Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,076
Leo dunia inaadhimisha nguvu, busara na mchango mkubwa wa mwanamke katika kujenga jamii na mataifa. Mwanamke si tu mzazi wa kizazi, bali pia ni nguzo ya maadili, dira ya jamii na tumaini la taifa.
Mwanamke anapokuwa imara katika maamuzi yake na kusimamia haki kwa ujasiri, jamii hupata utulivu na taifa hunawiri. Lakini pia historia imetuonyesha kuwa nafasi ya mwanamke inapokuwa na changamoto au mkanganyiko wa maamuzi, athari zake huonekana kwa jamii nzima.
Ndiyo maana siku hii ni ya kutukumbusha jambo moja muhimu:
Nguvu ya mwanamke si katika nafasi anayoshika tu, bali katika hekima ya kuitumia nafasi hiyo kwa ustawi wa watu wake.
Mwanamke ana uwezo wa kujenga mazingira ya amani, kusikiliza sauti za waliokandamizwa, na kuhakikisha haki na utu wa kila mtu unaheshimiwa. Pale ambapo mwanamke anasimama imara kwa misingi ya haki na huruma, hata taifa hupata matumaini mapya.
Kwa hiyo kwa wanawake wote popote mlipo na nafasi mnazoshika kumbukeni kwamba mikononi mwenu kuna nguvu ya kubadilisha maisha ya wengi na kuacha alama nzuri katika historia ya jamii zenu.
Hongereni sana wanawake wote kwa Siku ya Wanawake Duniani.
Endeleeni kuwa nguvu ya kizazi, dira ya jamii na tumaini la taifa.
Na kama wahenga wanavyosema kwa utani kidogo:
Simamaia nafasi yako vizuri… watu wa Mungu tule mema ya nchi bhana! 😄🌸