Simba kupokwa point za Ndanda?

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
Mnyama yupo hatarini kupokwa point kwenye mchezo wake na Ndanda baada ya kuwachezesha wachezaji wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini
Wanaweza kuwa na ITC na kupewa leseni na TFF lakini kibali cha kufanya kazi kinachotolewa na idara ya Uhamiaji ni kitu kingine
Tusubiri mtanange huo. Hats maelezo ya Kaburu yamejikita kwenye leseni. Bila kibali cha kufanya, leseni haitoshi
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500

Kanuni ipi hiyo?Imeanza lini?Wacha kufuata mkumbo. Nenda kasaidie wenzako kupiga magoti ili mishahara ilipwe. Wacha kukurupuka.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
Hapo wana kesi za uhamiaji wala si kesi za FIFA ama TFF.Hivyo kwa kuwa wana ITC tayari hakuna sheria yoyote ya kimichezo inayowazuia kucheza.
Ajira ya professional footballer ni kucheza mpira. Mambo yote ya TFF yapo subject ya kupata work permit!
TFF walisema hayo juzi kabla ya mechi za weekend. Ndiyo maana Zulu aliondolewa mechi ya Yanga.
Kama leseni ya TFF inatosha nani angetafuta work permit?
Tukubali wakubwa wameteleza
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Mfumo unaousema ni leseni ya kusajili haitolewi bila ya work permit. Ukishatoa leseni ni kwamba mchezaji yupo huru kucheza. Hamna kanuni itakayoweza kumzuia. Kama ipo itoe.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
Mfumo unaousema ni leseni ya kusajili haitolewi bila ya work permit. Ukishatoa leseni ni kwamba mchezaji yupo huru kucheza. Hamna kanuni itakayoweza kumzuia. Kama ipo itoe.
Zulu alikuwa na ITC pamoja na leseni lakini viongozi waliona asicheze kwa kuwa work permit ilikuwa bado.
Bado najiuliza swali hilo hilo. Work permit ya nini Kama mchezaji akiwa na ITC/leseni anaweza kucheza?
Itakuwa kinyume cha sheria za nchi kucheza kwa maana kufanya kazi bila kibali husika.
 
Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,070
2,000
Mnyama yupo hatarini kupokwa point kwenye mchezo wake na Ndanda baada ya kuwachezesha wachezaji wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini
Wanaweza kuwa na ITC na kupewa leseni na TFF lakini kibali cha kufanya kazi kinachotolewa na idara ya Uhamiaji ni kitu kingine
Tusubiri mtanange huo. Hats maelezo ya Kaburu yamejikita kwenye leseni. Bila kibali cha kufanya, leseni haitoshi
Hili suala sidhani kama ni la michezo, ni suala la jinai ambalo wahusika ni Idara ya Uhamiaji, ni sawa na lile suala na Ndanda Kosovo na wenzake ambao walishitakiwa na kuswekwa gerezani kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali hadi wakatunga ule wimbo 'Jela ni mbaya' na kujiita Wajelajela.

Kwenye soka, muhimu no ITC tu, na ndio maana wamepewa leseni na TFF baada ya kuridhika kuwa wamehamishwa kihalali kutoka timu zao walizochezea msimu uliopita,TFF hawahitaji kibali cha kufanua kazi nchi ili watoe leseni, hilo ni suala la sheria za nchi. Ni mtazamo Wangi tu.

Vv
 
bensog26

Senior Member
Feb 21, 2013
159
195
Zulu alikuwa na ITC pamoja na leseni lakini viongozi waliona asicheze kwa kuwa work permit ilikuwa bado.
Bado najiuliza swali hilo hilo. Work permit ya nini Kama mchezaji akiwa na ITC/leseni anaweza kucheza?
Itakuwa kinyume cha sheria za nchi kucheza kwa maana kufanya kazi bila kibali husika.
Work permit ndio tatizo hata ulaya inatokea unasajili mchezaji unakosa work permit na hachezi unampeleka kwa mkopo sehemu anayoweza pata work permit
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
Hili suala sidhani kama ni la michezo, ni suala la jinai ambalo wahusika ni Idara ya Uhamiaji, ni sawa na lile suala na Ndanda Kosovo na wenzake ambao walishitakiwa na kuswekwa gerezani kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali hadi wakatunga ule wimbo 'Jela ni mbaya' na kujiita Wajelajela.

Kwenye soka, muhimu no ITC tu, na ndio maana wamepewa leseni na TFF baada ya kuridhika kuwa wamehamishwa kihalali kutoka timu zao walizochezea msimu uliopita,TFF hawahitaji kibali cha kufanua kazi nchi ili watoe leseni, hilo ni suala la sheria za nchi. Ni mtazamo Wangi tu.

Vv
Mkuu, hivi unadhani nchi itairihusu TFF iruhusu wachezaji waingie uwanjani bila kufuata sheria za nchi ?
Ni wajibu was kila taasisi kuhakikisha wageni walioko chini yake wanatekeleza sheria za nchi! Kwa maana hiyo, lazima TFF wawe na kanuni za kizibana club kuhusu work permit kabla ya kuingia uwanjani
Ndiyo maana makocha hawakai benchi hadi wapate kibali cha kufanyakazi Tanzania.
Kabla ya Hapo wanakuwa na visa ya kitalii tu!
 
Mkuu, kama TFF wameweka hiyo kanuni ni sawa lkn usishangae ukikuta hiyo kanuni haipo maana hilo linahusika moja kwa moja na sheria za nchi.

Pia kumbuka kuwa soka ina taratibu zake ambazo sio lazima ziwe chini ya sheria za nchi.

Vv
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,649
2,000
Work permit ndio tatizo hata ulaya inatokea unasajili mchezaji unakosa work permit na hachezi unampeleka kwa mkopo sehemu anayoweza pata work permit
Kuna watu hawataki kukubali ukweli huo. Hay yamempata Farid was Azam kuichezea Tenerrife ya Spain!
Alipata kila kitu kasoro work permit!
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Kanuni hizo hazipo labda zitungwe sasa. Mchezaji akishapata leseni anaruhusiwa kucheza kwa kanuni za sasa hamna kipingamizi.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,757
2,000
Mnyama yupo hatarini kupokwa point kwenye mchezo wake na Ndanda baada ya kuwachezesha wachezaji wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini
Wanaweza kuwa na ITC na kupewa leseni na TFF lakini kibali cha kufanya kazi kinachotolewa na idara ya Uhamiaji ni kitu kingine
Tusubiri mtanange huo. Hats maelezo ya Kaburu yamejikita kwenye leseni. Bila kibali cha kufanya, leseni haitoshi
Muwe mnajifunza Sheria na Kanuni za Michezo ambazo zipo chini ya TFF na msitake kuyaleta ya Uingereza au huko Ulaya hapa Tanzania. Kanuni za TFF ili mchezaji wa Kigeni acheze mechi ya VPL ni mpaka awe na ITC tu na haisemi kuhusu Vibali vya kufanya Kazi hapa nchini kwani hiyo ni Kazi ya UHAMIAJI na siyo TFF na hata kama Klabu ya Simba itakutwa na hatia na UHAMIAJI ya kuwachezesha akina Daniel Agyei na James Kotei wote kutoka nchini Ghana bila kupatiwa working permit bado haitapokwa points zozote. Tuwe tunajikita sana katika kuzifuatilia Sheria na Kanuni za TFF ili siku nyingine tusije kuwa Watupu hivi kwa jambo jepesi tu kama hili.
 
avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
3,998
2,000
Ajira ya professional footballer ni kucheza mpira. Mambo yote ya TFF yapo subject ya kupata work permit!
TFF walisema hayo juzi kabla ya mechi za weekend. Ndiyo maana Zulu aliondolewa mechi ya Yanga.
Kama leseni ya TFF inatosha nani angetafuta work permit?
Tukubali wakubwa wameteleza
Acha mambo ya matamko weka sheria ya TFF tuone hicho kifungu.
 
MASIKITIKO

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
959
500
WASISAHA KUIPOKA YANGA POINT 24 WALIZOMCHEZESHA KESSY DURU LA KWA LIGI KUU!
BY 13BILLIONS PSPF
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom