Inasikitisha mjadala umejaa hofu ya nchi kunyimwa misaada wakati Lisu ameongea mengi yanayo hitaji kufuatiliwa ili wananchi tuufahamu ukweli. Suala la kuendesha nchi kwa misaada ni la kulionea aibu na si lakujivunia hata kidogo, hivyo halipaswi kutupotezea muda.
Kuna mambo ambayo yame kwepwa kuzungumziwa hapa, ambayo ni miongoni mwa vitu ambayo vimechangia bwana Lisu kudai Misaada isitishwe, mambo kama upendeleo wa kifamilia, kikabila, kikanda na kidini. Haya mambo si mazuri na hakika tukiwa kama wazalendo wa nchi hii tuna haki ya kujua ukweli wa jambo hili kutoka kwa bwana Magufuli na zaidi ufanyike uchunguzi wa wazi ili kujua kama Ofisi ya Urais inatumiwa vibaya kama ilivyo elezwa na bwana Lisu ama Lisu anajaribu kuichafua ofisi kuu nchini na kuigomabanisha na wananchi wake.
Na mwisho hatua kali zichukuliwe kwa yeyote atakaye onekana kutotenda haki katika hili nikimaanaisha kama ni maneno ya uongo Lisu awajibike lakini kama nikweli basi Magufuli awajiboke vile vile kadiri katiba yetu itakavyoona inafaa.