Mh sasa sijui zinahusika za wakati wa shule za msingitu?
Mi nakumbuka enzi zile TV maarufu ilitangaza mambo 3 (nayoyakumbuka) tena mtangazaji mwenyewe sasa hivi ni Mkuu wa Wilaya alitangaza:
1.
Oysterbay: Kutokana kuibuka kwa tabia ya vibaka kujikita maeneo ya Oysterbay na maeneo wanayoishi viongozi mbalimbali,wameamua mpango maalumu wa kuanza kufuga wanyama wa porini majumbani kwao ili kuimarisha ulinzi, wanyama hao ikiwa pamoja na Simba, chui nk( kipindi hiko sikuukuu ya wajinga ilikuwa ni kama haipo) , taarifa ikaendelea mpango maalumu ya wakuwapa mafunzomaalumu umeandaliwa na utaanzamara moja kudhibiti vinaka hao etc.
2.
Upimaji wa VVU Nymba kwa nyumba: Serekali imeanzisha mpango maalumu wa kupima VVU nyumba kwa nyumba na watakaopatikana watawekwa uwanja wa sabasaba uliotengwa maalumu kwa ajili hiyo...... na utalindwa masaa 24 na askari wenye bunduki...... jamani, nasikia mjeshi mmoja akasema na aje mtu hapa nyumbani kwangu kunipima kama sijamla shaba! Aidha mtoto mmoja so innocently akamuuliza mzazi wake kama atajificha asipimwe?,mweee!
3.
Kilimanjaro: Serekali ya ( nchi moja iliyoendelea) imejitolea kuongeza urefu Mlima Kilimanjaro kwa kuujenga kwenda juu ili uwe mlima mrefu zaidi ulimwenguni. Taarifa iliendelea , malori ya simenti. kokoto na michanga yameongozana kuelekea mlima Kilimanjaro kwa ajili ya ujenzi huo (nasikia watani zangu wakasema Yesu Ruwa hawa wazungu wanataka kutuletea majanga), hicho kitakachoongezwa si kitawaangukia?,kwani tangu wao wanazaliwa hawajahi sikia hiyo, wengine wakasema badala ya kuleta misaada ya kuwakwamua watu kiuchumi wanaleta balaa!
Baadae wakasema ni sikukuu ya wajinga, nahisi ilipigwa marufuku baadae maana sijasikia kwenye TV wakidanganya!???