Ndugu zangu, sikubaliani na kitendo kilichotokea bungeni usiku cha UKAWA kuzua kelele bungeni badala ya kujadili namna ya kuwahukumu wezi kama walivyoanza mwanzoni. Kwa kweli hii inaonyesha kuwa watu hawajakomaa kisiasa. Kitendo hiki kilianzishwa/kilitokea wakati Mbowe anaongea. Source yake ni Mbowe kwa kuleta ubishi usiokuwa na maana wakati naye ni mtuhumiwa pamoja na Zitto. Nilisikitika sana na kuhuzunika sana kuona UKAWA walivyovunja bunge kwa kelele na kutuabisha sisi wananchi tuliowachagua. Kitendo hiki sio cha kistaarabu hata kidogo. Kwanza huwezi kutoa amri kuwa waziri afukuzwe badala ya kuacha suala hilo kwa mhusika mkuu kutoa kwanza maamuzi.Mimi nilitegemea hayo yangetokea endapo kama Mh.Rais angesema kuwa hawezi kuyashughulikia. Aibu sana kwa taifa na "SHAME ON THEM".