...sikwambii.....

...sikwambii.....

Amenishinda huyo mume, ndio maana nikakwachia.
Kazidisha ugumegume, kila chakula adandia.
Ya chumbani tena usiombe, hadi kanichefua.
Bora tumia wako ufundi, huenda mkaendana!
mpenzi wangu!lol!METISHAAAAAAAJE!
nakuandalia bonge la wanda la maana!
af unasemje we ni mbovu kiswahili!
yani umekoshaje sasa! Gaijin anapaswa akupe tuzo maridhawa hapa!
 
Last edited by a moderator:
Is that all you can say?
sikwambii tu jinsi inabidi utaraji usiyotaraji
amekaa kidigitally zaidi!
af The Boss fidia sadaka ulizofanya zipungue kanisani!una kesi na sisi ujue na unazidi kuharibu hapa! Kaunga mwaya huyu tumwandalie vifungu kipanda tu mimbarini ataje ya utoto!
 
Last edited by a moderator:
mpenzi wangu!lol!METISHAAAAAAAJE!
nakuandalia bonge la wanda la maana!
af unasemje we ni mbovu kiswahili!
yani umekoshaje sasa! Gaijin anapaswa akupe tuzo maridhawa hapa!

Najaribu mpenzi; unajua ukitiwa moyo (si kukatishwa tamaa na wajuvi) basi unapata nguvu na ujasiri wa kujaribu; knowing that kuna watu watakukosoa positively.

Mambo lkn, maana siku hizi na 'dip' tu jamvini.
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh.
Amemiss ibada ngapi vile?

sikwambii tu jinsi inabidi utaraji usiyotaraji
amekaa kidigitally zaidi!
af The Boss fidia sadaka ulizofanya zipungue kanisani!una kesi na sisi ujue na unazidi kuharibu hapa! Kaunga mwaya huyu tumwandalie vifungu kipanda tu mimbarini ataje ya utoto!
 
Last edited by a moderator:
Miaka 3 baadaye bado msimamo ni huo huo; ila kuna mambo nimetumwa nikwambie. And I will soon.....
 
Sikwambii jinsi ya kuwa mama wa kiafrika, kwani tayari wewe ni mama tena Mwafrika
Sikwambii jinsi ya kulea mwanao, kwani kila mtoto ni unique
Sikwambii jinsi ya kutunza nyumba yako, kwani sijui kilichopo nyumbani mwako
Sikwambii jinsi ya kuishi maisha yako kwani Mungu KAKUAMINI na kukukabidhi maisha yako.

Sikwambii jinsi ya kuishi na mumeo, kwani huyo si mume wangu
Sikwambii jinsi ya kumwandalia chakula, kwani sijui mapendeleo yake
Sikwambii jinsi ya kuwa naye faragha, kwani ni ya wawili ya faraghani
Sikwambii jinsi ya kuishi maisha yako, kwani Mungu KAKUAMINI na kukukabidhi maisha yako.

Sikwambii ukashop wapi, kwani sijui mahitaji yako
Sikwambii uanze na kipi, kwani sijui uwezo wala matamanio yako
Sikwambii wahitaji nini, kwani mimi si mmiliki wa maisha yako
Sikwambii uishi vipi, kwani Mungu KAKUAMINI na kukukabidhi maisha yako.

Sikwambii; sio kwasababu sitaki, bali kwakuwa SIJUI
Sikwambii; sio kwasababu mchoyo, bali kwakuwa sitaki KUKUPOTOSHA
Sikwambii; sio kwasababu sijali, bali kwakuwa si MNAFIKI
Sikwambii kwakuwa naamini UNAJUA kwani Mungu KAKUAMINI na kukukabidhi maisha yako.

.....Love you all and wishing you prosperity 2013 all the way to 3013.....


Sikwambi ushikwapo shikamana.
 
Back
Top Bottom