kuondoa wachezaji mizigo na mafadher kwenye timu na kuleta wachezaji wenye Kasi na energy watakaoendana na mbinu zake vinginevyo kwa timu hii aliyonayo itamuharibia cv yake kabisa!
Aya tuliyasema kipindi kile kabla Simba aijakutana na yanga lakini tulibezwa matokeo yake mnara wa 5G ukasimama, Sasa tunawaambieni Tena rekebisheni timu yenu bado Iko unga aina ya mpira inaocheza na timu inazokutana nazo ni majanga yatakuja kuwapalia mbele ya safari alafu lawama aanze kutupiwa Tena mangungu na try again!
Unapokutana na timu inayokushambulia kwa Kasi muda wote na yenye fitness ya kutosha awawezi kukupa nafasi ya kumiliki mpira ata siku moja na lazima uchezee kichapo tu akuna namna na ndio ugonjwa sugu wa Simba hii!
MAPOVU NI RUKSA LAKINI UWEZI KWENDA PEPONI BILA KUFA KWANZA NA BILA KUIREKEBISHA TIMU YENU KUNA AIBU NYINGINE INANUKIA MBELE YA SAFARI!