Sikubaliani na Tundu Lissu kuhusu Hayati Magufuli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,084
2,000
Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.

Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.

Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.

Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!

Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.

Mambo yamekuwa mambo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
9,995
2,000
Unakubaliana na Lissu katika mambo gani?
Angalau matatu makubwa
 

mbuyake

Member
Feb 20, 2013
66
125
Mimi nimempata kwamba Lissu aliwahi kumwita anko magu dicteta uchwara kwamba hakukamilika kuitwa dicteta kamili lakin Kwa mtazamo wake yeye vuta nikuvute amemwona anko magu Kama dikteta kamili kutokana na sifa za dictator anavyozijua na baadhi amezitaja ambazo anko alikuwa anazitenda.
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
764
1,000
Ilibidi awe hivyo kutokana na!

Kwanza ndilo lilikuwa hitaji kamili la nchi wakati huo, lakini pia lilikuwa hitaji la Upinzani Kwa kuwa walitaka apatikane kiongozi sio dhaifu, ni mwenye chembe ya udicteta, na wakati nchi ikingia ktk Hali ya kuombea, watu waliomba apatikane kuiongozi atakayezuia wizi na ufisadi uliokuwa umekithili

Kukithili Kwa uwizi, ufisadi, huduma mbovu, uuzaji madawa ya kulevya, ukwepaji Kodi, Uonevu na kila Aina ya ufisadi, ilikuwa ni cheni iliyokuwa imechukua watu weeengi mpaka ktk ngazi za juuu kabisa za viongozi wetu,

Kuondoa huo uozo, ilitakiwa awepo Mtu kama huyo, na ilimbidi awe mithili ya Dicteta Kwa sababu bila hivyo, isingewezekana kuondoa huo mfumo

Kipindi cha nyuma, watu wengi Sana walikuwa walipoteza Maisha Yao Kwa kukosa huduma nzuri mahospitalini, kwani dawa zoote za Serikali zilikuwa zikigawanwa ju Kwa ju, huku Masikini na wasiojiweza kabisa wakiathirika na mfumo huo mbovu

Kipindi cha nyuma, vijana wengi wa Kitanzania walikosa mwelekeo Kwa sababu ya kujiingiza katika mihadarati ambapo huduma hiyo ilikuwa IPO kila eneo na hakuna kizuizi, ilifikia mtu akitaka kutaja wauza madawa, anapewa masaa 24 apotee au apotezwe, Kwa sababu tu ya nguvu ya wauza madawa, na walikuwa hatari kuishinda hata serikali yenyewe

Nahitimisha kusema, JPM ambaye ni Hayati, udicteta wake tunaousema leo, tuliutengeneza Sisi, ama mazingira yaliyokuwepo ndio yaliyomtengeneza kuwa Dicteta!
 

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
838
1,000
Mzee Vuta tupatupa, leo ndugu zako wa lumumba watakukalia kooni uko tayari? yaani mwendazake alikuwa ni kamili na si ucharwa? haya ccm hawakuyaona au walipewa kichuri cha Tarime na kutuletea aliye wanyamazisha? Makamba SR. alimuona maana alisema watu watabatizwa kwa moto, maneno yale ndio yaliyo akisi ukweli wa awamu ya tano chini ya uchwara/Kamili.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,144
2,000
Alikuwa dictator kabla hata hajashika madaraka, aliyoyapata madaraka ndio ikiwa platform ya kuanika udictator wake. Usitake kupotosha kwa kuonyesha eti wapinzani au mazingira ndio yalimfanya awe hivyo. Kama alikuwa anafanya waliyotaka wapinzani, mbona alizuia katiba mpya wakati lilikuwa ni dai la dhahiri la wapinzani?

Halafu kwa taarifa yako, hakuzuia rushwa bali alibadilisha utaratibu wa kula rushwa. Huko mahospitalini mnakosema huduma ni bora, wote tuko hapa nchini, udhaifu wa huduma za hospitali tunauona, msidhani propaganda na kuminya uhuru wa vyombo vya habari unaweza kutuondoa kwenye ukweli. Vibanda vya kujifukiza sio ubora wa matibabu, bali ni kuhalalisha ushirikina dhidi ya sayansi.
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
10,202
2,000
Amen,

UKWELI HUU UTAZIDI KUTUWEKA SOTE HURU.

Hata wale waliokuwa wananyamaza, wengine wakifurahia na kushangilia kuona

-maiti za binadamu wenzao zikiwa kwenye viroba
-wanadamu wenzao wakishambulia kwa marisasi
-wenye mawazo na mitazamo tofauti kukamatwa, kuteswa na kubambikiwa kesi.
-wa vyama vingine wakizuiwa kwa maguvu na mabavu ya dola kufanya kazi zao kikatiba.

AMEN
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom