Simba bila meno atamtisha nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba bila meno atamtisha nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oba, May 6, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Siyo siri, nani aweza kimbia akifukuzwa na simba asiye na meno? au ni nani aweza kusikia, kuamini na kutekeleza vitisho vinavyotolewa na wana siasa wasiojali au kuheshimu sheria walizotunga wenyewe?
  Huwa nakareka sana ninaposikia watawala wakitoa maagizo na kutishia kuchukua hatua endapo hayatatekelezwa. Mfano 1. Marufuku kutengeneza na kutumia mifuko ya plastic 2. Marufuku kuvuta sigara kwenye kundi la watu 3. marufuku kutupa taka ovyo 4. marufuku gari la abiria kupita sheli kujaza mafuta na abiria ndani 5. marufuku marufuku........ Yametolewa mengi lakini ni lini waliokiuka hayo walichukuliwa hatua? au ni lini sheria au kanuni za bunge au mabaraza ya madiwani zilipotekelezwa tukaona?Ni lini sheria ya kutokujenga ndani ya mipaka ya barabara ilipotekelezwa, zaidi ya baba mwenye nyumba kugeuka na kula matapishi yake kwa kuwatetea wavunja hiyo sheria?Ni lini dereva na konda wa daladala walipofunguliwa mashtaka kwa kuwapitisha abiria wao sheli kujaza mafuta?au tunasubiri daladala moja ilipukie sheli na abiria wote ndo tuanze kubwabwaja kisiasa kama kawaida yetu? Inakera sana!
  Kuna faida gani kutunga sheria au kanuni ambazo huwezi ku enforce? wana siasa wanaboa kweli katika hilo!Ndiyo maana tumetengeneza kizazi cha vijana wabinafsi na mafisadi kwasababu sheria na kanuni zilizopo haziwezi kuwafanya lolote maana ndugu zao/baba zao/ wajomba zao/ family friend wao ni watawala watawakingia kifua, inauma sana.
  Nani aweza kuogopa sheria au kanuni isiyo na meno? Nani aweza kuogopa simba asiye na meno?
  Mawazo yangu tu, I stand to be corrected!
   
 2. Mrx

  Mrx Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikweli unayo sema na uko sawa kabisa ndugu yangu ila sisi watanzania ni vipofu hatuyaoni haya na ndio maana siku zote utumekuwa mstari wambele kushabikia yale tusiyoyajuwaaa na ndipo madhara yanapotukutaa.
   
Loading...