Simba kupokwa point za Ndanda?

Watani huwa hawana moyo kama wato.... Wao hupenda miteremko mno..... Ndio maana wamekuwa wakipata shida sana kunyanyua makwapa.....

Kwenye Kesi ya Hassan Kessy walikuwa wanashinda kwa waganga wakiomba YANGA ipokwe alama...
Juzi pia Rage amepigilia msumari zaidi kuhusu hassan kessy.
 
Wamesahau
Huko kwa Kessy kulikuwa na kanuni lakini eti hili halina kanuni. Maadam kuna ITC na leseni basi mambo ya work permit haiwahusu.
We have a long way to go!
Ukisoma Comments zao hapa... Utagundua kuwa huwa hawapendi kanuni ziwavute shati...
 
Mbona huko ulaya wachezaji hawaruhusiwi kucheza bila work permit? Tena hiki huwa kikwazo kikubwa!!!!

Kama kwenye kanuni zetu za usajili lipo, basi Ndanda wanaweza kupewa pointi ingawa hivi vilabu vikubwa vinalindwa sana na TFF.

Vv
 
Kama mliwatuma hao Ndanda endeleeni kusubiri.Hilo swala si la TFF, uhamiaji ndio wanahusika na mpaka sasa wao ndio wamechelewesha.Hakuna kanuni ya TFF ya kupoka timu point kwa swala lisilo wahusu.
 
Nasubiri Rage atoe maoni yake kuhusu hili. Ukimya wake utakuwa na maana moja tu.
 
Mfumo unaousema ni leseni ya kusajili haitolewi bila ya work permit. Ukishatoa leseni ni kwamba mchezaji yupo huru kucheza. Hamna kanuni itakayoweza kumzuia. Kama ipo itoe.
Kama unaongea kwa maslahi ya Simba, fikiri mara mbili; hoja yako inapingana na msimamo wa Simba hiyohiyo ilipokomalia uharamu wa Kessy kuiwakilisha Yanga kwenye Nane Bora za Kombe la CAF licha ya kwamba alikuwa na leseni ya CAF tayari! Mantiki ya hoja ya Simba ni kuwa leseni pekee haitoshi kumhalalisha mchezaji ikiwa taratibu nyengine hazijakamilika. Na ndio hoja anayojaribu kuijenga mtoa mada.
 
Jibu rahisi la swali lako ni Ulaya kanuni hiyo ipo husajili mchezaji mpaka awe na work permit. Hapa Bongo tunakurupuka tu. Hamna kanuni hiyo kwenye sheria zinazosimamia mpira nchini.
Falsafa ya kisheria ni kwamba Katiba (ya nchi) ndiyo Sheria Mama na kwa hivyo sheria yoyote inayopingana na Katiba ni batili. Kadhalika Sheria ndiyo mama wa kanuni na kwa hivyo kanuni yoyote inayopingana na sheria ni batili. Sheria ya ajira ni kwamba waajiriwa kutoka nchi nyengine ni lazima wawe na vibali vya kufanyia kazi nchini. Kwa hivyo wageni kufanya kazi bila ya kibali ni kukiuka kanuni yoyote iliyopo (hata kama kanuni yenyewe itakuwa imetoa uhalali au iko kimya kama hii ya Ligi) kwa kuwa inapingana na Sheria.
 
Mwenyekiti wa bodi ya ligi Hamad Yahya amelitolea ufafanuzi suala hili.Amesema hawawezi kumruhusu mchezaji ambaye hana leseni kucheza.Kuhusu kibali cha kazi amesema suala hilo ni la Uhamiaji. Na ndio ilikuwa hoja yangu. Maneno mengi ya kujifanya bush lawyer hayatasaidia lolote.
 
Nilisema kinachoanza ni ITC pamoja na leseni ndipo work permit hufuata.
Mapovu yalikuwa mengi sana. Bado tujuzwe kuhusu kanuni za TFF!
 
Tuseme Ndanda wamekurupuka hawajui kanuni hata kidogo
Kamati husika ije na majibu haraka kukata mzizi wa fitna
Kuhusu kukatwa point Simba usahau mkuu. Cha kuwashukuru ndanda ni kuitoa TFF usingizini, naamini wataongezea hicho kipengele cha work permit kwenye kanuni zao. Ishu ya wachezaji kucheza bila work permit kilikuwepo tangu enzi za FAT! Mfano tu Ngandu Ramadhani alicheza kienyeji na akaondoka kienyeji kina Mwinyi Rajab, Masudi Shabaan hata Wasso hao ni kwa uchache tu!
 
Kama unaongea kwa maslahi ya Simba, fikiri mara mbili; hoja yako inapingana na msimamo wa Simba hiyohiyo ilipokomalia uharamu wa Kessy kuiwakilisha Yanga kwenye Nane Bora za Kombe la CAF licha ya kwamba alikuwa na leseni ya CAF tayari! Mantiki ya hoja ya Simba ni kuwa leseni pekee haitoshi kumhalalisha mchezaji ikiwa taratibu nyengine hazijakamilika. Na ndio hoja anayojaribu kuijenga mtoa mada.
Acha kutumia akili ya mtoto mchanga kuandika.
Ishu ya kesi ni tofauti na hii!
Kesi amesajili yanga akiwa na mkataba na Simba, na amepewa leseni akiwa si mchezaji halali.
Agyei na kotei ni wachezaji halali wa Simba ila hawakuwa na vibali vya kazi.
Ndanda hawajaweka pingamizi la usajili kwa Simba.
Uwe unasukutua ubongo wako kabla ya kuchangia. Huo ni ushabiki mwiba!
 
Kuhusu kukatwa point Simba usahau mkuu. Cha kuwashukuru ndanda ni kuitoa TFF usingizini, naamini wataongezea hicho kipengele cha work permit kwenye kanuni zao. Ishu ya wachezaji kucheza bila work permit kilikuwepo tangu enzi za FAT! Mfano tu Ngandu Ramadhani alicheza kienyeji na akaondoka kienyeji kina Mwinyi Rajab, Masudi Shabaan hata Wasso hao ni kwa uchache tu!
Itabidi TFF waje na hiyo kanuni. Vinginevyo wanashiriki kuikosesha nchi mapato!
 
Itabidi TFF waje na hiyo kanuni. Vinginevyo wanashiriki kuikosesha nchi mapato!
Hakuna kanuni hiyo mkuu. We subiri kukuche utatute supu unywe. Achana na hii habari, ishakwisha. Ndanda wamesaidia tu kuizindua tu TFF kuweka hicho kipengele. Na jana Afisa wa uhamiaji ametoa ushauri hicho kipengele kiwekwe ili kufisukuma vilabu kushughulikia mapema.
 
WASISAHAU KUIPOKA YANGA POINT 24 WALIZOMCHEZESHA KESSY DURU LA KWA LIGI KUU!
BY 13BILLIONS PSPF

1482546668107.jpg
 
Back
Top Bottom