Sikubaliani na Tundu Lissu katika hili...

Sikubaliani na Tundu Lissu katika hili...

Joined
Oct 4, 2016
Posts
49
Reaction score
81
Ndugu zangu kuna baadhi ya mambo ambayo viongozi wetu wamekuwa wakiya fanya mazuri na mabaya pia

Lakini nipende kuwambia kumsifia kiongozi anapokosea ni kuua nchi yetu

Si lazima kila kitu tukubaliane nacho

Tundulisu amesikika akisema kuwa jumuiya ya kimataifa isitoe misaada kwa tanzania maana kutoa misaada hiyo ni kuunga mkono utawala wa kukandamiza demokrasia

Hizi kauli nadhani ni kauli ambazo zimetolewa kwa hasira ,kuna njia nyingine ambazo tunaweza kuonesha ni kwa namna gani utawala huu unakamdamiza demokrasia kama ni kweli

Lakini hii hatua ya kushawishi jumiyya ya kimataifa kusitisha misaada kwa nchi yetu ni kupinga kwa wazi hatua kwa ajiri ya maendeleo

Nchi yetu bado tunahuataji misaada kwa ajiri ya kukuza uchumi wetu na kukuza maendeleo kwa ujumla kama ilivyo kwa nchi zingine.Tena si kupewa misaada tu hata kukopa nako pia tunatakiwa tukope

Watu kama hawa wanamlamu Tundu Lissu bila hata wao kutoa njia mbadala tufanyanye nini ili tusifike huko tuendako,

najua wenye akili ya kushikishwa wao hulaumu tu pamoja na kwamba Tundu Lissu ameelezea na sababu lakini tu wao huendelea kulaumu na kulalama na hii itakuja kutupa shida sana huko tuendako maana Mkubwa mmoja akimlaumu tu Tundu Lissu basi anakuwa kama amefungulia mbwa kila mtu anamlaumu tu ukimuuliza kwa nini anafanya hivyo anakuambia wewe hukumsikia Mkuu wa kaya akimlaumu Tundu Lissu???

Watanzania tuamke tusiwe na akili ya kushikishwa na sisi tunaimba wimbo ule ule wa wakubwa hii haitakiwi kabisa tunachotakiwa ni kufuata katiba yetu na utawala huu nguli wa kuvunja katiba yetu.
 
Huyu TL kwa hili la misaada kapotoka sana,inaonyesha ana hasira na jazba nyingi hadi amesahau hao wa kimataifa wakikubaliana na hoja zake hata wapiga kura wake nao wataathirika.Mtazamo huo wa TL ni sawa na mtu anayekata tawi alilokalia akitegemea kua hilo tawi litakapokatika eti yeye atabaki salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema Kamanda Lissu dhidi ya udhalimu unaofanywa na huyu mdhalimu fisadi, mwizi, muongo na dikteta uchwara nchini kwetu. Watanzania tunaojitambua tuko pamoja nawe.

Ndugu zangu kuna baadhi ya mambo ambayo viongozi wetu wamekuwa wakiya fanya mazuri na mabaya pia

Lakini nipende kuwambia kumsifia kiongozi anapokosea ni kuua nchi yetu

Si lazima kila kitu tukubaliane nacho

Tundulisu amesikika akisema kuwa jumuiya ya kimataifa isitoe misaada kwa tanzania maana kutoa misaada hiyo ni kuunga mkono utawala wa kukandamiza demokrasia

Hizi kauli nadhani ni kauli ambazo zimetolewa kwa hasira ,kuna njia nyingine ambazo tunaweza kuonesha ni kwa namna gani utawala huu unakamdamiza demokrasia kama ni kweli

Lakini hii hatua ya kushawishi jumiyya ya kimataifa kusitisha misaada kwa nchi yetu ni kupinga kwa wazi hatua kwa ajiri ya maendeleo

Nchi yetu bado tunahuataji misaada kwa ajiri ya kukuza uchumi wetu na kukuza maendeleo kwa ujumla kama ilivyo kwa nchi zingine.Tena si kupewa misaada tu hata kukopa nako pia tunatakiwa tukope

Watu kama hawa wanamlamu Tundu Lissu bila hata wao kutoa njia mbadala tufanyanye nini ili tusifike huko tuendako,najua wenye akili ya kushikishwa wao hulaumu tu pamoja na kwamba Tundu Lissu ameelezea na sababu lakini tu wao huendelea kulaumu na kulalama na hii itakuja kutupa shida sana huko tuendako maana Mkubwa mmoja akimlaumu tu Tundu Lissu basi anakuwa kama amefungulia mbwa kila mtu anamlaumu tu ukimuuliza kwa nini anafanya hivyo anakuambia wewe hukumsikia Mkuu wa kaya akimlaumu Tundu Lissu???Watanzania tuamke tusiwe na akili ya kushikishwa na sisi tunaimba wimbo ule ule wa wakubwa hii haitakiwi kabisa tunachotakiwa ni kufuata katiba yetu na utawala huu nguli wa kuvunja katiba yetu.
Unasema hivo unashindwa kutafakari kuwa ktk nchi yeyote ile dunia ufadhili wa misaada ni muhimu kwani husaidia kukuza maendeleo ya nchi

Kukataza nchi isipewe misaada kwa minadhiri ya uhuru wa kidemokrasia

Kwanza: Ni kushindwa kufikiri ktk upeo sahihi

Pili:ni kuchimba kabuli na kujifukia wenyewe

Hiyo ni sawa na mtoto anaye susa chakula huku ananjaa kisa mama yake kamkasirisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama hawa wanamlamu Tundu Lissu bila hata wao kutoa njia mbadala tufanyanye nini ili tusifike huko tuendako,najua wenye akili ya kushikishwa wao hulaumu tu pamoja na kwamba Tundu Lissu ameelezea na sababu lakini tu wao huendelea kulaumu na kulalama na hii itakuja kutupa shida sana huko tuendako maana Mkubwa mmoja akimlaumu tu Tundu Lissu basi anakuwa kama amefungulia mbwa kila mtu anamlaumu tu ukimuuliza kwa nini anafanya hivyo anakuambia wewe hukumsikia Mkuu wa kaya akimlaumu Tundu Lissu???Watanzania tuamke tusiwe na akili ya kushikishwa na sisi tunaimba wimbo ule ule wa wakubwa hii haitakiwi kabisa tunachotakiwa ni kufuata katiba yetu na utawala huu nguli wa kuvunja katiba yetu.

Lissu ameshaiona hatari ya kutorudi bungeni 2020. Anajaribu kujidhatiti kimkakati zaidi, bahati mbaya mbinu anayojaribu kuitumia haina manufaa sana, binafsi ningelikuwa Lissu ningejikita jimboni kwangu zaidi kuliko kupoteza mda kwenye media ambazo kwa hakika wananchi wa Singida Mashariki hawatamwelewa.

Watanzania wengi hasa vijijini wanachotaka ni kuona shughuli za maendeleo zikifanywa bega kwa bega na mbunge wao, kama afanyavyo profesa Jay wamitulinga kuliko huu upuuzi wa kwenye media wa huyu wakili msomi wa chadema.

Lissu apambane na ukanda na ukabila uliopo kwenye chama chake kwanza ndoo amseme magufuli,maana hata dada yake alichaguliwa viti maalumu chadema kama sikosei.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lisu analituhumu kanisa kupata upendeleo wa vibali vya kazi. Kinachoonekana ni hapa ni kuwa Lisu hajui utaratibu unaotumiwa na kanisa katoliki kuwawezesha wamisionary wageni kupata working permit.

Miaka yote Wamisionary wanaofanya kazi Tanzania hukusanya taarifa zao za maombi ya Residence permit na kuzipeleka Ofisi ya Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu. Baraza linachambua na kukagua viambatanisho mhimu ikiwa ni pamoja na malipo ya ada za vibali hivyo.

Baraza huwasilishwa documents hizo Ofisi ya Uhamiaji. Kama Lisu analalamikia huu utaratibu na kuuita upendeleo kwa wakatoliki? Akumbuke kanisa katoliki ni taasisi iliyodumu muda mrefu zaidi duniani. Hivyo imeshaandaa working standards ili kuepuka hujuma na migongano na serikali.

Lisu ikiwa ana stress za Lowasa kutangaza nia asema tu watu watamuelewa. Aache kuchonga maneno akifikiri kila mtu ni mbumbumbu.
 
Lisu ni DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA according to wahenga. Anatafuta kick anajua fika 2020 harejei bungeni..halafu alivyo nyumbu anafikiri jumuia za kimataifa zinasikiliza watu wapayukaji na wajinga kama yeye.Hio kitu haipo eti Tanzania isusiwe kwa ajili ya huyu chizi, NEVER IT WON'T HAPPEN.Hizo ni ndoto za wendawazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfano tukinyimwa misaada...yeye ndio ataleta demokrasia?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app

Kuwekewa Bikwazo au kunyimwa misaada ni njia ya kukulazimisha ufanye kitu fulani, point ni kuwa kuna mambo hayaendi sawa kwenye nchi na WAPINZANI, BUNGE na MAHAKAMA havina uwezo tena wa kujisimamia kama taasisi huru, Serikali haiwapi nafasi zao za kikatiba, hivyo ni Shinikizo pekee kutoka kwa wafadhili ndio litakaloweza kuirudisha nchi kwenye mstari

Watu wengi huwa hawamwelewi TL anapozungumza, waxhache sana ndio wanaomwelewa hapo kwa papo, wengine wanachukua wiki, mwezi, miezi, mwaka na hata miaka
 
Kabla sijasema chochote,natamani kujua kama TL anatujali sisi watz au anajali mkate wake tu,?Tukikosa misaada watoto wetu hatutachanja kuzuia maradhi,watakufa.ARVs hatutapata na watakaokufa ni wengi mno,bujeti yetu itasimama,umeme wa REA hautakuja tena,dhiki zitaongezeka ili yeye awe na amani,je hiyo ni sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inashangaza unaposoma baadhi ya wachangiaji wanaomkebehi Lissu. Hivi tumelogwa kiasi gani? Demokrasia imetoweka kama upepo wa vuli halafu Lissu anajaribu kuwaamsha mtambue linaloendelea mnasema siasa za maji taka siasa safi ni zipi na nani anayehubiri siasa safi??

Tulilogwa aliyetuloga sijui ni nani? Ubunge atapata tena kwa kura nyingi tuuuu endeleeni kulala mpaka mwizi aibe mpaka kijiko na sahani. Lissu endelea kutoa Elimu tutaelewa tu.
 
Huyu TL kwa hili la misaada kapotoka sana,inaonyesha ana hasira na jazba nyingi hadi amesahau hao wa kimataifa wakikubaliana na hoja zake hata wapiga kura wake nao wataathirika.Mtazamo huo wa TL ni sawa na mtu anayekata tawi alilokalia akitegemea kua hilo tawi litakapokatika eti yeye atabaki salama.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sielewi unachotetea. Budget ya mwaka jana ya maendeleo haikufikiwa kwa sababu ya huyo unayemtetea wala hakujali na hatajali. MCC na wafadhili wengine wameondoa pesa kibao mpaka tunaambiwa kuwaz hata hii budget ya juzi haitatekelezeka kwa kukosa pesa za misaada.

Sababu ni hayohayo mambo anayolalamikia Lissu na wenzake. Lissu aseme asiseme wenye hela zao wasiporidhika na mwendo wetu watakata hiyo misaada. Inasemekana hata fedha za mirdi mikubwa ukopaji ni shida sababu ni hizohizo. Bado makesi ya kutafuta kibao. Halafu tunatafua visingizio.
 
Back
Top Bottom