Mkuu hongera sana kwa kuwa na moyo wa kutoa na kusaidia, ubarikiwe sana,
Lakini sasa, kwa mpenzi wako jitahidi uwe wa kwanza kumweleza kuhusu hili, akijua mwenyewe au akiambiwa na mtu mwingine asie wewe, utapata tabu sana, narudia tena utapata tabu sana,
LA MUHIMU ZAIDI,
Endelea kumsaidia huyo binti na mtoto wake, lakini jaribu kuwa makini nae, pia nashauri ukae mbali kidogo.
Unafahamu, kwa namna ulivyomsaidia bila masharti yeye ndani anatamani kulipa fadhila japo kidogo.
Na kwa hali aliyonayo kitu pekee anaweza kulipa ni ngono. Kama atakuwa karibu na anaweza kushawishika kukutega katika hilo ili kulipa fadhira au hata kutamani kumpindua mpenzi wako akitamani hizo huduma azipate peke yake milele. Na wengi huenda mbali mpaka kutumia ushirikina. Yameshatokea sana. Yakitokea kwako utapata tabu sana.
Usitengeneze mazingira ya kumfanya atamani kulipa fadhila au kumpandisha kihisia au kumtamanisha akaanza kukutazama kwa mtazamo mwingine.
Kuna watu walitoa fadhila zikageuka madhila.