Siku za Lowassa CCM zinahesabika!

Siku za Lowassa CCM zinahesabika!

najua mnamuogopa sana lowasa nyie wazee wa mdimu....kwa taarifa yenu ni kwamba lowasa ni mtu wa plan b unachokiwaza leo kuhusu zengwe alkiwaza 4yrs ago so anajua cha kufanya 2015 ukitaka jimalze lowasa ts a presdent to be...ccm si mama yake wala baba yake
 
Hivi na zile siku 90 za kujivua gamba bado hazijaishja?
 
Mtoa uzi ameonesha wazi kuwa anachuki binafsi na Laigwanani Hon. E.Lowasa kwani unaanza uzi kwa kumtukana.
Pili iiingie akili mwako kuwa Katika CCM ya sasa ukitumia rushwa kama kigezo basi unafukuza wote kasoro makamu mwenyekiti ambaye naye utamstahi kwa kuangalia maisha yake binafsi na asivyosaidia ndugu zake wanaoenda kumuomba vimemo vya msaada katika kutafuta kazi. (Anawafukuza kwa kuwapa nauli tu). Hivyo basi rushwa katika CCM ya leo sio issue. Na juhudi za kumzuia Laigwanani kugombea urais wa CCM zitaicost CCM kuliko kuisaidia. Yetu macho.
Wosia wangu kwa JK juu ya hili, asifanye makosa aliyofanya Mkapa kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM. JK akijiingiza kichwa kichwa tu CCM ataondoka nayo 2015
 
Hakuna chama kinaendeshwa kidekteta kama CCM yaani Jakaya Kikwete wizi wake mwenyewe ameusahau akiondoka Lowassa Kikwete naye aondoke huu mtindo wa kuhamisha dhambi kwa wenzio haufai
 
Kwa hakika sasa si siri tena siku za gamba kubwa CCM Edward Ngoyaye Lowassa a.k.a Fisadi wa Richmonduli ndani ya CCM zinahesabika.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba kifikia tar 12/02/2013 Kamati Kuu ya CCM itakuwa imeundwa na baada ya kupata pigo kubwa kwa Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula, Katibu Mkuu Kinana na Kurudishwa kwa adui yake mkubwa Nape basi pigo la mwisho kwa EL ni uundwaji wa CC ambao kwa vyanzo vya jikoni kabisa..hakuna mtu wake hata mmoja.

Ikumbukwe vikao vitatu vya mwanzo vya uchujaji majina ya urais ni Sekretarieti chini ya Kinana na Nape, Kamati ndogo ya Maadili chini ya Mangula na Kamati Kuu chini ya JK...na kote huku hakuna kupiga kura ni mjadala tu then maamuzi..

Haya niyasemayo yalimkuta Lowassa mwaka 1995 aliondolewa kwenye kinyang'anyiro bila kura, yalimkuta pia Malecela aliondolewa bila kufilishwa kwenye kura...historia itajirudia 2015.
.

..Bado anayonguvu kubwa na ya kutosha katika CCM, wako watu wanaomtegemea yeye katika mambo mengi pamoja na nafasi zao katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM yenyewe na serikalini, pia CCM bado inaamini dhana isemayo huyu ni kada mwenzetu..... na katika kukiimarisha Chama hakuna haja ya kufukuzana ...kufukuzana kunazidi kuleta mpasuko, visa, visasi na mgawanyiko ... nia thabiti ya Chama ni kuleta umoja..mshikamano... na kuyasahau yaliyopita... kuweka nguvu kubwa kupambana na upinzani.....kamati ya akina Mangula itajikosha na kunawa kisha kusukumia wapiga kura waamue wenyewe...ili kukifanya chama kiendelee kushika dola ki - ulaini....... kama wengine wanavyosema ...kumdharau mtu ni adhabu tosha
 
CCM wasanii kweli,kwa hiyo mnaandaa kamati kuu ya kufanya kazi za chama au kumdhibiti Lowasa?
 
Labda kwa kukolimbwa. Alimuuliza swali moja bosi wake kuwa ni jambo gani alilipitisha bila kumshirikisha, hajawahi kujibiwa hadi leo. Yule pale mnavyomwona hatoki ccm, labda atake mwenyewe. Ni mwaga mboga nimwage ugali, hadithi tu ndio kitakachoendelea, hamna cha kumvua gamba wala nn
 
give me a break!!! i mean unaongelea huyu huyu EL tunayemjua sisi au? do that kama mnataka kukimalizia chama chenu hata before 2014.

sisi kikwetu ukichapia (ulimi ukiteleza) unaambiwa na wazee "tema mate chini" uondoe hoja yenye nuksi.
 
Mkuu Honey K,

1. Mbona Kinana naye ana tuhuma fulani hivi zinachukuliwaje na CCM!

2. Mbona JK amekalia tuhuma mbalimbali, yaani
a) Deep Green Finance,
b) Mwananchi Gold,
c) Meremeta,
d) Rada
e) EPA - hapa CCM imeshindwa kujibu alipo "Marehemu" Daudi Balali
f) Richmond, nk, na alipitishwa kugombea uchaguzi mkuu 2010 na sasa hivi ameendelea kulea rushwa ambayo imeendelea kuitafuna CCM hadi kwenye mifupa?

3. Wewe unafiliri CCM ilivyo kwa sasa ina "moral authority" ya kupambana na rushwa? Maana ikifika kwenye kura za maoni tunashuhudia jinsi CCM inavyotembeza rushwa kwa wapiga kura na viongozi WENGI kama si wote wa CCM

wametokana na rushwa!

El anamikakati mizito ya kuhakikisha kuwa anahamia ikulu 2015 vyovyote vile viwavyo ni kazi sana kusema mwisho wake CCM umewaia kwa kuwa ananetwork kubwa sana. kwa hivi sasa anajiimarisha makanisani na ndani ya chama na anawatu wanaomuunga mkono kwa nguvu zote
 
Labda kwa kukolimbwa. Alimuuliza swali moja bosi wake kuwa ni jambo gani alilipitisha bila kumshirikisha, hajawahi kujibiwa hadi leo. Yule pale mnavyomwona hatoki ccm, labda atake mwenyewe. Ni mwaga mboga nimwage ugali, hadithi tu ndio kitakachoendelea, hamna cha kumvua gamba wala nn


Kweli mkuu ametaka mwenyewe na ametoka
 
Back
Top Bottom