Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
baada ya kumaliza kozi ya ualimu, nikapata kazi ya kufundisha tuition mtaani kwetu nyumbani kwa mwanajeshi mmoja mkuria mkorofi sana nikafanya kazi yangu kwa uadilifu mkubwa mno, lakini bwana shetani huyu mbaya sana, pale ndani alikuwepo binti mkubwa tu ndugu wa mwenye nyumba tukaanza mahusiano ya siri sana, siku moja baba na mama wakaenda harusini mimi nikapata mwanya wa kurudi pale hm, nikanyata mpaka chumbani kwa binti, tukaanza yetu bila kulock mlango ila tukiwa tumezima taa, ni katikati ya mhemko nikahisi nafinywa mgongoni kuangalia ni mtoto mdogo wa pale ndani, nikastuka mno nikasepa kimyakimya nikijua dogo hajanitambua zilipita siku kadha ndio likatokea hili, nikiwa nawafundisha watoto kwa bidii na wazazi wako sitting room yule dogo akaropoka 'baba leo nimemkumbuka aliyemlalia dada siku ile, ni yule pale ticha' kwanza kilipita kimya kikuu nikahisi ganzi kisha joto kali halafu jasho mpaka kwenye meno na kiu kali mno sikujua nafanya nini ila nilijikuta natimua mbio na kutokomea !!!