Ni kweli kabisa mara nyingi ndo wako hivyo mimi kuna siku dada mmoja aliangusha pochi namwita dada kwa sauti amenikaushia hadi nikataja neno pochi ndo akastuka kaja mbio akaseama "asante sana kaka yangu huku ananikumbatia", nikamwambia usiwe na wasi wewe tanua tu, akazidi kunipamba baadae akazama akanipa za msimbazi mbili nikamuambia usijali imetoka wewe pesa yako tia mfukoni.
Akalazimisha hadi kunipa namba ya simu yake huku akiendelea kunipamba usikose kunipigia nikamjibu "ndio nitakupigia" tulivyoachana tu na namba yenyewe nikaitupilia mbali