Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,723
Ni jambo la kushukuru kwamba simba imeingia hatua inayofuata kwa msaada wa matokeo ya nyumbani baada ya kupata magoli mengi, lakini pamoja na ayo simba hii inayo mapungufu kibao kuanzia safu ya ulinzi na kiungo.
Endapo Red Arrows wangeongeza ubora wao angalau kidogo sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine, tatizo lililowaangusha red arrows ni ubutu wa safu yao ya ushambuliaji na beki zao za kati haziko makini pamoja na uzoefu pia imekuwa tatizo kwao.
Kwa upande wa simba shida kubwa ipo kwenye safu ya ulinzi wanakabia macho na mipira ya krosi imekuwa donda ndugu kwao. Pia kiungo cha Jonas Mkude na Kanuti kumekuwepo na shimo katikati yao kutokana na mkude kuwa taratibu Sana akipiga square pass nyingi na kanuti anacheza mpira wa taratibu Sana.
Watu hao 2 wakikutana na timu ambayo inacheza mpira wa kasi watalaumiwa bure, Simba rekebisheni makosa yenu mapema vinginevyo msije mkaanza kuwananga wachezaji kuwa wamewahujumu timu yenu bado Sana kiufundi na kibaya zaidi yamekuwa ni mapungufu ya kujirudia rudia ina maana kocha ajaona icho kitu au anasubili aibu tarehe 11🤣🤣🤣🤣