kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,316
- 12,614
Simba imepata sare ya 2-2 na Al-Ahly kwa Mkapa na 1-1 Cairo kwenye AFL mwaka huu. Kwa muda mrefu Simba huwa inaishia Robo Fainali kwnye Mashindano ya CAF, na sasa wameishia hapohapo kwenye robo ya mashindano kwa kutolewa na Al-Ahly kwa kanuni ya bao la ugenini.
Wadau wa Simba wanadai kuwa wametolewa kiume na kutoka sare na Al-Ahly ni dalili kamili ya kukua kwa mpira wa Simba, lakini kuna wanaosema kuwa kukua kwa mpira wa Simba kungekuwa kuvuka hatua ya Robo Fainali, kucheza Fainali au kuleta Kikombe cha CAF nyumbani na sio kutoa sare na timu kubwa na kutolewa kwenye mashindano.
Kutoka sare na Al-Ahly, je, ni kweli mpira wa Simba umepanda au ni kushuka kiwango kwa Al-Ahly kuliko miaka iliyopita?