Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 948
- 806
Serikali imeanzisha mfumo wa point kwa madereva wanaovunja sheria za barabarani. Lengo ni rahisi: ukifanya makosa, unapunguziwa point; ukizidisha makosa, leseni yako iwe hatarini.
Lakini hii ni Bongo.
Badala ya kusema “tufuate sheria,” tayari tunasikia: “Tutagoma!”
Yaani tunataka barabara salama, lakini tusiguswe tunapovunja sheria. Tunataka foleni zipungue, lakini tuendelee kukatiza njia. Tunataka ajali zipungue, lakini dereva anayefanya makosa mara kwa mara asipoteze leseni. Tunataka nidhamu lakini kwa hiari!
Halafu anakuja mwanasiasa: “Madereva wanaonewa!”
Anakuja mwanaharakati: “Msikubali!”
Lakini nani anatetea abiria anayekufa kwa uzembe? Nani anatetea familia inayopoteza mzazi kwa dereva asiye na nidhamu? Nani anatetea maelfu ya watu wanaopoteza saa zao kwenye foleni kwa sababu kila mtu anataka kuendesha anavyotaka?
Kuna mentality ambazo hazibadilishwi kwa semina, mabango na “tafadhali.” Zinahitaji sheria yenye meno.
Kigali haikupata nidhamu kwa miujiza.
Singapore haikujengwa kwa kuwaambia watu, “ukijisikia, tafadhali fuata sheria.”
Nidhamu ya umma hujengwa kwa sheria zilizo wazi na enforcement isiyochagua mtu.
Tanzania haihitaji dictator wa kisiasa. Inahitaji dictatorship of the law.
Sheria iwe dictator kwa dereva, bodaboda, daladala, mwanasiasa, mwanaharakati, tajiri, maskini na hata polisi mwenyewe.
Point system iwe transparent, iwe na haki ya kukata rufaa, ushahidi wa makosa utumie teknolojia, na isiwe mradi mwingine wa rushwa. Lakini baada ya kuweka safeguards hizo, vunja sheria, poteza point. Rudia, poteza leseni.
Simple.
Maana Bongo tumefika mahali pa ajabu:
Hata sheria inayotaka kutuokoa na sisi wenyewe tunataka kuigomea!