Siku yangu inavyomalizika kwa bahati

Siku yangu inavyomalizika kwa bahati

[emoji16][emoji16][emoji16] sijawahi aisee kwanza ananiheshimu balaa.
You did a good job.

Lakini be prepared. For sure drama zitaanza mpenzi wako atakaporudi...
 
Kuhusu wifi yako...yule mwanamke yuko smart balaa
You did a good job.

Lakini be prepared. For sure drama zitaanza mpenzi wako atakaporudi.

Sisi wanawake tupo very smart, and we see potential in a man. We can even smell it world's apart....

Sijui Kama atakuachia kirahisi japokuwa haupo kwenye mahusiano na yeye.

Ama ushapigaga kimasikhara mkuu Feyzal?
 
Nimetimiza wajibu wangu..mengine ni ya kibinadam
Mpenzi wako ulishamwambia? Ukumbuke si mwanao huyo, naona umetaarifiwa ukiambiwa 'mmepata mtoto' na wewe pia unachukuliwa kama umepata mtoto. Saidia inapokwezekana.
 
[emoji120]
Mungu akubariki Sana Sana... Pia akawe Mwamuzi kati yako na Mpenzio kwa Lolote litakalotokea.. Wanao na uzao wako kwa ujumla ukapate kuwa Baraka tele na pia Muwe Baraka kwa Kila Mtu...
 
[emoji120]
Mkuu hongera sana kwa kuwa na moyo wa kutoa na kusaidia, ubarikiwe sana,

Lakini sasa, kwa mpenzi wako jitahidi uwe wa kwanza kumweleza kuhusu hili, akijua mwenyewe au akiambiwa na mtu mwingine asie wewe, utapata tabu sana, narudia tena utapata tabu sana,

LA MUHIMU ZAIDI,
Endelea kumsaidia huyo binti na mtoto wake, lakini jaribu kuwa makini nae, pia nashauri ukae mbali kidogo.
Unafahamu, kwa namna ulivyomsaidia bila masharti yeye ndani anatamani kulipa fadhila japo kidogo.
Na kwa hali aliyonayo kitu pekee anaweza kulipa ni ngono. Kama atakuwa karibu na anaweza kushawishika kukutega katika hilo ili kulipa fadhira au hata kutamani kumpindua mpenzi wako akitamani hizo huduma azipate peke yake milele. Na wengi huenda mbali mpaka kutumia ushirikina. Yameshatokea sana. Yakitokea kwako utapata tabu sana.

Usitengeneze mazingira ya kumfanya atamani kulipa fadhila au kumpandisha kihisia au kumtamanisha akaanza kukutazama kwa mtazamo mwingine.
Kuna watu walitoa fadhila zikageuka madhila.
 
Mungu atanilinda katika hili kwa sababu nilikua na nia safi.
Umefanya jambo jema ila kasoro naona kukubali jina lako kutumika. Tumshukuru tu mzungu kwa DNA vinginevyo balaa lake lingekua zito kwa huyo mpenzi wako na pia binadam sio wema kama wewe, unaeza kuja kuta huyo bint siku akajakugeuka kichomi kwa maana alitumia jina lako kwenye kadi ya klinik bila kukupa taarifa huwezi jua motive aliyokua nayo nyuma yake.
 
Zarina, Ila Sasa akimaliza uzazi msaidie arudi kwao, pia Kama ulimpa jina lako mwambie Sasa majina ya mbele aweke ya kwao, unaweza kumsaidia mtaji akafanye mengine akiwa kwao kwa usalama wa penzi lako jitahidi kuwa mbali naye kwa Sasa na mchumba wako usimuonyeshe anafananaje Ila hiyo kukaa kwa dada yako nayo haikuwa vizuri cause atakupeleleza mengi kweli umetoa msaada Ila Kuna vitu vingi umeshakosea Kama Hilo la kumsogeza karibu na familia yako maana huwezi jua yeye na familia yake Sasa wanakuchukuliaje, kikubwa wewe jitahidi arudi kwao alafu utaendelea kumsaidia akiwa kwao.
 
Nimesema hapo juu atakaa mwezi mmoja kisha atarudi kwao...familia yake inajua kila kitu ,,,msaada mwingine nitatoa akiwa huko kwao.Na hata yeye mwenyewe aliniambia akalee mtoto wake kwao na akianza kuchangamka basi nimsaidie pesa kidogo ajishugulishe na biashara kwao..

Ila nashukuru umenishauri jambo la msingi...kuhusu kumuweka karibu na familia yangu kuanzia mwezi jana alisumbuliwa sana na tumbo na kule kwao hakuna huduma nzuri tukaamua aje huku.
Zarina, Ila Sasa akimaliza uzazi msaidie arudi kwao, pia Kama ulimpa jina lako mwambie Sasa majina ya mbele aweke ya kwao, unaweza kumsaidia mtaji akafanye mengine akiwa kwao kwa usalama wa penzi lako jitahidi kuwa mbali naye kwa Sasa na mchumba wako usimuonyeshe anafananaje Ila hiyo kukaa kwa dada yako nayo haikuwa vizuri cause atakupeleleza mengi kweli umetoa msaada Ila Kuna vitu vingi umeshakosea Kama Hilo la kumsogeza karibu na familia yako maana huwezi jua yeye na familia yake Sasa wanakuchukuliaje, kikubwa wewe jitahidi arudi kwao alafu utaendelea kumsaidia akiwa kwao.
 
Habari ya mchana,

Mwaka huu mwezi wa 1 niliingia JamiiForums. Nilikuta uzi jamaa mmoja ameuanzisha unaosema[emoji116]

Je, kuna jambo lolote ambalo hutalisahau mwaka huu 2020 ambalo limekutokea sasa!

Kila mtu ali-share jambo lake ,mimi nilishea jambo langu pia,,,kwa faida ya ambao hawakusoma ule uzi nilishea hivi[emoji116]

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi, nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba. Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu, lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.

Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani, baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu, bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.

Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa, boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha. Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga, baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.

Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha, pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.

Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo..maisha yakawa magumu kwakua hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia. Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.

Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na boda boda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo. Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa. Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.

Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili, jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe. Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.

Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa. Alijaribu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu. Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae. Alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu. Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.

Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula ,,nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu, ikiwemo na kumlipia kodi, hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kua mtoto hana baba basi jina langu lingefaa).

Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama ake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake,ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.

Kufupisha stori. Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu. Nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama .Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.

Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.

Nb: Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.

#Ndefu ila tuvumiliane

Leo 27/01/2021

Niliamka nikiwa mchovu sana kwakua wiki nzima nalala saa 6 na kuamka saa 11 alfajir ,leo nilipata nafasi ya kulala mpaka saa 3 asubuhi. Nimeamka sikua na dk wala sms kwenye simu yangu siku ilianza kwa kuboa kiukweli nikakumbuka natakiwa kwenda serikali ya mitaa ili wakanijazie fomu zangu kuna mahala nahitaji kufungua duka la dawa, nikajianda nikafika sehemu husika nikakuta ukiritimba sikufanikiwa kujaziwa masharti yalikua kibao na hela juu walikua wanataka,nikakubaliana na M/Kiti nitarudi J3. Nikiwa njiani narudi nilijikwaa sehemu mpaka nikakaa chini kwa maumivu[emoji51]. Nikaona heri nirudi nyumbani nitatoka jioni.

Nikafika home saa 5 na dk 24 asubuhi nikaona nilale. Nimekuja kuamshwa na simu saa 8 na dk 11 mchana mpigaji ni nani? Alikua ni binti aliyebeba ule ujauzito anaongea kwa furaha huku akilia "Feyzal tumepata mtoto wa kike, M/Mungu ni mwema nimefurahi sana kunivusha salama"

Baada ya hayo maneno Moyo wangu ulijawahi na furaha na machozi ya mbali yalinilenga hakika nimefurahi M/Mungu amenipa mtoto leo, hakika Mungu ni mwema. Nimeshajiandaa nampitia mama yangu ili twende tukamuone mtoto. Naombeni jina la kike zuri kwa ajili ya binti yangu tafadhali.

#There is no victory without history[emoji3059][emoji3059][emoji3059]
Oya hapo mwisho unanivuruga huyo mtoto ni wayule dada uliyemsafirisha ama ni wa mpenzi wako
 
Hongera sana broh kwa utu wako, hongera kwa wema wako, hongera kwa yote kiujumla, nakosa maneno mazuri ya kuandika kiukweli kutokana na ulicho eleza kwenye story,, ilatu mungu akujalie mafanikio zaid

"Love for all and hatred for non"
 
Watu wote wangekuwa km ww. Hii dunia ingekuwa salama sana.
Hongera, Mungu akubariki. Shemeji yako akikasirika kisa umemhudumia huyo mwanamke, ujue hauna mke hapo.
Wengine kazi kushinda msikitini na makanisani lkn wanaroho mbaya sana na wamejaa chuki muda wote.
Usichoke kumhudumia, tena ikiwezekana msimame mpaka atoboe kimaisha.
Asante sana.....Nina furaha sana na kwakua wiki iliyopita nilimrudisha Dar na yupo kwa sista yangu kazi imekua rahisi, nipo kwenye usafiri Kila mmoja ana furaha Mama amefurahi zaidi.
 
Back
Top Bottom