It is true that Mzee Mwinyi did not kill Arusha Declaration rather he abandoned every principle stated on Arusha Declaration!
LOL!! naona umetumia fatuma sasa!
Nilisema mnamwonea huyu naona umekubali!-Mtu pekee ambaye angelichukua AD na kubadilika na wangestahili hukumu ni Sokoine au Kawawa,
Wala hakujiangaisha kusoma na kukariri kanuni zenu, alichukua nchi na ku-assume ndiyo anaanza!! LOL!
Hivi nani ana clue kwa nini Kawawa hakuwa rais? baada ya JKN?
...
Sasa turudi katika kitabu cha Mtei. Katika ukurasa wa 149, yeye aliamua kuwaalika weledi wa IMF wakiongozwa na Bo Karlstrom ili washirikiane na weledi wa Wizara ya Fedha kubuni program ya kufufua uchumi. Anasema katika jopo lao, IMF walikuwa tayari kutoa mkopo wa kufufua uchumi lakini kwa masharti matatu. Mtei ameyaorodhesha hayo masharti kuwa ni; Mosi, kushusha thamani ya shilingi, pili, kuleta wawekezaji kutoka nje ya nchi, na tatu, serikali iache kusaidia kifedha mashirika ya umma na viwanda, na badala yake iyabinafsishe. Anatoa mfano wa benki ya taifa ya biashara NBC, kuwa ilikuwa ni kubwa mno iliyotishia usalama wake yenyewe.
Mtei alirudi kumueleza Bo Karlstrom kuwa Nyerere ameyakataa masharti. Bo Karlstrom akamwambia Mtei kuwa ebu niwezeshe nionane naye hana kwa hana nitamlainisha na atayakubali. Tarehe 29 November 1979 alimkutanisha na Nyerere Msasani. Baada ya maongezi, Nyerere alimwambia Mtei kuwa awaambie warudi zao Washington kwani yeye hawezi kuruhusu nchi yake iendeshwe kwa amri kutoka Washington (Washington consensus).
Hata wakubwa pia wanaweza kujifunza kutoka kwa wadogo.
Wadogo wenyewe ni hawa ambao wanaweza hata kuiba fedha kutoka kwenye benki kuu yao wenyewe kwa ajili tu ya kutafuta ushindi kwenye uchaguzi. Give me a break! Nani atakubali kujifunza kutoka kwa watu kama sisi - wizi mtupu!
Tukubali tu kwamba sisi vichwa vyetu vimejaa ugali na si ubongo na hatuwezi katu kuelewa lipi ni jema kwa manufaa ya umma. Tuko tayari kulibadili lile lililo jema kwa manufaa ya umma liwe 'jema' kwa manufaa binafsi ya viongozi na wateule wachache.
Mwalimu JKN kichwa chake kilijaa ubongo hakuna lolote ambalo limo kwenye Azimio la Arusha ambalo si valid leo katika nchi yetu hii yenye asilimia 80 ya watu maskini na iliyojaa wawekezaji feki wanaohujumu uchumi wa nchi. Kuna wenzetu wanaojidai wao ni wasomi lakini kuna mambo madogo sana ya muhimu katika maendeleo na ustawi wa jamii yetu yanawapiga chenga. Ningekuwa Rais wa nchi hii leo ningelirejesha Azimio la Arusha in full force - kwa manufaa ya umma!
Kinachotakiwa kwa serikali ni kusimamia majukumu yake ya kuongoza nchi ikiwa ni pamoja na uweka mazingira mazuri ya kustawi kwa uchumi wa nchi, hii ni kazi ya serikali. Kwa hiyo kazi ya serikali si kufanya UCHUUZI kama ilivyokuwa ikifanywa hapo awali. Hata huko umarekani serikali haifanyi UCHUUZI inahokifanya ni kutimiza wajibu kama msimamizi wa sera za ustawi wa uchumi.
Hapa Mzee Mkjj huna hoja ya nguvu, hivi sasa Tanzania kuna wafanyibiashara wa kuku wangapi ukilinganisha na wakati huo? Je, wanapata wapi vifaranga? Kampuni ya kuku haikuwa na umuhimu wowote wa kumilikiwa na serikali. Serikali ilitakiwa kuwekeza katika vituo vya utafiti wa kuku na wanyama wengine na sio kufanya biashara.
Vituo vya utafiti ndiyo vingetumika kutoa ushauri wa jinsi ya wafugaji wanaweza kuwekeza katika biashara ya kutotoa vifaranga, ubora wa chakula cha kuku, matibabu, nk. Resources muhimu ya kufanya mambo hayo zilipotezwa kwa kuanzisha na kuiendesha kampuni hiyo. Tukubali wazo halikuwa sahihi.
Kama nilivyoeleza kazi za serikali sikuchuuza bali ni kubuni na kusimamia utekelezajiwa sera za kustawisha uchumi ambazo wananchi watazituma/watafaidika nazo katika kujiletea maendeleo yao. Kwa hiyo katika issue ya GM/ Chrysler/mabenki serikali ya umarekani ilichokifanya kutimiza kazi yake ya usimamizi (regulator mkuu wa uchumi) na wala si vinginevyo.
Hali kama hiyo inaweza ikamkuta mtu yeyote yule anayefanya biashara pale ambapo biashara yake haiendi vizuri basi anaweza kuteuliwa maneja wa kuisimamia kampuni yako kwa maslahi ya wale wenye interest kwenye biashara yako kama vile wanahisa au wadogo au creditors.
Juu ya Fannie Mae na Fred Mac, haya makampuni yameanzishwa kwa malengo maalum na yana mfumo wa uendeshaji wa private mbali ya kwamba ni ya serikali.
Mfumo kama huo ndiyo ambao umeanzishwa Tanzania - TASAF ambapo in the long run iwe inajiendesha yenyewe kama partner wa jamii. Kwa hiyo makampuni ya Sallie Mae na Fannie Mae hayapo kwa malengo ya kufanya biashara.
Swali lako linajibika kwa swali hili
Nipe mfumo ambao serikali inafanya UCHUUZI karibu katika kila jambo kuanzia Viatu, Nguo, Vyakula, Kuku, Ng'ombe, Maziwa, list ni ndefu
Wewe ungeamua kugombea ubunge leo hii ningekunyima kura yangu.
Nchi ilikuwa na makampuni ya serikali takribani 400 na mengi yao yanategemea ruzuku ya serikali ambayo inatokana na pesa za walipa kodi wa nchi nyingine, wanaokupa hizo pesa za kulipa mishahara ya walimu na polisi wanakuambia kuwa hatuwezi kubeba mzigo wa hasara zinazopatikana katika makampuni yako, wewe utaendelea kuwaambia kuwa nipeni tu?
Busara unayoisema wewe ndiyo hiyo ambayo serikali ya Mwinyi na Mkapa iliifanya ya kuyarekebisha mashirika hayo kupitia Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma, ambapo yale yaliyokuwa mzigo na hayawezekani kurekebishwa yalipigwa chini ikiwemo Kampuni ya Kuku. Na mengine yaliuzwa. Na huo ndiyo ulikuwa uamuzi sahihi.
Kwa kumalizia serikali haitakiwi kufanya biashara isipokuwa inatakiwa kutengeneza mazingira muafaka kwa akina Ruge na Kusaga waweze kuwa wabunifu, Bakhresa na Gulam Dewji waweze kutumia uzoefu wao, Profesa J, Jide na Mwana FA waweze kutumia vipaji vyao, list ni ndefu inaendelea...
Wadogo wenyewe ni hawa ambao wanaweza hata kuiba fedha kutoka kwenye benki kuu yao wenyewe kwa ajili tu ya kutafuta ushindi kwenye uchaguzi. Give me a break! Nani atakubali kujifunza kutoka kwa watu kama sisi - wizi mtupu!
Tukubali tu kwamba sisi vichwa vyetu vimejaa ugali na si ubongo na hatuwezi katu kuelewa lipi ni jema kwa manufaa ya umma. Tuko tayari kulibadili lile lililo jema kwa manufaa ya umma liwe 'jema' kwa manufaa binafsi ya viongozi na wateule wachache.
Mwalimu JKN kichwa chake kilijaa ubongo hakuna lolote ambalo limo kwenye Azimio la Arusha ambalo si valid leo katika nchi yetu hii yenye asilimia 80 ya watu maskini na iliyojaa wawekezaji feki wanaohujumu uchumi wa nchi. Kuna wenzetu wanaojidai wao ni wasomi lakini kuna mambo madogo sana ya muhimu katika maendeleo na ustawi wa jamii yetu yanawapiga chenga. Ningekuwa Rais wa nchi hii leo ningelirejesha Azimio la Arusha in full force - kwa manufaa ya umma!
Utalirejesha in full force na kulitelekeza kwa namna gani, kama sheria?
Mzee Mwanakijiji;857634]Sijui kama unajua unalosema; serikali inamiliki kampuni ya Posta, inamiliki kampeni ya Reli (Amtrak), inamiliki kampuni ya Bima (FDIC), na ina miliki kampuni nyingine mbalimbali kama GM, Chrysler na hata kutoa fedha kuendesha mabenki binafsi yaliyoanzishwa na watu binafsi. Na siyo hivyo tu, kampuni imetaifisha mabenki kadhaa ambayo yalikuwa yanafeli na kuteua uongozi wake wa juu! Serikali ya marekani inafanya uchuuzi!
Sasa kwa nini serikali ifanye utafiti huo na siyo watu binafsi?
Sasa, bila taasisi ya mfano utatoa ushauri kutoka wapi? Serikali ina vyuo vya Kilimo vinavyofanya utafiti na humo humo kuna taasisi za mifano zinazoendeshwa kibiashara. Sasa unataka hata hilo lisiwepo? Huwezi kuindoa serikali moja kwa moja katika kufanya biashara iwe kwa sababu ya nature ya biashara yenyewe au sababu ya unyeti wake.
Ni wazi kwamba hujui Obama alichofanya; serikali ya Marekani imenunua hisa kwenye makampuni hayo, imesimamia uongozi wake na kuuteua, na licha ya kuwapa uhuru wote, bado GM na Chrysler zinasimamiwa kwa karibu na wamiliki wake (ambao mmoja wao ni serikali ya Marekani!). Serikali haikuishia kwenye usimamizi tu.
Hazina ya Marekani na ile ya Canada nao ni wamiliki; to remind you Marekani na Canada ni nchi za Kibepari!
Kwa hiyo serikali inaweza kumiliiki makampuni na kuyaendesha kibinafsi lakini chini pia ya usimamizi wa serikalki hiyo hiyo. Ni kampuni gani isiyoanzishwa kwa malengo maalum? Kuna tofauti gani kubwa kati ya Freddi, Mac na NHC au Benki ya Nyumba ya Tanzania?
Whaaat! yanafanya biashara tena biashara kubwa tu. Usidhanie yapo kwa ajili ya charity.
Sasa hili ndilo linajadilika; tulipoanza wakati wa Uhuru ni nani alikuwa na mtaji mkubwa wa kuwekeza katika sekta hizo zote isipokuwa kikundi cha watu wachache. Yaani, ulitaka kuanzia ardhi, miradi yote iishie kufanywa na kikundi cha watu wachache? Serikali ilichofanya kupitia AA ni kujaribu kutengeneza uwiano wa nafasi za kufanikiwa na kuwapa Watanzania ambao wengi wakati ule walikuwa hawana elimu ya kutosha nafasi ya kuweza kufanikiwa. Hata haya mafanikio ambayo tunayaona leo hii yametokana na nafasi hiyo iliyowekwa na Azimio.
Vinginevyo, leo tungekuwa na issues za ardhi kama za Zimbabwe (ambazo naamini kwa kadiri CCM inaendelea na sera yake mbovu tutafikia) ambapo kiasi kikubwa cha ardhi kiliwekwa mikononi mwa watu wachache huku ubepari ukitakiwa uendelee tu. Leo hii hata Afrika ya Kusini haijakubali kuuachilia ubepari ufanye upendavyo maana wanajua kabisa kwa kufanya hivyo waliokuwa nacho wataongezewa na wasio nacho wataendelea kuombea wawe nacho.
Bahati nzuri, sina fikra hizo hasa kama watu wenye kuwaongoza wana mawazo ya kwako; nisingethubutu kuomba kura kwako.
Hapana unatakiwa kutumia ubongo wako na kujiuliza "nifanye nini" kukimbilia kuuza tu ni woga usiio na msingi. Busara ilitakiwa watu wakae chini (kama walivyofanya wenzenu kwenye nchi tajiri) na kusema ni makampuni yapi tuyauze, makampuni gani tubadilishe modeli ya uendeshaji wake, makampuni gani tuyaconsolidate n.k Hatukufanya juhudi zozote za kuboresha au kuokoa mashirika yetu, kwa woga wa kina Mwinyi wakaamua kuweka manyanga chini.
Bahati mbaya hawakurekebisha mashirika walikubali tu kuwa ni bora kuyauza au kuyaacha yafe wakijua kuwa wao watapata nafasi ya kuyaanzisha au kuyanunua kwa bei chee. Hawakufanya juhudi ya kuyaokoa. Leo hii wameshindwa mara mbili sasa kwenye TRL na bado wanazungumzia "kutafuta mwekezaji" yaani katika vichwa vyoa wao wanaamini wawekezaji ndio watu pekee wenye uwezo wa kuendesha mashirika yetu. Hii siyo hekima ni upumbavu.
Umeshakubali hapo juu kuwa kuna wakati serikali inatakiwa kufanya biashara and as a matter of fact karibu dunia nzima serikali zinafanya biashara. Jambo la msingi ni jinsi gani, namna gani, na kwa modeli gani serikali naweza kufanya biashara gani. Huwezi kukwepa serikali kufanya biashara. Hakuna nchi yoyote duniani ambayo serikali yake haifanyi biashara kabisa.
Nafikiri unashindwa kuelewa nini lengo la serikali ya Marekani katika hayo makampuni uliyoyataja. Serikali inachokifanya ni ku regulate economy na wala si kuyandesha na kuyaikili mashirika hayo kama tulivyokuwa tunafanya sisi. Ni muhimu kuelewa hilo. Kilichotokea Marekani kinaweza kufanywa na Serikali yetu kunapotokea matatizo kama yalivyotokea Marekani lakini yote inategemea na uwezo wa kifedha wa serikali husika. Kwa mfano katika nyakati tofauti serikali imeweza kuingilia uendeshaji wa mabenki yaliyokuwa na matatizo kama vile GreenLand, Meriadian-Biao na ile bank ambayo ilibadilishwa kuwa Azania Bancorp. Uingiliaji wa shughuli hizo ni mahsusi kwa ajili ya kuprotect au regulate economy only na si uingiliaji wa kudumu
Serikali inawajibu wa kuaandaa mazingira mazuri ya kukua kwa uchumi ikiwemo ku-fund researches ambazo zitatumika katika kuendeleza biashara na mambo mengi yanayohusiana na sekta hiyo.
Ndiyo maana nilisema kuwa kama wewe utataka kuwa mwakilishi wangu kwa jambo kama vile mbunge sintokupa kura yangu kwa sababu mawazo yako ya kuwa na taasisi za mfano kama Kampuni ya Kuku siyakubali kwani hayana tija na yanatumia resources muhimu za walipa kodi ambazo zingekwenda kwa wanataaluma kufanya tafiti mbalimbali juu ya kuku.
The do it kwa sababu ni kazi ya serikali kusimamia policies zote iwe za uchumi, afya, viwanda, ulinzi, nk. Serikali ya Marekani inaweza kuchukua hatua hizo katika ku-regulate uchumi wa nchi yake kwa namna ambayo wanaweza, nayo kuwa na fedha ya kuweza kufanya hayo. Kama huna fedha huwezi kuiga wanayofanya Marekani, fedha yetu ya kufanya mambo kama hayo ndiyo hiyo tunategemea kulipana mishahara na kana kwamba haitoshi inabidi tupewe msaada wa kulipa mishahara hiyo kutoka kwa donors. Kwa mtaji huo huwezi kufanya yale ambayo nchi tajiri kama Marekani inayafanya.
Tofauti kubwa ni kwamba hayo makampuni ya Marekani yanaendeshwa kwa ufanisi wakati hayo ya kwetu yamekuwa yakiendeshwa bila ya ufanisi wa kuridhisha, hatimaye benki kama THB ikayeyuka na NHC kujikita kuwa shirika la Upangishaji Nyumba.
Primarily si mashirika ya kibiashara na ndiyo maana surplus zake zinakwenda kwenye foundation zinazozisimamia kwa ajili ya re-investment.
Samahani, mawazo yako hayaleti maana yeyote, unadhani kulima shamba la kijiji watu 100 ndiyo kupata tija? Uchumi unatufundishaje juu ya Marginal Returns and Marginal Cost? Nchi yetu ili iendelee kiuchumi na kuwa na uchumi imara tunahitaji wafanyibiashara wakubwa wachache tu na with time wafanyibiashara wadogo na wakati wangejijenga kutokana na mazingira mazuri ya kufanya biashara na shughuli zingine.
I don't believe serikali ilitakiwa kumiliki njia kuu za uchumi kwa maana ya kuzuia private participation katika nyanja hiyo. Haikuwa sahihi kwa serikali kuchukua mabenki, makampuni ya bima, na mengine kama hayo kwani hapo ndipo tulipoharibu.
Kama nilivyosema hapo awali serikali ilitakiwa kubuni mikakati ya kweli ya kustawisha uchumi lakini badala ilileta mikakati ambayo haikuwa sustainable na ndiyo maana leo hii tumerudi nyuma kuanza pale ambapo 1966/67 tulipochepukia.
Laiti kama serikali ingekuwa inaelewa kuwa uchumi ni muhimu kumilikiwa na wananchi hata kama ingechukua miaka 30 baada ya uhuru lakini tungestawi kwa kuwa wazalishaji zaidi na watanzania wengi wangekuwa wanashiriki katika kuendesha uchumi wa nchi yao leo hii.
Hayo mambo ya kusema kuwa tungekuwa na matatizo ni mambo ya kijinga na woga usiokuwa na maana kwa kukwepa kuwajibika katika mambo ya kweli na yenye manufaa kwa nchi na wananchi. Kujenga uchumi imara hakuna short cut.
Ni kweli maana ungejaribu tu usingepata kitu kwa maana ungezidi kuturudisha nyuma na hatimaye ukishindwa unaangukia kwenye rushwa kama short cut kujenga wealth badala ya kuweka sera makini za kukuza uchumi
Huhitaji kusema unatumia ubongo tu pia unaangalia facts zilizopo mbele yako. Serikali imekuwa ikiruzuku almost mashirika yote kwa gharama za walipa kodi na fedha za wafadhili. Wafadhili wanakuambia hatukupi tena pesa ya kufidia hasara ya mashirika yako, at the same time huna pesa ya kutosha ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali, kweli bado utang'ang'ana? Unless you dumb!!!!
Uamuzi wa kurekebisha mashirika haukuweza kuepukika kwani kwa namna yeyote ile mashirika mengine yalikuwa ni lazima yafe yanataka hayataki (wapi KAMATA? wapi NAFCO? wapi Kampuni ya Baiskeli NABCO? wapi Kampuni ya Vyombo vya Nyumbani HOSCO? Dartex? Natex? na utitiri wa makampuni ya kama hayo ambayo hayakuwa na ulazima wowote)
Si kupingi katika serikali kumiliki shirika kama la reli, lakini hata hivyo ni vema serikali ikaweka nafasi yake wazi katika mustakabali wa kudumu wa shirika kama hilo na ma mengineyo ya mawasiliano. Uzoefu duniani kote unaonesha kuwa Mashirika ya mawasiliano si muhimu tu kwa malengo ya kiuchumi pekee bali pia kiusalama.
Kwa hiyo serikali labda ingechukua upande wa kuwa na hisa nyingi si lazima majority na kutengeneza mgawanyo mwingine wa hisa nyingi kwa induvidual private owner na zinazobaki kwa public. Lakini hata hivyo hayo yote yanawezekana endapo tu mashirika hayo yatakuwa profitable kwani hisa zake zitauzwa kwa mujibu wa sheria.
That's how you think, lakini ninakurudisha nyuma kuwa serikali ndiyo msimamizi wa policies zote ziwe za uchumi, ulinzi, elimu, maji, kilimo, nk. Kwa hiyo serikali ina kazi zake nazo ni ku-regulate mambo haya. Sasa unapoona wana regulate uchumi ukatafsiri ni lazima wafanye biashara, basi huo ni mtazamo wako unahitaji mjadala mwingine.
Leo hii sijui hii nchi inaendeshwa na consensus ya nani tena.
Azimio la Arusha ilikuwa dira, kama vile ngazi ambayo mtu anaweka ukutani ili imwezeshe kufika paani. Katika msukosuko wa upepo, anakuja Mzungu, tena yuko paani, anakwambia itupe hiyo nganzi nitakutupia kamba alafu nikuvute. Ukiiangalia ngazi unaona imebuniwa na mswahili mwenzako na kamba imebuniwa na mzungu, tena yuko paani unapotaka kwenda. Unaitupilia mbali hiyo ngazi na kubakia kubembea kwenye kamba. Mzungu anavuta kidogo alafu anaiachia unadondoka puu!. Anakwambia kabla ujaishika tena kamba, nitupie hilo embe, unamtupia, nitupie Hindi la kuchoma, unamtupia na yeye anakula. Na hivi ndivyo wanavyotufanya. Nasi tunashangilia Hoyeeeee!
😎
Azimio la Arusha ilikuwa dira, kama vile ngazi ambayo mtu anaweka ukutani ili imwezeshe kufika paani. Katika msukosuko wa upepo, anakuja Mzungu, tena yuko paani, anakwambia itupe hiyo nganzi nitakutupia kamba alafu nikuvute. Ukiiangalia ngazi unaona imebuniwa na mswahili mwenzako na kamba imebuniwa na mzungu, tena yuko paani unapotaka kwenda. Unaitupilia mbali hiyo ngazi na kubakia kubembea kwenye kamba. Mzungu anavuta kidogo alafu anaiachia unadondoka puu!. Anakwambia kabla ujaishika tena kamba, nitupie hilo embe, unamtupia, nitupie Hindi la kuchoma, unamtupia na yeye anakula. Na hivi ndivyo wanavyotufanya. Nasi tunashangilia Hoyeeeee!
Anyway, Haya masharti ya IMF ambayo Bo Karlstrom alitaka kumuingiza mkenge Nyerere ni upuuzi mtupu. In fact, Rais Mwinyi aliyakubali yote na mengine ya ziada -kama cost-sharing katika elimu na afya. Walimpa dose ya kuvizika kabisa viwanda na mashirika ya umma, kuididimiza elimu na idara ya afya. Hiyo dose iliitwa SAPs - Structural Adjustment Programs.
!
😎
Lets then discuss in this way, lets assume Nyerere angeendelea mpaka 1995, na hakutaka kufuata mipango ya IMF au WB unafikiri nchi yetu ingeendelea kwa kiasi gani , na toa sababu ya jibu lako. You can take example in Kenya. Angalia nchi ilipokuwa at that time mwaka 1985 AND reflect hali hiyo mpaka 1995 tungekuwa mbele au nyuma kwa kiasi gani. any one may help on this