Sikubaliani na Tundu Lissu kuhusu Hayati Magufuli

Ndugu yangu Kila siku nakuasa humu.

Tangu kura za 2015 hujatulia kiakili. Kubariana na mimi katika hili kisha tusonge mbele.

Kabla ya 2015 ulikuwa ukipost kitu humu kila mtu anasoma kwa umakini.

Unaonaje sasa kama haya mawazo utaanza kuyaweka kule wasapu na facebook?.

JF inatakiwa iheshimiwe na ni saver ya kudumu.

Hoja za CAG kwako unaona zinauzito basi umekopwa akili.
Umeandika nini sasa!
 
List ya madikteta wa ukweli inajulikana na mwendazake hawezi kuwamo. Hapo unazungumzia watu wa viwango vya akina:

Hitler, Mussolini, Lenin, Stalin, Kim, Saddam, Gaddafi, na wa aina hiyo.

Tambua nguvu za hawa kijeshi, kiintelijensia na hata kiuchumi. Tambua hawa walitetemesha dunia.

Mwendazake? Wajameni mbona Lissu aligonga penyewe? Alikuwa na nini huyu zaidi ya kuonea watu hata wasiokuwa tishio kwake?

Madikteta wa ukweli hawahangaiki kununua watu kuunga juhudi, hawaendi kudhulumu watu mali zao, hawali mahindi barabarani, Siyo washamba, nk.

Mwendazake zake alikuwa dikteta mshamba ambayo ndiyo maana halisi ya dikteta uchwara.

Hiiiiii bagosha!
Basi sawa. Dikteta ni dikteta- awe uchwara au kamili.
Tumshukuru Mungu kwa kazi yake isiyo na makosa.
 
Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.

Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.

Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.

Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!

Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.

Mambo yamekuwa mambo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
Kwa asilimia kubwa viongozi walinyamaza kimya kwa kulinda matumbo yao na si kwa kumuogopa Mwendazake . Kikubwa walichokiogopa ni kutumbuliwa tu.
 
Vioja vyenu ni hivi hivi kila siku. Sasa yote uliyotuandikia amekwisha ondoka nayo. Je, wewe unalalamika mpaka sasa unaisaidia vipi jamii kupata kile ambacho hawakupewa kwa makusudi au bahati mbaya. Watu bado wanakula mlo mmoja tena ugali na mboga ya kisamvu kisichougwa!

Sasa mjinga wewe leta hoja ya kusukuma maendeleo ya taifa mbele maana yule unayemwita dikteta ameondoka na yake. Wewe utabaki kulalamika mpaka lini, hivi vioja vyenu huwa ni chuki tu au kutafuta likes na sifa za wajinga wajinga?
 
Basi sawa. Dikteta ni dikteta- awe uchwara au kamili.
Tumshukuru Mungu kwa kazi yake isiyo na makosa.

Mola ni wa kushukuriwa kwa kila jambo.

Hoja ni katika kumuweka mleta mada kubakia kwenye mstari au reli. Wanaita waungwana, kuweka rekodi sawa sawa japo kwa vizazi vijavyo.

Au na hilo nalo hulitaki ndugu yangu?
 
Hebu pitia title yako hapo juu na soma kwa umakini content yako, then utagundua kama upo sahihi au la. Umempinga mtu lkn kwa maelezo yako bado una reflect yaleyale ya uliempinga.
Muelewage bageshi?! Anapingana na Lissu kumuita Mwendazake Dikteta Uchwara, akimaanisha alikuwa Dikteta kamili au mbaya zaidi kama kina Idd Amin, Stalin, Hitler, Bokassa, Franco wa Spain nk nk! Bajameni!
 
Ilibidi awe hivyo kutokana na!

Kwanza ndilo lilikuwa hitaji kamili la nchi wakati huo, lakini pia lilikuwa hitaji la Upinzani Kwa kuwa walitaka apatikane kiongozi sio dhaifu, ni mwenye chembe ya udicteta, na wakati nchi ikingia ktk Hali ya kuombea, watu waliomba apatikane kuiongozi atakayezuia wizi na ufisadi uliokuwa umekithili

Kukithili Kwa uwizi, ufisadi, huduma mbovu, uuzaji madawa ya kulevya, ukwepaji Kodi, Uonevu na kila Aina ya ufisadi, ilikuwa ni cheni iliyokuwa imechukua watu weeengi mpaka ktk ngazi za juuu kabisa za viongozi wetu,

Kuondoa huo uozo, ilitakiwa awepo Mtu kama huyo, na ilimbidi awe mithili ya Dicteta Kwa sababu bila hivyo, isingewezekana kuondoa huo mfumo

Kipindi cha nyuma, watu wengi Sana walikuwa walipoteza Maisha Yao Kwa kukosa huduma nzuri mahospitalini, kwani dawa zoote za Serikali zilikuwa zikigawanwa ju Kwa ju, huku Masikini na wasiojiweza kabisa wakiathirika na mfumo huo mbovu

Kipindi cha nyuma, vijana wengi wa Kitanzania walikosa mwelekeo Kwa sababu ya kujiingiza katika mihadarati ambapo huduma hiyo ilikuwa IPO kila eneo na hakuna kizuizi, ilifikia mtu akitaka kutaja wauza madawa, anapewa masaa 24 apotee au apotezwe, Kwa sababu tu ya nguvu ya wauza madawa, na walikuwa hatari kuishinda hata serikali yenyewe

Nahitimisha kusema, JPM ambaye ni Hayati, udicteta wake tunaousema leo, tuliutengeneza Sisi, ama mazingira yaliyokuwepo ndio yaliyomtengeneza kuwa Dicteta!
Sisi waTz tulizoea kupata pesa kilaini hatutaki pesa ya jasho. Ndo maana kila mtu analake
 
Kwani ilifikia hatua kama hao uliowainisha hapo chini? Maybe there was some elements and not the way u think.
Muelewage bageshi?! Anapingana na Lissu kumuita Mwendazake Dikteta Uchwara, akimaanisha alikuwa Dikteta kamili au mbaya zaidi kama kina Idd Amin, Stalin, Hitler, Bokassa, Franco wa Spain nk nk! Bajameni!
 
Mimi nimempata kwamba Lissu aliwahi kumwita anko magu dicteta uchwara kwamba hakukamilika kuitwa dicteta kamili lakin Kwa mtazamo wake yeye vuta nikuvute amemwona anko magu Kama dikteta kamili kutokana na sifa za dictator anavyozijua na baadhi amezitaja ambazo anko alikuwa anazitenda.
Magufuli alianzia kwenye uchwara lakini aliendelea Hadi akahitimu Udikteta kamili. Magu alikuwa zaidi ya Dicteta.
 
Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.

Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.

Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.

Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!

Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.

Mambo yamekuwa mambo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
Uko sawa mwandishi.
 
Ilibidi awe hivyo kutokana na!

Kwanza ndilo lilikuwa hitaji kamili la nchi wakati huo, lakini pia lilikuwa hitaji la Upinzani Kwa kuwa walitaka apatikane kiongozi sio dhaifu, ni mwenye chembe ya udicteta, na wakati nchi ikingia ktk Hali ya kuombea, watu waliomba apatikane kuiongozi atakayezuia wizi na ufisadi uliokuwa umekithili

Kukithili Kwa uwizi, ufisadi, huduma mbovu, uuzaji madawa ya kulevya, ukwepaji Kodi, Uonevu na kila Aina ya ufisadi, ilikuwa ni cheni iliyokuwa imechukua watu weeengi mpaka ktk ngazi za juuu kabisa za viongozi wetu,

Kuondoa huo uozo, ilitakiwa awepo Mtu kama huyo, na ilimbidi awe mithili ya Dicteta Kwa sababu bila hivyo, isingewezekana kuondoa huo mfumo

Kipindi cha nyuma, watu wengi Sana walikuwa walipoteza Maisha Yao Kwa kukosa huduma nzuri mahospitalini, kwani dawa zoote za Serikali zilikuwa zikigawanwa ju Kwa ju, huku Masikini na wasiojiweza kabisa wakiathirika na mfumo huo mbovu

Kipindi cha nyuma, vijana wengi wa Kitanzania walikosa mwelekeo Kwa sababu ya kujiingiza katika mihadarati ambapo huduma hiyo ilikuwa IPO kila eneo na hakuna kizuizi, ilifikia mtu akitaka kutaja wauza madawa, anapewa masaa 24 apotee au apotezwe, Kwa sababu tu ya nguvu ya wauza madawa, na walikuwa hatari kuishinda hata serikali yenyewe

Nahitimisha kusema, JPM ambaye ni Hayati, udicteta wake tunaousema leo, tuliutengeneza Sisi, ama mazingira yaliyokuwepo ndio yaliyomtengeneza kuwa Dicteta!
Kuzuia ufisadi ni kuzuia mfumo wa vyama vingi nchini?? Hivi unapoleta maneno mengi ya kijinga unajenga au unabomoa?Ona sasa mnavyodhalilishana wenyewe kutokana na mifumo yenu mibovu wengine wanatamani marehemu afufuka ili waendelee kupiga kwa kisingizio cha uzalendo feki,huu ni uzwazwa
 
Lisu ni mpumbavu anayetumia 071 kulelewa na wanaume wenzake ulaya
Achana na kiwango chako cha akili, bali kwa kiwango chako cha umri tu unapaswa kujiheshimu na kujizuia baadhi ya hisia zako usizitoe hadharani. Unawatilia aibu wazazi wako na wote ambao ulipita mikononi mwao kwamba hawakufanya chochote katika kukujengea tabia njema. Cha ajabu unaweza kushangaa wewe ni mume au mke wa mtu au hata mzazi wa watoto. Ona aibu kuwa wa hovyo kiasi hiki.

Hata kama hayo mambo ndio fani yako na unayapenda na pengine hata sasa hivi unafanyiwa au unayafanya, basi yaache. Ni tabia chafu na haikubaliki kwa mtu wa heshima kama wewe.
 
Unakubaliana na Lissu katika mambo gani?
Angalau matatu makubwa
Hebu pitia title yako hapo juu na soma kwa umakini content yako, then utagundua kama upo sahihi au la. Umempinga mtu lkn kwa maelezo yako bado una reflect yaleyale ya uliempinga.
Yaani nyie wawili tu wa awali mmeamua kuwa "wajinga wa makusudi" kwa kutoa comment bila hata kusoma na kuelewa, au siyo?

Jifunzeni kusoma/kumsikiliza na kuelewa mtu kwanza kabla ya kushika kalamu au kupanua midomo yenu kusema lolote...!

Ni ushauri tu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom