Silaha za Laser: Marekani na mbio za silaha mpya za miale na mionzi (DEW) katika Karne ya 21

Sisi bado tunatafuta magaidi wa kubumba au tumeacha.

Mimi nashauri kwamba tuachane kabisa na somo la sayansi kwa sababu halina kabisa maana yoyote kwetu na tunawapotezea watoto wetu muda bure tu.

Sisi tunasoma hilo somo la sayansi ili iweje. Sayansi ni utafiti na sisi hata siku moja serikali haijawahi kutoa hata senti tano kuwekeza kwenye utafiti kwanza sisi hatuna kitu kinachoitwa utafiti.

Kwa nchi zilizoendelea sayansi wanasoma Block Study kama asilimia 10 tu na zingine 90 wako field watu wanafanya utafiti na matokeo yake ndio hayo tunayoyaona. Sisi tunawangisha watoto vichwa bure tu na sayansi ya maigizo.
Hukuona utafiti wa makinikia na uchafuzi wa mto Mara ?
 
Marekani wanayo Arrow 3 kwa kushirikiana na wayahudi, hii ni teknolojia ya kupoteza makombora hasa ya masafa marefu balltic,

Hata Turkey last year ameingia mkopo wa kuiweka hii tek ktkkulinda anga lake

Na Germany majuzi hapa walikuwa wanafikiria kuikopa hii tek ...ambayo kwa saa ina gharimu USD Trilioni 1
Hii inafanyaje kazi?
 
ICBM ambazo mataifa karibu yote makubwa yanazo zinasafiri kwa hizo Km 10,000 kwa saa.
Missile zinazosafiri haraka kuliko sauti, Za urusi zinasafiri hadi kilomita 10,000 kwa saa. Moscow mpaka london dk 15 tu inachukua.
 
Silaha za laser "Laser weapons" ndio silaha zinazotegemewa kuwa silaha za viwango vya juu zaidi duniani kuyasaidia majeshi dhidi ya makombora yote katika karne ya 21.

Silaha za laser ni silaha za aina gani?

Silaha za laser ni silaha zitakazokuwa zinatumia nguvu za miale ya laser kuharibu mifumo ya vifaa vya kijeshi kama maroketi, helicopters, ndege, rada, makombora n.k ishindwe kufanya kazi zake, kutembea au ishindwe kulipuka kama ilivyokusidwa kwenye target yake pale miale hiyo ya laser inapoelekezwa katika vifaa hivyo.

Hizi ni silaha mojawapo katika kundi la silaha zinazoitwa Directed Energy Weapons (DEW), nyingine ya silaha katika kundi hili zitakuwa ni za microwaves, particle beams na sound beams.

Jinsi gani silaha za laser zitabadilisha sanaa ya vita?
Ikiwa zitafanikiwa kwa kiwango kikubwa wale watakaokua wanazimiliki watapata faida kubwa katika vita kwa sababu watakuwa wana uwezo wa kuharibu ufanyaji kazi wa silaha, nyenzo na vifaa vingi muhimu vya kijeshi vya kisasa vinavyowasaidia wanajeshi katika mapambano, hii ina maana kitisho cha silaha kama za roketi na makombora kitapunguzwa sana na hivyo matokeo ya vita yataamuliwa zaidi na silaha za karibu kama bunduki na mapambano ya karibu ya moja kwa moja ya wanajeshi katika uwanja wa vita.

Nani anaongoza mbio za kuzipata silaha hizi?

Tangu mwaka 1999 Marekani walizitizama silaha za DEW kama teknolojia ya juu zaidi ya silaha katika karne ya 21 na Pentagon wakaanza kutengewa bajeti ya kufanya utafiti na kuanza kutengeneza silaha za aina hiyo za majaribio madogo madogo.

Baada ya majaribio madogo ya muda mrefu hatimaye Pentagon waliwapa kandarasi ya kutengeneza silaha kubwa makampuni mawili ya silaha ya Boeing na General Atomics Aeronautical Systems(GA-ASI). Majaribio ya kwanza ya silaha kubwa za kilowat 300 za laser yanatarajiwa kufanyika kuanzia mwaka 2022.

Matokeo yoyote ya majaribio hayo utakuwa mwanzo mwingine wa mchuano mkali wa mashindano ya silaha "arm race". Teknolojia inazidi kuwalipa walioamua kufikiri na kutazama mbele ya wakati siku zote.
Laser ipo siku nyingi tu kwenye vita, waturuki wapo mbele sana kwenye hii sector na tayari 2019 walishatumia laser kudondosha ndege ya China vita vya Libya


Video ya maonesho yao.

Hivyo si silaha mpya
 
ICBM ambazo mataifa karibu yote makubwa yanazo zinasafiri kwa hizo Km 10,000 kwa saa.
Hypersonic zinauwezo wa kubadili route ni maneuvarable compare na Balistic
1EF0FFBC-DAE1-4B30-A569-DC3364824B10_w408_r0_s.png

Ukiangalia hio picha inaonesha jinsi balistick zinavyotembea na ambavyo ni rahisi kuonekana na radar hata zikiwa mbali compare na hypersonic


Soma zaidi hapa tofauti ya hypersonic na Balistic

Pia ukisoma hio Article utaona marekani karequest kama trilioni 10 kwenye Budget kujenga defence ya Hypersonic na kudevelop hizo silaha.
 
Laser ipo siku nyingi tu kwenye vita, waturuki wapo mbele sana kwenye hii sector na tayari 2019 walishatumia laser kudondosha ndege ya China vita vya Libya


Video ya maonesho yao.

Hivyo si silaha mpya
 
Marekani tayari ina mfumo wa radar uliotapakaa dunia nzima. Wanazo radar kwenye manowari na meli zinazolizunguka taifa lao na zinazozunguka dunia nzima, zipo radar kwenye mataifa yote ya NATO ambayo yako karibu na Russia.

Hypersonic walizo nazo Russia ni Air to ground, ambazo inabaidi watumie ndege kuzirusha. Kwa taifa ambalo lina ulinzi mzuri wa anga huwezi kusogelea anga yao hata kupata hiyo nafasi ya kufany mambo yako.
Hypersonic zinauwezo wa kubadili route ni maneuvarable compare na Balistic
1EF0FFBC-DAE1-4B30-A569-DC3364824B10_w408_r0_s.png

Ukiangalia hio picha inaonesha jinsi balistick zinavyotembea na ambavyo ni rahisi kuonekana na radar hata zikiwa mbali compare na hypersonic


Soma zaidi hapa tofauti ya hypersonic na Balistic

Pia ukisoma hio Article utaona marekani karequest kama trilioni 10 kwenye Budget kujenga defence ya Hypersonic na kudevelop hizo silaha.
 
Hatuwezi kuwekeza kwenye vita,,
Hatuna adui wa kututisha sisi
Jibu rahisi tu. Nani kakuambia kwamba sayansi ni vita tu. Unafahamu hata kilimo ni sayansi na unafahamu kwamba Ukraine wanazalisha karibu tani milioni 100 za nafaka kwa mwaka, sasa jiulize sisi tunazalisha tani ngapi wakati tuna ardhi kubwa kuwazidi na hatuna Winter.
 
Back
Top Bottom