Siku ya Sheria: No mention of Tundu Lissu!, Je ni amesahaulika tu kutajwa, amepuuzwa au ameepukwa?!.

Kaka Pascal Mayalla, hotuba huendana na hadhira,muktadha na lengo. Bila shaka hakukuwa na haja wala nia ya kumtaja Rais wa TLS Lissu kwakuwa hotuba haikulenga huko. Kumleta Lissu katika jambo la leo, labda, kungeleta tafrani isiyokuwa ya lazima na kuanzisha mazungumzo yasiyotakiwa.

Nakuhakikishia, Lissu ana nafasi yake katika nchi hii. Ana umuhimu wake na hatasahaulika kirahisi kama unavyohisi au kutaka watu waamini au wajadili. Lissu anaendelea kutajwa anapotakiwa kutajwa; atasemwa anapotakiwa kusemwa. Si lazima atajwe au asemwe kila mahali au kila unapopatazama au kupasikia wewe.

Nakuhakikishia, sote wananchi wa Tanzania tunamkubali na kumkataa fulani kwa mambo yetu binafsi. Hatulazimishwi kukubaliana au kutofautiana. Nakuhakikishia, Lissu anakubalika kwa wanaomkubali (ambao hawawezi kumsahau). Pia wapo wasiomkubali na ambao hawajawahi hata kumkumbuka.
Awamu hii hata kuwa verified user JF inahitaji moyo, either ujitoe muhanga au ujitoe ufahamu kama Mselewa.

Hadhira ni nini? Ni watu, mahali, event au nini!!! Muktadha na lengo vinaweza kutofautiana na watu na event yenyewe??Ratiba ya shughuli hiyo inaonesha kuwa Rais wa TLS ambaye ni Lisu alitakiwa kutoa hotuba as per Pascal- Je, ratiba iliyomtaja Rais wa TLS haina uhusiano na event, hadhira na lengo?

No matter what!!! speech ilikuwa ianze hivi "Kwaniaba ya Rais wa TLS Mh.Tundu Antipas Lisu" ..........Kutomtaja Lisu hususani kwenye hotuba ya TLS inawezekana ni woga au hajui hata taratimu za uongozi pia ni aibu kubwa sana kwa TLS kwa sababu walipomchagua Tundu kwa kura nyingi walikuwa na akili zao timamu na utashi wao.
 
Wewe Sio mwanasheria,,,ni kanjanja, mwanasheria gani muoga na hajui kujenga hoja zaidi ya kujikomba tu,, yaani wewe kama mtu ana hamu ya kwenda jela akutumie wewe kwenye kesi yake, lazima apigwe mvua thelasini,, yaani we unaona sawa kwa huyo makamu wa TLS kushindwa kumtaja Rais wake
Ukitaka kujua kwanini serikali yetu huwa inashindwa kirahisi mahakamani basi hebu jifanye huyu naye ndio hao mawakili wa serikali ndio utapata jibu.
 
Hujaelewa, soma tena. Usiwe unakurupuka tu kwa nia ya kupinga. Uwe unasoma, kutafakari na kuchangia ukiwa umeelewa.
Umekuwa "Kunguru" Sana ndugu...

Hivi umewahi kwenda kwenye hadhara Fulani kumuwakilisha mhusika yeyote ambaye ni Mkubwa wako kikazi hapo kwenye hiyo Taasisi iliyokuajiri?

Na Je umewahi kuhudhuria hadhara ambayo muhusika mtajwa katika ratiba hajahudhuria kwa sasabu zozote zile ila akawakilishwa na mtu mwingine?
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kuangalia sherehe za maadhimisho wa siku ya sheria zilizokuwa zikitangazwa live na TBC. ...
Pamoja na kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa na yuko hospitalini, bado yeye ndie rais halali wa TLS!. Kuumwa hakumfanyi Tundu Lissu asiwe rais wa TLS, hivyo he was worth mentioned, na kutakiwa uponyaji wa haraka!.

Get Well Tundu Lissu, pole sana, umesahaulika mapema!.

Paskali
Paskali katika ubora wako na mada zenye hoja tatanishi. Mimi naamini kutokutajwa kwa Lissu leo katika hotuba zote kutokana na jinsi shambulio lake lilivyotekwa kisiasa. Na si hilo tu hata matibabu yake na upelezi wa tukio umeghubikwa na mtazamo wa kisiasa.
 
Kaka Pascal Mayalla, hotuba huendana na hadhira,muktadha na lengo. Bila shaka hakukuwa na haja wala nia ya kumtaja Rais wa TLS Lissu kwakuwa hotuba haikulenga huko. Kumleta Lissu katika jambo la leo, labda, kungeleta tafrani isiyokuwa ya lazima na kuanzisha mazungumzo yasiyotakiwa.

Nakuhakikishia, Lissu ana nafasi yake katika nchi hii. Ana umuhimu wake na hatasahaulika kirahisi kama unavyohisi au kutaka watu waamini au wajadili. Lissu anaendelea kutajwa anapotakiwa kutajwa; atasemwa anapotakiwa kusemwa. Si lazima atajwe au asemwe kila mahali au kila unapopatazama au kupasikia wewe.

Nakuhakikishia, sote wananchi wa Tanzania tunamkubali na kumkataa fulani kwa mambo yetu binafsi. Hatulazimishwi kukubaliana au kutofautiana. Nakuhakikishia, Lissu anakubalika kwa wanaomkubali (ambao hawawezi kumsahau). Pia wapo wasiomkubali na ambao hawajawahi hata kumkumbuka.
Inawezekana unatetea kibarua chako ila kukaa kimya ingesaidia sana na ungewatendea haki hata wale wanaokuamini hasa walimu wako.
Hivi kweli ndugu yetu hujaelewa kinachomaanishwa kweli au makusudi tu? Ngoja niamini umeteleza tu ila hukukusudia hivyo na utarekebisha ili hii thread isionekane UCHWARA.
 
Hivi kwa ile tu ' body language ' ya Kiuwoga aliyokuwa nayo Makamu Rais wa TLS na vile alivyokuwa ' akitetemeka ' na ' kujiumauma ' huku akituchanganyia Kiingereza chake cha ' hapa na pale ' ulitegemea kabisa angethubutu kumzungumzia Bosi wake ambaye hivi sasa ni Mgonjwa Mheshimiwa Mbunge Tundu Antipas Lissu?

Kamarada Wewe nakujua ni mwana Mawasiliano mwenzangu tena ' mbobezi ' kabisa na nina uhakika katika Masomo yako ya Mawasiliano ( Communication ) ulifanya Somo zuri la ama Psychology au Communication Psychology hivyo nilitegemea kwamba ungeshagundua huo ' udhaifu ' ambao umeusema Kwetu.

Nimalizie tu kwa kutoa maoni yangu kwamba Kiutamaduni wa Kitanzania tuliorithishwa na akina Hayati Nyerere na Karume hata kama Watu tuna Uadui wa kiasi gani lakini pale ambapo Mtanzania mwenzetu akiwa na matatizo basi yatupasa kushirikiana nae au basi kama tupo mbali nae tuweze kumkumbuka na kumpa Heshima yake.

Kilichofanywa leo hasa na huyo Makamu Rais wa TLS ni dharau kubwa na kali sana isiyovumilika aliyomfanyia Tundu Lissu na hata Wanasheria wenzake wengi na binafsi bila unafiki au itikadi yangu ya Kisiasa nadhani kutotajwa kwa Tundu Lissu ama na Rais mwenyewe JPM au huyo Makamu Rais wa TLS ni jambo baya sana na nadhani sasa Siasa za Tanzania zinaelekea kubaya.

Yangu ni hayo tu.
Baada ya kusoma comment yako sitachangia maana umemaliza kila kitu, acha nibaki mpenzi msomaji.
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kuangalia sherehe za maadhimisho wa siku ya sheria zilizokuwa zikitangazwa live na TBC. Chama cha wanasheria ni mdau muhimu wa maadhimisho haya ambayo huhutubiwa na rais wa chama hicho. Kwa vile rais wa TLS ni Tundu Lissu, na ameshindwa kuhudhuria kutokana na kuwa mgonjwa, jina la Tundu Lissu, halikutajwa popote!. Swali la kujiuliza, ni kutotajwa huku kutokana na kusahaulika tuu, Lissu amepuuzwa as if he doesn't exist, or ameepukwa kutajwa kwa makusudi?.

Kwenye ratiba ya maadhimisho hayo, kulionyesha kuna mahali rais wa TLS, angepaswa kutoa salamu. Kwa vile rais wa TLS, Mhe. Tundu Lissu, ni mgonjwa kwa shambulio la risasi, aliyekuja kuzungumza nafasi ya rais wa TLS, ni Makamo rais wa TLS, nikitegemea, alipoanza kuzungumza, kwa vile aliyepaswa kuzungumza sii yeye ni rais wa TLS, hivyo anaongea kwa niaba ya rais wa TLS, then, kistaarabu tuu, alipaswa kusema anazungumza kwa niaba ya rais wa TLS ambaye ni mgojwa. Huyu Makamo rais wa TLS, aliposimama kuzungumza, alisimama na kujitaja kuwa anazungumza kwa niaba yake!. Ratiba inasema mzungumzaji ni rais wa TLS, wewe sio rais wa TLS, unasimama kuzungumza badala ya rais wa TLS, ilibidi kumtaja rais wa TLS as an excuse ndipo uendelee!.

Naibu Spika, Tulia Akson, amemuwakilisha Spika ametajwa kuwa yupo anamuwakilisha spika. Naibu DPP ametajwa kumwakilsha DPP, Naibu Mwanasheria Mkuu ametajwa kumwakilisha Mwanasheria Mkuu, kwa nini huyu Makamo rais wa TLS akajitaja yeye ili hali kwenye ratiba aliyeandikwa ni rais wa TLS.

Aliposimama mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, naye katika maelezo yake, akamtaja rais wa TLS na kujikwaa, akamtaja Makomo rais wa TLS.

Huku kutotajwa kabisa kwa rais wa TLS, Tundu Lissu. ni oversight tuu ya kusahaulika, au ni omission kuwa Tundu Lissu asitajwe popote.

Rais katika hotuba yake, akatoa pole kwa mhimiliwa mahakama kwa kifo cha Jaji Robert Kisanga ambaye aliishastaafu siku nyingi, kama mtu aliishastaafu siku nyingi na kufariki, mhimili huu unapewa pole, vipi kuhusu shambulio la rais wa TLS ambaye hadi sasa anauguza majereha ya shambulizi, hatajwi popote, wala hata kumtakia uponywaji wa haraka!.

Amini usiamini, kama Tundu Lissu, angekufa kwa shambulio lile, hotuba ya TLS ingemtaja, na kile aliyehutubia, angetoa pole kwa TLS kwa kuondokewa na rais wake, lakini kwa vile Lissu yuko hai, amenusurika, hadi marehemu wastaafu wanapewa pole, lakini walio hai wanaohitaji kuombewa tuu uponyaji wa haraka, wamesahaulika, kama sio kuepukwa!.

Kama huku sio kusahaulika, bali ni kuepukwa, then bandiko hili, ndio taarifa ya awali, kuwa urais wa Tundu Lissu kwenye TLS, unaofikia kikomo miezi miwili ijayo, Mwezi April, 2018, wanasheria watakutana na kumfuta rasmi kazi Tundu Lussu kama rais wa TLS, na inawezekana kabisa, jina la Tundu Lissu likaingia kwenye kumbukumbu za TLS kuwa Tundu Lissu ndie rais wa TLS ambaye he did almost nothing, tangu achaguliwe, kwa kudumu kwa miazi mitatu tuu TLS, ba baada ya hapo, akashambuliwa, hivyo kumaliza Kipindi chake chote cha urais akiwa hospitalini.

Pamoja na kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa na yuko hospitalini, bado yeye ndie rais halali wa TLS!. Kuumwa hakumfanyi Tundu Lissu asiwe rais wa TLS, hivyo he was worth mentioned, na kutakiwa uponyaji wa haraka!.

Get Well Tundu Lissu, pole sana, umesahaulika mapema!.

Paskali
Amechagua kusahaulika.
 
Yericko Nyerere umeeleweka vizuri tu wala hakuna anayezuia mitandao ya kijamii Tanzania ....tatizo la vijana wengi katika mitandao ni matusi tu hilo ndiyo tatizo kubwa.Tunalinganisha nchi yetu na nchi zingine kumbuka maadili yanatofautiana sana.

Sisi hapa huwezi kutembea beach baba,mama na watoto wamevaa chupi na hata nyumbani kwako tu lakini kuna nchi hayo yanafanyika tu.

Tumeona Marekani jinsi wanavyomtukana Rais wao Trump tena matusi mabaya kabisa lakini anayekamatwa vitu ambavyo kwa maadili yetu ni ngumu sana.

Hakuna anayeshughulikiwa kwa kuikosoa Serikali mara nyingi hapa ni huo utoaji wwa taarifa je ndiyo channel yake mara nyingi huwa naona hapo ndipo penye mkanganyika...lakini serikali inakoselewa tu tena sana ndiyo tunaziita changamato ambazo ndizo zinafanya watua wafanaye kazi kila kukicha.
Matusi ni nini hasa, Je ni kuyasikia usiyopenda kuyasikia ?! Mkiambiwa muainishe hayo matusi aliyotukanwa mkuu wala huwezi kufanya. Kinachomkera mkuu ni kutokutaka madhaifu yake na ya serikali yake kuwekwa wazi na kutamkwa wazi wazi.
e.g. - Waliposema serikali inaminya uhuru wa watu kujieleza. Je si kweli ?!
- Waliposema ndege yetu imeshikwa kwa sababu deni lililosababishwa waziri wa ujenzi wa wakati huo. Je huo ni uongo ?!
- Je watu walipohoji uhalali wa PhD. Wapo ? Wamepotezwa
_ Mkuu unapozuia wabunge wenye mawazo mmbadala kikatiba kuikosoa serikali bungeni ili watoke nje uwashughulikie, na kweli wanashugulikiwa. Je nauliza huo ndiyo uhuru unauuzungumzia ?!
Imefikia wabunge karibu wote wa upinzani wa kesi za uchochezi ktk mahakama zetu. Je huo ni huo ndiyo uongozi, tunautaka ndani ya vyama vingi vilivyopo kikatiba ?! Wakafanye kazi zao wapi ?! Kama bungeni hapana na majimboni pia hapana !!!

Katiba yetu ina shida kwa watu wanaoitwa D.C. na OCD kutumia mamlaka waliopewa vibaya kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi. Lakini boss anasema si kipaumbele chake. Nani wa kuhoji kama si wabunge walionyamazishwa ?!
Kwani angetajwa ndio Yesu angashuka?
Ona akili kama hii.
Pole !! Hukumuelewa Pasco
 
Kaka Pascal Mayalla, hotuba huendana na hadhira,muktadha na lengo. Bila shaka hakukuwa na haja wala nia ya kumtaja Rais wa TLS Lissu kwakuwa hotuba haikulenga huko. Kumleta Lissu katika jambo la leo, labda, kungeleta tafrani isiyokuwa ya lazima na kuanzisha mazungumzo yasiyotakiwa.

Nakuhakikishia, Lissu ana nafasi yake katika nchi hii. Ana umuhimu wake na hatasahaulika kirahisi kama unavyohisi au kutaka watu waamini au wajadili. Lissu anaendelea kutajwa anapotakiwa kutajwa; atasemwa anapotakiwa kusemwa. Si lazima atajwe au asemwe kila mahali au kila unapopatazama au kupasikia wewe.

Nakuhakikishia, sote wananchi wa Tanzania tunamkubali na kumkataa fulani kwa mambo yetu binafsi. Hatulazimishwi kukubaliana au kutofautiana. Nakuhakikishia, Lissu anakubalika kwa wanaomkubali (ambao hawawezi kumsahau). Pia wapo wasiomkubali na ambao hawajawahi hata kumkumbuka.

Urudi kufundisha shule ya msingi ile ulikua unafundisha zamani
 
Back
Top Bottom