Siku za Lowassa CCM zinahesabika!

Siku za Lowassa CCM zinahesabika!

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Kwa hakika sasa si siri tena siku za gamba kubwa CCM Edward Ngoyaye Lowassa a.k.a Fisadi wa Richmonduli ndani ya CCM zinahesabika.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba kifikia tar 12/02/2013 Kamati Kuu ya CCM itakuwa imeundwa na baada ya kupata pigo kubwa kwa Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula, Katibu Mkuu Kinana na Kurudishwa kwa adui yake mkubwa Nape basi pigo la mwisho kwa EL ni uundwaji wa CC ambao kwa vyanzo vya jikoni kabisa..hakuna mtu wake hata mmoja.

Ikumbukwe vikao vitatu vya mwanzo vya uchujaji majina ya urais ni Sekretarieti chini ya Kinana na Nape, Kamati ndogo ya Maadili chini ya Mangula na Kamati Kuu chini ya JK...na kote huku hakuna kupiga kura ni mjadala tu then maamuzi..

Haya niyasemayo yalimkuta Lowassa mwaka 1995 aliondolewa kwenye kinyang'anyiro bila kura, yalimkuta pia Malecela aliondolewa bila kufilishwa kwenye kura...historia itajirudia 2015.
 
Mkuu Honey K,

1. Mbona Kinana naye ana tuhuma fulani hivi zinachukuliwaje na CCM!

2. Mbona JK amekalia tuhuma mbalimbali, yaani
a) Deep Green Finance,
b) Mwananchi Gold,
c) Meremeta,
d) Rada
e) EPA - hapa CCM imeshindwa kujibu alipo "Marehemu" Daudi Balali
f) Richmond, nk, na alipitishwa kugombea uchaguzi mkuu 2010 na sasa hivi ameendelea kulea rushwa ambayo imeendelea kuitafuna CCM hadi kwenye mifupa?

3. Wewe unafiliri CCM ilivyo kwa sasa ina "moral authority" ya kupambana na rushwa? Maana ikifika kwenye kura za maoni tunashuhudia jinsi CCM inavyotembeza rushwa kwa wapiga kura na viongozi WENGI kama si wote wa CCM wametokana na rushwa!
 
Thubutu maccm hayana tabia yakuadabisha wanachama wanao toka nje ya mstari.
 
Mkuu Honey K,
1. Mbona Kinana naye ana tuhuma fulani hivi zinachukuliwaje na CCM!
2. Mbona JK amekalia tuhuma mbalimbali, yaani a) Deep Green Finance, b) Mwananchi Gold, c) Meremeta, d) Rada e) EPA - hapa CCM imeshindwa kujibu alipo "Marehemu" Daudi Balali !
Mkuu,
Unauliza mahali alipo marehemu?
Simple, yuko KABURINI!...au hujui kuwa makaburi ya kisiasa marehemu unaweza kupigana naye kikumbo mtaani!!
 
Last edited by a moderator:
Buchanan

Majibu ya maswali yako ni siri ya taifa kwa serikali yetu. Na kama siku wakiyatoa ni kama kuendelea kujaza tyre mpira na mwishoni likashindwa kuhimili upepo utasikia kishindo cha puuuuuup ishara ya kwamba umezidisha upepo na hapo ndiyo mwisho wa story!!
 
Last edited by a moderator:
samahani mkuu sijakuelewa anayehesabu hizo siku ni nani??

ila tukubaliane kumtoa CCM hawawezi labda hilo la kumpitisha kugombea urais
 
Honey K

Ila kuweni makini kaka.

Haya mambo ya watu kuwekana ndani ya chama kwa kupangana kiasi cha kwamba inafikia watu kushindwa kuwajibishana ndiyo yanayotuharibia chama.

Kuweni makini sana kwa sababu siasa za sasa zinahitaji weledi na uadilifu mkubwa la sivyo lazma tutapata changamoto kuu.
 
Last edited by a moderator:
Buchanan

Mkuu haya maswali yako yalishaondolewa kwenye mitaala ya elimu. Hivyo unatoa maswali kwa vitu ambavyo havijafundishwa darasani kwa maana hiyo hakuna majibu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Waovu wanapopambana wao kwa wao inakuwa ni unafuu kwa watu wa haki.

M4C......lets go...
 
wee honey K, EL siku zake zinahesabika??????????

EL kukoma kwake uanachama wa magamba ni kifo tu kitakapomnyemelea....ama jela itakapo mhitaji 2015 chadema wakiwa magogoni.
 
Mh EL naye ni mwanasiasa...wakimtoa CCM ataenda CDM , TLP CUF au chama chochote kile.....kwa wanasiasa wenzake.....
 
Damn if they do, damn if they dont! Lowassa anaweza (singlehandedly) kuizika CCM. Safu yote ya juu CCM iko contaminated vibaya na huyu Mh (Lowassa) anatembea na funguo: hakuna cha Kinana wala Mangula. Kwani Mangula si ndio alikuwa Katibu mkuu wakati wa EPA? Kinana - pa kuanzia shida!
 
Wewe hujui unaandika nini lowassa ndio mwenye chama huyo mwenyekiti wako huwa anamfuta nguludoto kule,unabwabwaja tu subiri uone mziki wake kama kuna mtu anaweza kumnyoshea kidole ndani ya ccm!!!!!!!!
 
Mkuu Honey K,

1. Mbona Kinana naye ana tuhuma fulani hivi zinachukuliwaje na CCM!

2. Mbona JK amekalia tuhuma mbalimbali, yaani
a) Deep Green Finance,
b) Mwananchi Gold,
c) Meremeta,
d) Rada
e) EPA - hapa CCM imeshindwa kujibu alipo "Marehemu" Daudi Balali
f) Richmond, nk, na alipitishwa kugombea uchaguzi mkuu 2010 na sasa hivi ameendelea kulea rushwa ambayo imeendelea kuitafuna CCM hadi kwenye mifupa?

3. Wewe unafiliri CCM ilivyo kwa sasa ina "moral authority" ya kupambana na rushwa? Maana ikifika kwenye kura za maoni tunashuhudia jinsi CCM inavyotembeza rushwa kwa wapiga kura na viongozi WENGI kama si wote wa CCM wametokana na rushwa!

Mkuu zamani kulikuwa na tangazo la kujifunza english la CILOS. ''Anaongea Ki ingereza kigumu, njoo uongee nae wewe'' sasa na wewe haya maswali yako ni magumu sana naamini hata fastjet akiyaona hataweza kuyajibu zaidi ya kusema kuwa huu ni upepo na utapita tu.
 
hii ndio si HASA, (assumption + forecasting)
wakati maisha ya wengi ni duni huku wachache bado wakifurahia na kushabikia kapu la samaki walioza kwa ufisadi na utawala mbovu usio na credit kwa majority.
 
Back
Top Bottom