Siku ya Sheria: Rais Magufuli azindua Mahakama inayotembea, Mfumo wa kieletroniki wa kuratibu mashauri! Asema uongozi wake hauingilii Mihimili mingine

watu wenye busara wataacha kwenda misikitini na makanisani yatakayokuwa yanaongozwa na viongozi wa ainahi, hivi hao viongozi wadini wanashandwaje kumuuliza kwanini wastaafu hawalipwi mafao yao?
 
Rais Magufuli katika maadhimisho ya wiki ya sheria anazindua mahakama inayotembea Dhana ya mahakama zinazotembea ni mahususi kwa kuwapunguzia gharama wananchi wa Tanzania,kuwapunguzia muda wa kwenda mahakamani, kuwapa uhuru wa kuweza kufanya shughuli zao na kuwapa elimu wananchi juu ya haki zao za msingi katika mahakama.

Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.
 
Lugha ya huyo Mama mwakilishi wa WB utatuletea pia???
Karibu!

Maadhimisho hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere.

Up dates;
Wageni mbalimbali wameshaingia ukumbini akiwemo Spika Ndugai pamoja na viongozi wa dini.
Mawakili na wadau wa sheria nao wamejazana kwa wingi ukumbin

Viongozi wa vyama vya siasa Chadema, Cuf, UDP na Chauma wanaonekana hapa, nawaona Mzee Cheyo, Lipumba na Dovutwa wakijadiliana jambo.i

Kwa sasa washiriki wametulia wakimsubiri mgeni rasmi mh Rais Magufuli aingie ukumbini.

Rais Magufuli ameshawasili katika viwanja vya ukumbi huu na sasa anapewa maelezo kuhusu mahakama inayotembea. Mahakama inayotembea itaanza kutoa Huduma katika mikoa ya Dsm na Mwanza, mahakama hii iko ndani ya gari ambalo lina vifaa vyote vya mahakama. Thamani ya gari hili ni zaidi ya sh 470 milioni.
Sasa mh Rais Magufuli anakata utepe kuzindua rasmi Huduma za mahakama inayotembea.
Rais Magufuli sasa ameingia ndani ya gari hilo na anapewa maelekezo ya namna kesi zitakavyoendeshwa ndani ya mahakama hiyo.

Rais Magufuli na msafara wa majaji wanaingia ukumbini tayari kuanza rasmi kwa shughuli hii.
Wimbo wa taifa ndio unapigwa sasa

MC anawatambua viongozi mbalimbali waliohudhuria ambapo mkuu wa mkoa wa Dsm amewakilishwa na mkuu wa wilaya ya Ilala bi Mjema.
Sasa ni wakati wa kusoma dua na maombezi na wa kwanza ni mwakilishi wa Mufti Abubakar aitwaye shehe Kizenga.
Sasa mwakilishi wa Kanisa Katoliki anafanya maombezi kwa ajili ya siku hii.

Padre Richard Kamenya kwa niaba ya askofu mkuu wa Anglican analiombea taifa na mamlaka zote akiwemo Rais na wasaidizi wake.

Mwakilishi wa wahindu ndio anasoma dua sasa

Mwisho ni mwakilishi wa askofu mkuu wa KKKT analiombea taifa na mahakama pamoja na Rais wetu.
Kifuatacho sasa ni wimbo maalumu wa mahakama ambao utaimbwa na watumishi wa mahakama.

Mwakilishi wa benki ya dunia sasa anatoa salamu za benki hiyo kwa mahakama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli katika maadhimisho ya wiki ya sheria anazindua mahakama inayotembea Dhana ya mahakama zinazotembea ni mahususi kwa kuwapunguzia gharama wananchi wa Tanzania,kuwapunguzia muda wa kwenda mahakamani, kuwapa uhuru wa kuweza kufanya shughuli zao na kuwapa elimu wananchi juu ya haki zao za msingi katika mahakama.

Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.
Rwanda walikua na Gachacha mobile Court sisi tumekua nchi ya pili Africa kua na Mobile court.....sasa lini madarasa ya watoto wetu au nawenyewe mtabuni mobile class rooms za magari!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli katika maadhimisho ya wiki ya sheria anazindua mahakama inayotembea Dhana ya mahakama zinazotembea ni mahususi kwa kuwapunguzia gharama wananchi wa Tanzania,kuwapunguzia muda wa kwenda mahakamani, kuwapa uhuru wa kuweza kufanya shughuli zao na kuwapa elimu wananchi juu ya haki zao za msingi katika mahakama.

Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.
Hizo zinazotembea ni mpito tu Kama mlivyozindua vituo vya polisi mobile
Mpk sasa havifanyi kazi yoyote

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa vyama vya siasa Chadema, Cuf, UDP na Chauma wanaonekana hapa, nawaona Mzee Cheyo, Lipumba na Dovutwa wakijadiliana jambo.i
Sema tu Ukweli wanajadiliana je Zitumwe kwenye M-Pesa au Zituwe kwenye A4 Envelope.
 
Back
Top Bottom