LOVE STORY: That Guy

Just Nana

JF-Expert Member
Jul 27, 2023
500
1,001
Note; hii Ni story ya kweli kabisa imemkuta one of my close friends, nilimuomba kuipost kwa ahadi ya kuficha utambulisho wake na ameruhusu, kuna la kujifunza hapa. Twende kazi.

Naitwa Bella (sio jina halisi), nikiri kua muumba amenipendelea sana, ni mzuri wa umbo na sura na pia nimetoka familia bora mnooo, nimesoma shule bora tena nje, miaka kadhaa nyuma hapa Tanzania hapakua na hizi English mediums schools kwaio ili mtoto wako apate elimu bora ilikulazimu umpeleke Kenya au South, the best option kwa wazazi wengi wa kitanzania ilikua Kenya, nami niliangukia huko.

Nilisoma primary na secondary Kenya, nikaja Tanzania kufanya degree yangu ya kwanza, nikaenda south Africa for Masters degree , nikapata kazi kwa NGO moja pale South ambayo niliipata kipindi naandika dissertation kwa ajili ya kumaliza Masters yangu.

Nikiri tu life was good, support ya nyumbani ilikua kubwa sana, namshukuru babangu mpenzi alipambana nami ili nifikie malengo yangu, my mom ni wale kinamama wanaopenda amuone binti ake karibu mda wote, yaani ikifika mda wa kusafiri mama hadi analia kabisa, baba hakua na shida wala, pambana unavyoweza nitakusapoti popote ulipo.

Mkasa wangu unaanzia niliporudi Tanzania baada ya graduation ya Masters, niliugua ghafla homa kali mno iliyopelekea kulazwa hospitali moja kubwa tu hapa jijini, nilikua pale kwa takribani siku tatu hivi, mmoja wa madaktari walionihudumia anaitwa Karim (sio jina halisi), alinipa upendo mkubwa sana, si Kama wengine hawakutoa ushirikiano hapana, ila niliona Karim went extra mile, alikua anahakikisha nimepata huduma stahiki, nimekula, nimeoga , nimekunywa dawa kwa wakati, nimechomwa sindano zangu kwa wakati hadi mama akawa ananiuliza kwani huyu nani , huwezi amini huduma zote hizo na hata namba hakuomba daahhhh.

Siku naruhusiwa hospitali Karimu was off duty, aisee , nilikua naomba tu daktari aseme bado sijapona niendelee kubaki niwe namuona Karim, kwa sababu hospitali sio lodge wala hotel, we had to go, tukakusanya virago vyetu hao nyumbani. Sikua na makazi yangu binafsi hapa dar kwaio nikija likizo nilikua nafikia nyumbani.

Zilipita siku kadhaa za kulazimishwa kupumzika wee, kula kulala kurudisha afya, kuboreka kama kote, hiyo siku meamka nikasema hapana acha nikazurure, huyu mama akinuna atajua yeye. Nikampigia mdogo angu wa kiume by then alikua anasoma chuo hapa hapa dar, nikamwambia leo nataka kuzurura nahitaji kampan yake, ila tunaanzia hospitali, dogo akauliza unaumwa tena au? si umetoka huko juzi tu hapa, nikamwambia kuna mtu naenda kumcheck, just drop me please!

Ilikua Kama zari tu maana Ile tunawasili mapokezi na dokta Karim was signing off, nikamkimbilia Kama kichaa, dokta dokta, yaani ni kama ananikumbuka halafu hanikumbuki daaah, nikamkumbusha pale nilikua mgonjwa wake nikamtajia scenario, doooh , kumbe haikua exception bhana, ule ni utaratibu wake jinsi anahandle wagonjwa wake ni vile mi nilikua V.I.P room nikaona labda ni special treatment.

Nikiri tu niliumia sana,nikaona Kama najichoresha, nadhani alijua hilo, to save me from embarrassment ikabidi anitoe pale maana pale macho ya watu yalikua mengi, manesi si unajua walivyo wambea. Mdogo angu akawa anachek kama haelewi ivi, akanifata sister vipi, nikamwambia usijali it's some kind of miss understanding tu usiwaze. Karim akatuomba tumjoin lunch, tukatoka pale hadi canteen ya ile hospitali, hapo uso upo chini yaani daaah, mbona nimejichoresha ivi, mi nilijua ananihudumia vile labda amenipenda kumbe ndio jinsi anafanya kazi zake, yaani hata hanikumbuki pamoja na kujielezea vile daah.
 
SEHEMU YA PILI

Tukiwa pale canteen ilibidi tu Karim aokoe jahazi, aliona jinsi nimekua down , akaanza kutupigisha story mbili tatu just to know me, kimoyoni nikajisemea nikitoka hapa hatokaa anione tena walahi, sio kwa hii aibu ya leo kumshobokea mtu halafu hata hakukumbuki.

Ila ile situation niliona jinsi imemkata dogo, si unajua watoto wa kiume ,alikua anajikaza tu ni vile ananiheshimu ila nadhani angenitia makofi, maana nimemchoresha kumwambia kuna mtu namchek halafu mtu mwenyewe mwanaume na tena hata hanikumbuki, dogo alikua amenuna balaa. Nikaona hapa nikizubaa hata namba sitoombwa , ikabidi nimwambie dogo naomba kanichukulie pochi yangu kwa gari kuna research pepa natakiwa nimkabidhi daktari for recommendations , sijui alijua nampanga au niaje, ila dogo akanielewa akaenda kunichukulia , na dokta nae akawa kama ameelewa ivi intention yangu akatumia huo mda kuniomba namba , dogo alipoleta pochi nikazuga kutafuta iyo report baadae nikamwambia itakua nimeisahau nyumbani, nikamwambia dokta nitakupigia nikuletee , ni muhimu sana, tukaachana na dokta tukasepa na dogo.

Ili nisiendelee kumkwanza dogo ikabidi nimwambie achague yeye tunaelekea wapi , akachagua City Mall, dogo anajua kua napenda sana movie , tukaanzia pale , kisha samaki samaki , jioni mida ya saa tatu tukarudi nyumbani. Mama Kama kawaida yake, anaanzia kuongea chumbani anaingia jikoni anaenda sebuleni anaongeaga tuuu, ila wamama jamani, daaah....kisa tumerudi saa tatu usiku , angejua South saa tatu ndio pamekucha daaah.

Nilisubiria simu ya Karim kama vile nasubiria taarifa ya kua visa yako ya kwenda kwa Malkia imekua approved daah....Masaa yalikata ila yule kaka hakupiga simu jamani, nikawa najishangaa ivi Bella Mimi ndio wa kukaa nachungulia simu utafikiri nasubiria email ya tenda daaah, mapenzi nyoko.

Wiki zilikatika, likizo yangu nayo ilikua inakaribia kuisha, ilibidi nikubali tu matokeo . Siku tatu kabla ya safari ,nipo na mama supermarket si nikamuona Karim, mama akanambia Bella yule sio dokta Karim, nilishtuka, Ni kama nimeona nyoka sijui, mama akanambia una nini wewe? ikabidi nizuge hamna kitu mama, Kuna mdudu amenigusa, daah ....

Yule kiumbe kumbe alituona pia, akawa anakuja upande wetu, alipofika akaniita Bella huku anatabasamu daaah, akatusalimia pale na mama, mi nikawa nazuga kua nipo bize naongea na simu, yaani sikupenda zile dharau ameniletea, tatzo mama akawa anaongea nae wanacheka ,nipo kiruuu, ni nini hii,huyu mama jamani afanye tuondoke, nikiangalia list ya vitu vya kununua bado ndefu na list anayo mama ikabidi niwe mpole tuuu.
 
SEHEMU YA PILI

Tukiwa pale canteen ilibidi tu Karim aokoe jahazi, aliona jinsi nimekua down , akaanza kutupigisha story mbili tatu just to know me, kimoyoni nikajisemea nikitoka hapa hatokaa anione tena walahi, sio kwa hii aibu ya leo kumshobokea mtu halafu hata hakukumbuki.

Ila ile situation niliona jinsi imemkata dogo, si unajua watoto wa kiume ,alikua anajikaza tu ni vile ananiheshimu ila nadhani angenitia makofi, maana nimemchoresha kumwambia kuna mtu namchek halafu mtu mwenyewe mwanaume na tena hata hanikumbuki, dogo alikua amenuna balaa. Nikaona hapa nikizubaa hata namba sitoombwa , ikabidi nimwambie dogo naomba kanichukulie pochi yangu kwa gari kuna research pepa natakiwa nimkabidhi daktari for recommendations , sijui alijua nampanga au niaje, ila dogo akanielewa akaenda kunichukulia , na dokta nae akawa kama ameelewa ivi intention yangu akatumia huo mda kuniomba namba , dogo alipoleta pochi nikazuga kutafuta iyo report baadae nikamwambia itakua nimeisahau nyumbani, nikamwambia dokta nitakupigia nikuletee , ni muhimu sana, tukaachana na dokta tukasepa na dogo.

Ili nisiendelee kumkwanza dogo ikabidi nimwambie achague yeye tunaelekea wapi , akachagua City Mall, dogo anajua kua napenda sana movie , tukaanzia pale , kisha samaki samaki , jioni mida ya saa tatu tukarudi nyumbani. Mama Kama kawaida yake, anaanzia kuongea chumbani anaingia jikoni anaenda sebuleni anaongeaga tuuu, ila wamama jamani, daaah....kisa tumerudi saa tatu usiku , angejua South saa tatu ndio pamekucha daaah.

Nilisubiria simu ya Karim kama vile nasubiria taarifa ya kua visa yako ya kwenda kwa Malkia imekua approved daah....Masaa yalikata ila yule kaka hakupiga simu jamani, nikawa najishangaa ivi Bella Mimi ndio wa kukaa nachungulia simu utafikiri nasubiria email ya tenda daaah, mapenzi nyoko.

Wiki zilikatika, likizo yangu nayo ilikua inakaribia kuisha, ilibidi nikubali tu matokeo . Siku tatu kabla ya safari ,nipo na mama supermarket si nikamuona Karim, mama akanambia Bella yule sio dokta Karim, nilishtuka, Ni kama nimeona nyoka sijui, mama akanambia una nini wewe? ikabidi nizuge hamna kitu mama, Kuna mdudu amenigusa, daah ....

Yule kiumbe kumbe alituona pia, akawa anakuja upande wetu, alipofika akaniita Bella huku anatabasamu daaah, akatusalimia pale na mama, mi nikawa nazuga kua nipo bize naongea na simu, yaani sikupenda zile dharau ameniletea, tatzo mama akawa anaongea nae wanacheka ,nipo kiruuu, ni nini hii,huyu mama jamani afanye tuondoke, nikiangalia list ya vitu vya kununua bado ndefu na list anayo mama ikabidi niwe mpole tuuu.
Kumbe mnapatikanaga na nyie....
 
SEHEMU YA TATU

Saa nne usiku baada ya kutoka supermarket, tulikua tunachek movie na madogo home, Karim akapiga simu, nilinyanyua simu kivivu maana nikiwa nachek movie sipendagi usumbufu, kucheki jina Karim...yaani ni Kama shoti hivi ilipiga kwa moyo, nilipaniki.... dogo akaniuliza sister uko poa, nikamwambia yaaap, nikanyanyuka nikaingia room kwangu, ilibidi nifunge mlango kabisa maana niliona kama muujiza.

Zile hekaheka za maandalizi ya kupokea simu, si ikakata bwana, ikabidi nimpigie kumbe salio sina daaah....nikaanza process za kununua salio toka kwa account yangu ya benki, yaani mara nikosee password mara badala ya kuconfirm nacancel. Nikaona kununua nachelewa , nikaenda kumuomba dogo simu yake nimpigie yule bwana mapozi, simu iliiiita ikakata, sijui aliona namba ngeni...nikaona siwezi kuteseka mimi, nikapiga video call watsaap... Iliita hadi ikakata, nikasema dooooh, Kuna watu wanajua kuringa jamani

Sikumbuki nililala mda gani, ila nikiri tu ile ilikua siku ya kwanza kwa yule mwanaume kunitoa machozi, nilipoamka ilibidi nivue nguo zote nisimame kwa kioo, labda kuumwa kumenifanya nimefubaa au? nikiwaza list ya madon wa SA wanavyonifukuzia, who the hell is Karim, nilipiga ukuta ngumi nikaishia kuumia tuuu, nikaingia bafuni nikafungua shower ili nimalizie machozi yangu vizuri...hua maumivu yangu nayamaliziaga bafuni , na siku Ile niliiadhibu kweli Ile shower maana I cried over hours, isingekua mama kuja kuniamsha for breakfast na kukuta mlango umefungwa sijui Kama nilikua natoka bafuni Karim kaniweza walahi , kaniweza.


Ilitokea hekaheka Ile palivyokucha, mi nilikua bafuni na shower iko on kwaio sikua nasikia chochote , waligonga wakachoka, wakapiga simu wakachoka, mama akashauri utafutwe ufunguo wa ziada wa kuingia room kwangu. Mama ilibidi aingie yeye kwanza maana mi ni binti pekee nyumbani, ukitoa dada wa kazi waliobaki ni wanaume. Mama akakuta kitanda kitupu ila simu yangu ipo hapo kitandani, akatupa macho mlango wa bafuni akaona michirizi ya maji maana ni mlango wa kioo, ikabidi awaambie kua yupo anaoga, madogo wakatawanyika maana walijaa wote mlangoni, kilichowapa hofu ni Ile picha ya jana usiku ya kuhangaika kumpigia mtu asiepokea , kwa hiyo walikua wana haki ya kuhofia.

Mama akaniacha niendelee kuoga ,lakini kilichomshangaza ni mda kuzidi kukatika, akamtuma dada akanigongee kua chai tayari, dada akaja kugonga alipoona siitikii akaingia ndani, alikuta mazingira yaleyale na aliyoyaacha mama, akarudi kumpa jibu kua bado anaoga. Mama akaona hii haipo sawa, akaja hadi bafuni akaniita, Bella, kimya , akaita tena kimya, akaamua kusukuma mlango wa bafuni, bahati nzuri sikua meufunga kwa ndani, akanikuta mekaa chini nalia, shower bado inatiririsha maji, na nilikua nalia huku natetemeka kwa baridi ikimaanisha kua nimekaa kwenye maji mda mrefu sana.
 
SEHEMU YA NNE;


Kwa msaada wa mama nikatoka bafuni, akanipa nguo za kuvaa akaenda kunifatia chai akaniletea chumbani...ukubwa dawa , mama akajua tu hapa pana namna, hakutaka kuniuliza sana, akanambia tu nijiandae tutoke wawili, amemisi kukaa na mimi sehemu tulivu.

Mama alikua dereva ile siku, alijitahidi kuniongelesha ili niwe okay, nilijitahidi kua sawa maana mama angu ni dakika mbili mbele, ukizingua makofi, alishawahi kunambia nitakutandika makofi hata mbele ya mme wako, hua sipendi ujinga...kwaio nakuaga nae kwa machale sana. Tulifika Bagamoyo mchana wa kama saa nane ivi, mama alimpigia mzee kua tutalala Bagamoyo nipo na Bella, 'we need some girls quality time...'baba akasema haina shida mkikwama mtanambia.

Tulipata msosi safi pale, sea food za kutosha , nilizimiss walahi, angalau nikawa naanza kua poa, mama akaniuliza kama ningependa kuogelea nikamwambia hapana labda tukae tu ufukweni tupunge upepo. Akaanzia mbali yule mwanamke ila mwisho wa siku ikabidi tu nimwambie ukweli kua nampenda sana Karim na naona Kama haoneshi nia...mama akaniuliza sasa mwanangu mwenzio anajua Kama unampenda? Nikamjibu hatujawahi ongea ila hisia hazifichi mama, mama akaniuliza unajua lolote kuhusu Karimu? Nikamwambia hapana maana hajanipa muda wa kumfahamu...mama akanambia sasa mrembo wangu, unataka kunisononesha na kujitoa roho kwa mtu ambae hata hajui Kama unampenda? Nikamwambia mama Karim anajua ananifanyia tu makusudi, akaniuliza umewahi hata kumtumia ujumbe kua unahitaji uonane nae, some guys are shy baby girl...hebu jaribu kumuweka karibu, mtext maana watsaap haiongopi, akiendelea kukuignore then sio fungu lako...nikamwambia mama nitafanya hivyo, lilifata somo la mahusiano pale kama lote, unaweza kujaza counter book quire one dahhh...thank you mom!
 
NA HII NI NAMBA TANO;

Siku moja kabla ya safari nilijipa ujasiri wa kumtext bwana Karimu...niliandika nikafuta, niliandika nikafuta, ilibidi niandike nikiwa nimezima data ili asije akawa online akaona jinsi natumia nusu saa kuandika single text, finally nikapata cha kuandika ...

'Karim ... nimekutana na wewe katika ugonjwa ila nadhani natakiwa kushukuru kua niliugua, zilikua ni siku tatu njema katika maisha ya usichana wangu...one of my best days...sina mda zaidi maana kesho nasafiri kurudi SA...ila ningependa japo niione sura yako, najua upo na mambo mengi lakini naomba uzingatie ombi langu, nina mengi ya kuongea nawe, zaidi, nikutakie kila lenye kheri katika majukumu yako, am flying tomorrow...pease see me !

Nilihakiki ule ujumbe kama mara tatu hivi, mara niweke koma mara nitoe , ili mradi tafrani...mwisho nikaona huu ufala, nikawasha data nikautuma... I prayed for blue tick, nilijisumbua tu bure kuzima data, that guy alikua off line daah....

Sikua na namna nilifanya maandalizi yangu ya mwisho ya safari, usiku tukalala, alfajiri na mapema nikawa zangu airport mimi na familia kwa ajili ya safari ya kurudi SA. Mara zote hua nakua nafuraha ikifika mda wa kusafiri maana kukaa nyumba moja na mama angu yahitaji uwe na degree ya uvumilivu, ila leo ni kama nilikua naomba ndege ipate hitilafu nisisafiri daaah...

Sijui hata ilikuaje nikasema niangalie watsaap kwa mara ya mwisho kabla sijangia ndani ya uwanja, lahaula...nikakuta nimejibiwa jamani doooh...akaniuliza unaondoka na ndege ya saa ngapi? nilianza kuhaha pale, maana nilikua nimechelewa dakika kadhaa, I had to check inn, na wakati huohuo nataka kuchart na Karim, nikasema acha nifanye pata potea tuu, nikamtext chap, nipo Airport time hii, naondoka soon...nitakuchek nikifika SA...

Nikawaaga familia, sijui hata niliipata wapi nguvu, nikabeba mizigo yangu nikaingia ndani chap, nikachek inn na kupanda kwa ndege, I landed at O.R Tambo Int. Airport safely that day, baada ya kutulia na kumalizana na familia ilibidi nimchek Karim kua nimefika niko poa na mambo zingine... we had several conversations and yes I had to say the words , kijana unanimaliza...I confessed my feelings to him, alichonijibu ni kua anajua tangu nimemfata hospitali na dogo kua niko na feelings kwake, ila as a man hakutaka kuniumiza, ana mchumba na anamuheshimu sana.

Yaani tu kwa kifupi, mwanaume niliempenda like crazy was someone's else's fiancee...aisee ,lile jibu ni kama kisu kilikata hivi, akaniuliza are you there Bella, hata sikujibu nikatoka online...days went by, hio siku nikaona ni ujinga tu maana nilikua memblock baada ya kunijibu vile , nikamtoa kwa block nikamtumia text chache kua nitakua a secret lover, naomba nipe nafasi, I love you madly, nipe tu nafasi nikiona nimeshindwa nitaacha mwenyewe.

Sio Kama sikua na boyfriend , I had a guy from France alikua akiitwa Leon ( si jina halisi) , yule kaka alikua ananipenda sana, nilishatambulishwa hadi kwao, ilibaki kwa Leon kuja kwetu, hadi dakika hiyo Leon sikua nimeonana nae, nina wiki SA lakini namkwepa , kila akinichek namkwepa, Leon is very understanding, nilimwambia tu nipo biz nabanwa na mambo ya kazi , si anajua nimetoka likizo wala hakua na shida.

Baada ya kumsumbua sana Karim akanambia okey, unatakaje Bella? nikamwambia just give me a chance, nitamuheshimu mwanamke wako, I promise...so yakaanza mapenzi pale, I never been happy like that, that guy knows how to treat a woman, so loving, so caring, just imagine wagonjwa tunahudumiwa vile, mwanamke wake je? ndugu enu nikazidi kufall deeper and deeper.

Leon aliona mabadiliko yangu, akawa anauliza ila namkwepa, tukisex I don't feel it...inabidi nimvutie picha Karim just to feel Leon, ila sikuweza kumuacha Leon maana najua Karim alikua ni kwa mda , I just borrowed him. Tukaarange na Karim tukutane Kenya, niliomba likizo ya wiki moja job, Karim hakua amechukua likizo mda mrefu kwaio aliomba likizo kubwa, we spent that week like Honeymooners, we had lots of fun, his sex was magic daamn , it was so good...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom