Sikuhitaji . . . !!

Sikuhitaji . . . !!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Urafiki limekua ni jambo la hovyo sana siku hizi
'
Japokua dhana yenyewe ya urafiki sikubaliani nayo kabisa sina jinsi zaidi ya kukubali kuwa na marafiki kwa kuwa naishi dunia hihii ya watu wanaokubaliana na dhana hii
'
Tofauti na urafiki kuna kujuana,kujuana kuna karibu maana sawa na urafiki kwani huwezi kumfanyia jambo fulani mtu unaemjua
'
Kujuana au kufahamiana kwa mfano rahisi ni hapa JF.Wapo wasiojuana au wasiofahamiana kwa maana ya hawajawahi kuonana,au hana "umaarufu" wa kufanya watu wakujue hapa
'
Nikizungumzia mahusiano hayo yanayokaribia kufanana,nitazungumzia tafsiri mbovu na binafsi nisiyoipenda ambayo watu wanakua nayo hapa na mitaani tunamoishi
'
Urafiki na kujuana au kufahamiana watu wanaelewa kama kutokumkosoa au kutompinga mtu ambae una mahusiano ya aina hiyo
'
Hii ni tafsiri ya hovyo sana na siitaki.Unapounga mkono kila ninachosema hata kama ni jambo la hovyo nitajifunzaje?
'
Kama unaona nimepotoka mtu wa kwanza kuniambia ni wewe kama huwezi sitaki tujuane au urafiki na wewe
'
Kukukosoa ni kukufahamisha mtazamo tofauti na wako na wala sio ugomvi,kama hutaki kukosolewa tusijuane,kama hutaki kuniambia mtazamo wako ambao ni tofauti na wangu sitaki urafiki na wewe wala usinijue
'
Kutofautiana ni ishara ya kukua!
 
Heading imenitisha, nikatua talaka tayari nimepewa; thanks heavens it's not!
 
Bora yangu mm cna rafiki,every body is my friend,salamu nimemaliza!
 
Eiyer
::
Utakuwa mtu wa pekee sana.
::
Ni tabia ya mwanadamu kupenda wanaompongeza,,wanaomsifu na kuwashuku wote wanaompinga.
::
Adui wa karibu ni bora kuliko rafiki wa karibu ambae ni mnafiki
=
 
Last edited by a moderator:
Daaa umenena vema! Wengine wanaogopa kupingana kwa kuhofia kuvunja urafiki!
 
Usijali my waifu Kaunga nakupenda kama ugali na nswalu
'
Ila usiponikosoa nakumwaga . . Lol!
 
Last edited by a moderator:
Tetra ukweli wa ukweli ni muhimu sana katika maisha yetu
'
Lakini ukweli wa uongo ndo mzuri zaidi
'
Watu hawajui kutofautisha kati ya ugomvi na kuambiwa ukweli
'
Siku moja nilikua naangalia mpira mahali,akaingia jamaa mmoja na simu anasikiliza muziki kwa sauti ya juu sana,nikamuambia kuwa anatupigia kelele!
'
Jamaa alikuja juu na kuanza kutoa maneno ya ajabu kuwa nimemtusi,kwa kweli mpaka leo sijui nilimtusi wapi
'
Binadamu wengi hatupendi kuambiwa ukweli,tunataka tudanganywe,jambo ambalo siliafiki!
 
Last edited by a moderator:
Eiyer umegusa kitu wengi hawapendi.
But for me always i play with the points
 
Last edited by a moderator:
Eiyer umegusa kitu wengi hawapendi.
But for me always i play with the points

Kama tunataka tujifunze ni lazima tukubali kuwa kuna wakati tunafanya madudu!
 
Last edited by a moderator:
Sasa mdogo wangu, unapokomalia unataka ukosolewe! Ina maana unajua kabisa unakosea ila basi tu?
Usijali my waifu Kaunga nakupenda kama ugali na nswalu
'
Ila usiponikosoa nakumwaga . . Lol!
 
Last edited by a moderator:
Sasa mdogo wangu, unapokomalia unataka ukosolewe! Ina maana unajua kabisa unakosea ila basi tu?

Kujiaminisha kuwa hukosei ni tatizo tena kubwa.Hakuna binadamu asiekosea,kama hukosei wewe sio binadamu.Kujikubali na kujua wewe ni nani ni ishara ya kupunguza makosa,kujifungia ndani ya kiberiti na kuamini hukosei au unakosea kwa kiwango fulani ni ishara ya udhaifu mkubwa!
 
Back
Top Bottom