Simba hana namna lazima ashinde kesho au sare ya 3-3 ndio asonge mbele

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,902
15,330
Simba kesho inabidi ashinde au vinginevyo atoe sare ya mabao 3-3 ndio aweze kufuzu kucheza nusu fainali.

Hii ni kwa mujibu wa sheria ya goli la ugenini kuhesabiwa mawili pale magoli yanapokuwa sawa baada ya mechi mbili kumalizika.
---

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya African Football league kuelekea mchezo wa kesho kati ya Al Ahly dhidi ya Simba lile bao la ugenini lipo.

Kanuni ya 15 kifungu kidogo cha tatu kimeondoa sintofahamu hiyo ikiweka wazi kwamba kwa mechi za hatua ya robo fainali, nusu fainali timu itakayokuwa na idadi kubwa ya mabao ya ugenini itafuzu hatua inayofuata.

Kanuni hiyo hiyo kipengele kinachofuata ikaeleza kuwa bao hilo la ugenini linatumika mpaka kwenye mchezo wa fainali ambapo timu yenye mabao mengi baada ya mechi ya pili itachukua ubingwa.

Kwa upande wa kanuni ya 16 kipengele cha kwanza nacho kimeeleza kuwa kuanzia hatua ya robo fainali endapo timu zote zitalingana kwa mabao ya kufunga na yale ya ugenini mechi hiyo itaamuliwa kwa mikwaju ya penalti.


Ufafanuzi huo unaifanya Simba kesho kuendelea kuupigania ushindi kwenye mchezo huo wa ugenini au sare ya mabao 3-3 na zaidi ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali.

Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 hapa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Ahly ambao ni mabingwa wa Afrika na kesho saa 11 jioni timu hizo zitamalizana kwa mchezo wa pili wamarudiano utakaopigwa Jijini Cairo nchini Misri.

Mwanaspoti
 
Simba Hawezi KUSHINDA.

ANATAKIWA APUNGUZWE TU IDADI YA MAGOLI YA KUFUNGWA.

Lwanga Alikuwa anaikoa sana Simba
Simba Haina No 6 kama Lwanga.

USHAURI kesho acheze na Viungo watatu kwa pamoja.

Kanute.
Mzamiru.
Ngoma.

Otherwise naona Goli 5
 
Simba kesho inabidi ashinde au vinginevyo atoe sare ya mabao 3-3 ndio aweze kufuzu kucheza nusu fainali.

Hii ni kwa mujibu wa sheria ya goli la ugenini kuhesabiwa mawili pale magoli yanapokuwa sawa baada ya mechi mbili kumalizika.

fuatilia soka sheria ya goli la ugenini halipo kwenye AFL
 
Y
Simba Hawezi KUSHINDA.

ANATAKIWA APUNGUZWE TU IDADI YA MAGOLI YA KUFUNGWA.

Lwanga Alikuwa anaikoa sana Simba
Simba Haina No 6 kama Lwanga.

USHAURI kesho acheze na Viungo watatu kwa pamoja.

Kanute.
Mzamiru.
Ngoma.

Otherwise naona Goli 5
Mwana Simba una hali gani?
 
Back
Top Bottom