Siku yangu ya kwanza kuangalia video

Chenchele

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,984
2,500
Basi bhana kijiji fulani hivi Kuna jamaa alikua wakwanza kununua video Katika Kata ile around 2002/3. Yule bwana alikuw anaitwa Deo kama kawaida watu wa Kuoga na kulala kwenye majivu wa kijiji kilee tulikuwa machungoni mbuzi, ng'ombe etc. tukazinyaka habar njema tukiwa machungoni na kurudisha mbuzi kabla halijazama na kutinga mjengoni kuhakikisha alaa Deo kanunua video?.

Basi bwana yuleee siku ile ya kwanza alikua anatest zana mpya zile za sanaa Nakumbuka aliweka Mwinjuma Mimi eee!! banda LA nyasi chini pamefagiwa na kumwagiwa maji Ili kuzuia vumbi wazee wa Kazi makachero tukatinga chini Mwinjuma ikaisha...

Akapigwa maiko kipensi akaisha Akapigwa saida kaloli.. Ohoooo Saa nane kama kawa kiingilio hamsini mpaka Mia. Hhhhhhh zilipigwa miamia na hamsini nyumbani mpaka wakaomba poo. Mbuzi zulikuw zinarud Saa tisa Sina hela ili niwahi kufagia niingie bure siku za mbele nikataimiwa Dili LA kufagia Daaa ntafanyaje niingie Sina hela.....bwana yuleee akaruhusu mahindi ya kuchoma... Hhhhh matuta ya nyumbani yalipigwa mpaka mabua yote chini kisa Kuna kanda mpya Za the hard way, American ninja na vandane.... Nikaanza kuchelewa namba shuleni mwisho shule nzima ikamezwa na video vya Deo....

Hhhhh Palikuw na HP mnoko alikuja kwa Deo usiku akaandika majina ya wanafunzi Kesho yake shuleni kilinuka zilitembea fimbo shule nzima alibaki HP tu Kwahyo Wateja kwA Deo wakapungua. Binafsi sikuacha ila kasi ilipungua na kesi Za mahindi na tu hamsini na tumiamia zikapungua nyumbani ila kesi ikabaki kwenye kuwahisha mbuzi mapema nyumbani......
 
Nakumbuka kipindi hicho mwaka 2000..Baba ndo alinunua video aise nakumbuka nilikuwa muda mwingi sitoki home alivyonunua dish nikadanganya kuwa chumbani kwangu kuna wachawi nikamuomba mama nianze kulala sebuleni ili niwe nalala naangalia kideooo..
 
Mm mwenyew nimeshangaa hlf yuko comfortable kabisa kuna watu wa porini humu..
Hhhhhhhhhhhhh Acha Uchochezi Mkuu... Sio porini sana ila umeme ndo Umeenda mwaka huyu baada ya Kuzaliwa town Wazaz wakashuka Kijijini kwajili ya kilimo na ufugaji
 
Mm mwenyew nimeshangaa hlf yuko comfortable kabisa kuna watu wa porini humu..
labda kama kwenu ilikuwa dar vinginevyo sehemu nyingi za tanzania miaka hiyo hakukuwa na umeme ,nyumba za nyasi kibao hata smart phone hazikuwepoooo
 
Niliwatoa kule nikawaleta hapa.

Walaaniwe wote wanaosema JK hakuleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom